Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Perù: Lima, Puerto Maldonado & Trujillo

Maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia yaanza kushika kasi mjini Vatican.

Maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia yaanza kushika kasi mjini Vatican.

Maandalizi ya Sinodi ya Amazonia yaanza kushika kasi!

13/04/2018 15:23

Maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia itakayofanyika mwezi Oktoba 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu "Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa ajili ya ekolojia endelevu" yameanza kutimua vumbi mjini Vatican kwa uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira duniani wanaendelea kupukutika kama majani makavu kutokana na ukoloni mamboleo!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira wanaendelea kupukutika kutokana na vita ya ukoloni mamboleo inayoendeshwa kichini chini!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira duniani wanavyopukutika!

07/03/2018 07:29

Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wake wa kitume "Laudato si" anaitaka familia ya Mungu duniani kusimama kidete kulinda, kutetea, kutunza na kuendeleza mazingira nyumba ya wote ili kukuza na misingi ya haki, amani, usawa, utu na heshima ya binadamu wote pasi na ubaguzi!

Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia: Kuibua sera na mbinu mkakati wa uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji msingi ya binadamu: kiroho na kimwili.

Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia: Lengo kuu ni kuibua sera na mbinu mkakati utakaosaidia mchakato wa Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Sinodi ya Amazonia: Sera na mikakati ya maendeleo inayofumbata Injili

28/02/2018 07:00

Baba Mtakatifu Francisko ameitisha Sinodi ya Maaskofu wa Ukanda wa Amazonia itakayoadhimishwa mwaka 2019. Lengo ni kuliwezesha Kanisa kuibua mbinu mkakati wa shughuli za kichungaji zitakazosaidia kudumisha utu, heshima, ustawi na maendeleo ya wengi, binadamu akipewa kipaumbele!

 

Papa Francisko asikitishwa sana na vurugu zinazoendelea huko nchini DRC na kuwataka wahusika kurejesha utawala wa sheria na demokrasia.

Papa Francisko asikitishwa na uvunjifu wa misingi ya haki, amani na maridhiano nchini Congo DRC na kuwataka viongozi wa Serikali kurejesha utawala wa sheria na demokrasia.

Papa Francisko asikitishwa na mateso ya wananchi wa DRC

22/01/2018 15:33

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jimbo kuu la Lima, nchini Perù ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na vurugu na uvunjaji wa haki msingi za binadamu unaoendelea nchini Jamhuri ya Watu wa Congo na kuwataka viongozi wa serikali kurudisha utawala wa sheria na haki,

Papa Francisko: Watakatifu ni mashuhuda wa imani, huruma, mapendo na matumaini ya watu wa Mungu.

Papa Francisko: Watakatifu ni mashuhuda wa imani, matumaini na mapendo ya watu wa Mungu kwa Kristo na Kanisa lake.

Papa: Watakatifu wa Mungu ni mashuhuda wa imani, upendo na matumaini!

22/01/2018 15:10

Kanisa nchini Perù limekuwa ni maabara ya kuzalisha watakatifu Amerika ya Kusini. Hawa ni watu waliokita maisha yao katika sala, toba na wongofu wa ndani; wakawa tayari kushuhudia huruma, upendo, imani na matumaini yanayobubujika kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake! Waaminifu wa Injili.

Bikira Maria ni mlango wa mbingu, ni mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu.

Bikira Maria ni mlango wa mbingu, ni mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu.

Papa Francisko: Bikira Maria ni mlango, Mama wa huruma na matumaini

21/01/2018 15:18

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Bikira Maria ni mlango wa mbinguni, nyota ya asubuhi; ni Mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu ambaye kimsingi ni Lango la Huruma ya Mungu. Familia yote ya Mungu inapata utambulisho wake kwa Bikira Maria, Mama wa wote!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na furaha ya utambuzi binafsi; mwaliko wa wito wao na kushirikisha furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na utambuzi binafsi wa wito wao; kutambua na kuthamini mwaliko wa maisha na utume wao pamoja na kuhakikisha kwamba, wanawashirikisha wengine ile furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Wakleri na watawa: zingatieni: utambuzi binafsi, mwaliko na furaha!

21/01/2018 14:05

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kukazia ile furaha ya utambuzi wa mtu binafsi kile anachotenda; pili watambue na kuthamini muda wa mwaliko wa kumfuasa Kristo kwani hii ni kumbu kumbu endelevu katika kumfuasa Kristo na kwamba, wajitahidi kushirikisha furaha ya Injili.

Papa: Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini ili kupambana na uharibifu mkubwa kwa mazingira nyumba ya wote!

Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini dhidi ya uharibifu wa mazingira nyumba ya wote!

Papa Francisko: Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini

20/01/2018 11:54

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wazazi, walezi na wadau mbali mbali wanaojisadaka kwa ajili ya huduma makini kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi kuhakikisha kuwa, wanawezekeza zaidi katika sekta ya elimu itakayowasaidia kuheshimu mazingira, mila na desturi njema.