Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Pentekoste

Roho Mtakatifu ni paji la Mungu. Anatakasa, anahuisha, anatakasa Kanisa na ni Sakramenti ya umoja wa Utatu Mtakatifu na wa watu.

Roho Mtakatifu ni paji la Mungu. Anajenga, anahuisha na kulitakasa Kanisa; ni Sakramenti ya umoja wa Utatu Mtakatifu na wa watu!

Sherehe ya Pentekoste, kuzaliwa kwa Kanisa!

16/05/2018 15:44

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima: atokaye kwa Baba na Mwana. Anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana: aliyenena kwa vinywa vya Manabii. Hii ndiyo imani ya Kanisa juu ya Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu; Sakramenti ya Umoja!

 

Mkesha wa Siku kuu ya Pentekoste kwa Mwaka 2017 umekuwa ni muda wa sala ya kiekumene, tafakari na shuhuda mbali mbali.

Mkesha wa Sherehe ya Pentekoste kwa mwaka 2017 imekuwa ni fursa ya sala ya kiekumene, tafakari makini ya Neno la Mungu na shuhuda kuhusu maisha na utume wa Kanisa kadiri ya karama za Roho Mtakatifu.

Mkesha wa kiekumene umekuwa ni muda wa sala, tafakari, toba na sherehe

04/06/2017 15:37

Mkesha wa Sherehe ya Pentekoste kwa Mwaka 2017 kwenye Uwanja wa Circo Massimo mjini Roma, imekuwa ni fursa ya kujikita katika sala ya kiekumene, tafakari makini ya Neno la Mungu; ushuhuda wenye mvuto na mashiko pamoja na kumwimbia Roho Mtakatifu utenzi wa sifa na shukrani kwa mapaji yake!

Sherehe ya Pentekoste imekuwa ni fursa kwa Kanisa kusali kwa ajili ya mahitaji ya familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia.

Sherehe ya Pentekoste imemkuwa ni fursa ya kusali kwa ajili ya kuombea mahitaji ya familia ya Mungu, sehemu mbali mbali za dunia!

Sala ya Kanisa kwa ajili ya mahitaji ya familia ya Mungu!

04/06/2017 14:36

Katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Sherehe ya Pentekoste kwa Mwaka 2017, Waamini wamesali kwa ajili ya kuliombea Kanisa, viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa ili waweze kutafuta na kudumisha misingi ya haki na amani ya kweli, wamewakumbuka waamini wanaoteseka pia!

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki Duniani kinaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake!

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki, Wakarisimatiki Wakatoliki, kinaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza kwa kuendelea kuwa ni "majembe ya nguvu" katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene.

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki ni jembe la uekumene duniani!

02/06/2017 16:18

Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki Duniani ni muda wa sala, tafakari, makongamano, toba na wongofu wa ndani, tayari kuandika ukurasa mpya wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika huduma, damu, maisha ya kiroho na sala!