Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Patriaki Bartolomeo I

Toba na wongofu wa ndani ni muhimu katika utunzaji wa mazingira kwani uharibifu na uchafuzi wa mazingira ni dhambi!

Toba na wongofu wa ndani ni muhimu katika kulinda, kutunza na kudumisha mazingira nyumba ya wote na kwamba, uchafuzi na uharibifu wa mazingira ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Toba na wongofu wa kiekolojia ili kutunza mazingira nyumba ya wote!

08/03/2018 10:00

Viongozi wa Makanisa wanasema, kuna haja ya kutubu na kuwa na wongofu wa kiekolojia; kwa kumwilisha mahubiri na sala katika uhalisia wa maisha, ili kulinda, kutunza na kudumisha mazingira nyumba ya wote, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi! Uharibifu wa mazingira ni dhambi!

Kwaresima ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; upendo na mshikamano unaomwilishwa katika ushuhuda wa imani.

Kwaresima ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; upendo na mshikamano unaomwilishwa katika ushuhuda, kielelezo makini cha imani tendaji!

Kwaresima ni kipindi cha upendo na mshikamano; toba na wongofu!

17/02/2018 06:40

Patriaki Bartolomeo wa kwanza katika ujumbe wake wa Kwaresima kwa Mwaka 2018 anasema, Kwaresima ni kipindi cha upendo na mshikamano wa kikanisa na kijamii; ni muda muafaka wa toba na wongofu wa ndani kwa kujikita katika liturujia ya Kanisa inayoshuhudiwa katika uhalisia wa maisha!

Waamini wa dini mbali mbali wanapaswa kushikamana kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano na utunzaji bora wa mazingira.

Waamini wa dini mbali mbali wanapaswa kushirikiana kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano na utunzaji bora wa mazingira.

Patriaki Bartolomeo I: waamini wa dini mbali mbali dumisheni umoja!

02/01/2018 07:23

Patriaki Batolomeo wa kwanza anasema, mshikamano wa kweli ni msingi madhubuti wa tunu bora za maisha ya kijamii yanayofumbatwa katika: uhuru wa kweli, upendo, haki na amani. Hizi ni nguzo za kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu dhidi ya kinzani, mipasuko na misimamo mikali ya kidini!

Vijana wanakumbushwa kwamba, wao ni mahujaji wanaopaswa kuwajibika katika mchakato wa kuleta mageuzi ulimwenguni.

Vijana wanakumbushwa kwamba, wao ni mahujaji hapa duniani wanaopaswa kuwajibika katika mchakato mzima wa mgeuzi hapa duniani, ili ulimwengu uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi.

Wakristo ni mahujaji wanaopaswa kuwajibika kikamilifu katika maisha

31/12/2017 14:11

Vijana wanapaswa kuwa makini katika kila hatua ya maisha wanayopiga kama sehemu ya mchakato wa ukuaji na ukomavu katika maisha yao ya kiroho na kimwili, tayari kushiriki kikamilifu  katika mchakato wa maboresho ya ulimwengu huu ili uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi!

Ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kutoka kwa Patriaki Bartolomeo wa kwanza: haki msingi za binadamu, amani, uhuru, upendo, mshikamano na majadiliano!

Ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kutoka kwa Patriaki Bartolomeo wa kwanza: haki msingi za binadamu, amani na uhuru wa kweli; mshikamano na utunzaji bora wa mazingira; maridhiano; majadiliano na ushirikiano!

Ujumbe wa Noeli kutoka kwa Patriaki Bartolomeo wa kwanza!

21/12/2017 13:54

Patriaki Bartolomeo wa kwanza katika ujumbe wake wa Noeli kwa Mwaka 2017 anakazia: haki msingi za binadamu; amani na uhuru wa kweli; upendo na mshikamano wa dhati sanjari na utunzaji bora wa mazingira kwa kutambua kwamba, binadamu wanapaswa kushirikiana ili kukamilishana katika hija yao!

Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I amejikita kwa muda mrefu katika kuhamasisha na kutafuta suluhisho la kipeo cha mazingira ya sayari hii tunamoishi

Patriaki wa kiekumeni Bartolomeo I amejikita kwa muda mrefu katika kuhamasisha na kutafuta suluhisho la kipeo cha mazingira ya sayari hii tunamoishi.

Patriaki Bartolomeo I anatoa wito wa ukarimu ambao ni zawadi

07/09/2017 16:10

Mungu ni mwajibikaji kwa ajili ya kazi yake ya uumbaji ambayo amemkabidhi binadamu kutunza kila kiumbe kwa jina lake.Ni maneno ya Patriaki Bartolomeo I. Anabainisha kuwa kuongea juu ya ukarimu kwa watu walio wengi ni bigudha wakati huo ukarimu ni zawadi kutoka kwa Mungu na tuliyoiokea

 

 

Papa Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza wanawasihi viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kusikiliza kilio cha maskini.

Papa Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza wanawasihi viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kuwasikiliza kwa makini maskini wanaoathirika kutokana na uharibifu wa mazingira!

Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira, 2017

30/08/2017 15:35

Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox katika maadhimisho ya Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira kwa Mwaka 2017 inayoadhimishwa tarehe 1 Septemba, wameandika ujumbe kuwasihi viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kusikiliza sauti ya maskini!

Kuanzia tarehe 1 Sept- 4 Okt ni kipindi cha kaadhimisha  Siku ya Dunia ya Sala ya Kuombea Huduma ya viumbe na mazingira iliyowekwa na Papa Francisko

Kuanzia tarehe 1 Sept- 4 Okt ni kipindi cha kaadhimisha Siku ya kuombea utunzaji bora wa mazingira mwaka 2017 iliyowekwa na Baba Mtakatifu Francisko 2015 kwa waraka wa Sifa kwa Bwana.

Siku ya Kuombea utunzaji bora wa mazingira mwaka 2017

29/08/2017 15:05

Tarehe1Septemba ilitangazwa kuwa ni Siku ya Dunia ya sala ya Kuombea Huduma kwa viumbe,kwa upande wa Kanisa la Kiotodosi  ilitangazwa tangu 1989, kwa njia hiyo hata makanisa mengine pamoja na  Baba Mtakatifu Francisko wameungana kwa pamoja hivi karibuni mwaka 2015.