Patriaki Tawadros II nchini Misri amemtumia matashi mema ya Pasaka,Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya Video akisisitiza kuwa,Kristo amefufuka kweli kweli Kafufuka.Wakati huo huo hata matashi mema kwa ajili ya kutimiza miaka mitano tangu kuchaguliwa kwake kama kharifa wa Mtume Petro!
Papa Francisko ni shuhuda na chombo cha majadiliano ya kiekumene kinachowawezesha Wakristo kutembea, kusali na kufanya kazi katika umoja kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia.
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Machi 2018 anaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 5 tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kwa kulitaka Kanisa kujielekeza zaidi katika: huduma kwa maskini kama amana na utajiri wa Kanisa; Amani na Utunzaji Bora wa Mazingira bila kusahau Uekumene!
Patriaki Tawadros II: Jifunzeni unyenyekevu wa watoto wadogo, toba, wongofu wa ndani, ukweli na uwazi; hekima na busara ili kudumisha haki, amani na maridhiano kati ya watu duniani.
Patriaki Tawadros II wa Kanisa la Kiorthodox la Kikoptik nchini Misri katika ujumbe wake kwa familia ya Mungu katika maadhimisho ya Sherehe ya Noeli kwa Mwaka 2018 anawataka waamini kujenga na kudumisha fadhila ya toba na wongofu wa ndani; ukweli na uwazi; hekima na busara, ili kudumisha amani!
Viongozi mbali mbali wamelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika tarehe 29 Desemba 2017 huko Misri na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.
Viongozi mbali mbali wa kidini na kisiasa wamelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa huko mjini Helwan na Cairo, nchini Misri na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya. Vitendo vya kigaidi ni kinyume kabisa cha mafundisho ya dini na ni ukatili dhidi ya binadamu!
Viongozi mbali mbali wa Makanisa na Jamii wanalaani majuaji ya kigaidi yaliyotokea huko Misri
Baba Mtakatifu Francisko anaungana na viongozi mbali mbali wa Makanisa kulaani kwa nguvu zote kitendo cha kigaidi kilichopelekea mauaji ya watu 28 kuuwa kikatili na wengi wao walikuwa ni watoto waliokuwa wanakwenda kusali. Anaombe mchakato wa haki, amani na maridhiano nchini Misri.
Papa Francisko amemwandikia ujumbe Papa Tawadros II akikazia: umuhimu wa Ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi, umoja na mshikamano; udugu na urafiki ili siku moja waweze kuwa na umoja kamili.
Baba Mtakatifu Francisko anasema, tarehe 10 Mei ya kila mwaka sasa ni Siku ya Urafiki kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kikoptik la Alexandria nchini Misri. Ni wakati wa kuendelea kuimarisha kifungo cha Sakramenti ya Ubatizo, Umoja na Udugu miongoni mwa Wakristo ili kuwa na umoja kamili.
Papa Francisko alipokuwa anarejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume nchni Misri tarehe 29 Aprili 2017 alipata nafasi ya kuchinga na waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya kitaifa na kimataifa.
Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija ya kitume ambayo imeacha "gumzo kubwa" nchini Misri amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu: majadiliano, diplomasia, amani, wahamiaji, majadiliano ya kidini na kiekumene; na umuhimu wa ushuhuda!
Baba Mtakatifu Francisko na Papa Tawadros II wametia sahii katika tamko la pamoja kuhusu mchakato wa majadiliano ya kiekumene katika sala na maisha ya kiroho; katika damu na huduma makini kwa watu wa Mungu.
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake ya kitume nchini Misri ametia sahihi tamko la pamoja na Papa Tawadros II wa Kanisa la Kikoptik la Misri juu ya umuhimu wa kuendeleza majadiliano ya kiekumene yanayojikita katika sala na maisha ya kiroho; katika damu na huduma makini kwa watu wa Mungu!
Mitandao ya kijamii: