Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa: Miaka 70 WCC: Kutembea, Kusali na Kazi

Yaliyojiri wakati wa mahojiano kati ya Papa Francisko na Waandishi wa Habari wakiwa njiani kutoka Geneva, Uswiss, 21 Juni 2018.

Yaliyojiri katika mahojiano maalum kati ya Papa Francisko na waandishi wa habari wakati akiwa njiani kutoka Geneva Uswiss, tarehe 21 Juni 2018.

Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Papa Francisko na Wanahabari!

23/06/2018 16:00

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hija yake ya kiekumene nchini Uswiss imemwezesha kukutana na viongozi mbali mbali wa Kanisa wanaoendelea kujizatiti kwa ajili ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika kutembea, kusali na kushirikiana kama ushuhuda wa uinjilishaji mpya!

Papa Francisko amewaishukuru kwa dhati familia ya Mungu nchini Uswiss kwa mapokezi na ukarimu wake!

Papa Francisko ameishukuru kwa dhati familia ya Mungu nchini Uswiss kwa mapokezi maito na ukarimu wao kwake na kuwataka waendelee kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene!

Papa Francisko aonesha moyo wa shukrani nchini Uswiss!

22/06/2018 17:12

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anarejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kiekumene nchini Uswiss, ameishukuru familia ya Mungu nchini humo kwa mapokezi makubwa na moyo wa ukarimu, akawatakia wananchi wa Italia, heri, baraka na ustawi, baada ya kukutana mahujaji wa kiekumene!

Majadiliano ya kiekumene: Ushuhuda wa kiinjili; huduma kwa maskini na changamoto mamboleo.

Majadiliano ya kiekumene: Ushuhuda wa Injili, huduma kwa maskini na wanyonge pamoja na mshikamano katika kupambana na changamoto mamboleo.

Jubilei ya Miaka 70 Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Ushuhuda na huduma

19/06/2018 14:37

Majadiliano ya kiekumene ni mchakato unaotaka kuratibu tofauti za Makanisa katika: uelewa wa kitaalimungu, kiliturujia na kitasaufi, ili kuwa na mwelekeo mpya utakaosaidia kuganga na kuponya majereha yaliyosababisha mpasuko wa Kanisa, tayari kushikamana ili kushuhudia kweli za Kiinjili kwa pamoja!

Waraka wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni uko tayari kuwakilishwa katika Mkutano Kuu utakao fanyika mjini Geneva 21 Juni 2018

Waraka wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni uko tayari kuwakilishwa katika Mkutano Kuu utakao fanyika mjini Geneva 21 Juni 2018

Waraka wa Baraza la Makanisa duniani uitwao,tunaitwa kubadili matendo!

04/06/2018 13:08

Shirikisho la Kiluteri duniani na Shirikisho la mshikamano wa matendo na Baraza la Kiekumene la Makanisa watia saini kwa Waraka  uitwao:Tunaitwa kubadili matendo. Ushemasi wa kiekumeni. ni Waraka ambao utawakilishwa katika kamati kuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni mjini Geneva. 

 

 

Roho Mtakatifu awajalie waamini kutafuta, kulinda na kudumisha haki, amani na maridhiano kati ya watu.

Roho Mtakatifu awajalie waamini kutafuta, kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu ili wote waweze kuwa na roho moja na moyo mmoja.

Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Ujumbe wa Pentekoste kwa Mwaka 2018

19/05/2018 09:04

Baraza la Makanisa Ulimwenguni katika ujumbe wake kwa Sherehe ya Pentekoste kwa mwaka 2018 linamwomba Kristo Mfufuka, anayewajalia waja wake maisha mapya, awawezeshe kusimama kidete kutafuta, kulinda na kudumisha haki, amani na maridhiano, ili waweze kuwa na roho moja na moyo mmoja.

Uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko katika Jubilei ya miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni ni zawadi kwa Makanisa!

Uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye Jubilei ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni ni zawadi kubwa kwa Makanisa!

Papa Francisko ni zawadi kwa Makanisa katika majadiliano ya kiekumene

16/05/2018 08:40

Nembo na kauli mbiu inayoongoza hija ya kiekumene ya Baba Mtakatifu Francisko mjini Geneva nchini Uswiss, tarehe 21 Juni 2018 inakazia umuhimu wa Makanisa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kama muhtasari wa dhamana na malengo makuu ya majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa!

Papa Francisko tarehe 21 Juni 2018 anashiriki katika kumbu kumbu ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni.

Papa Francisko tarehe 21 Juni 2018 anashiriki katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni.

Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Papa kushiriki, 21 Juni!

08/05/2018 15:04

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa hapo tarehe 21 Juni 2018 kushiriki kikamilifu katika kumbu kumbu ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Atashiriki sala ya kiekumene, mkutano na viongozi wa Makanisa pamoja na kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu.

Makanisa ulimwenguni yanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa: uinjilishaji, utamadunisho na haki msingi za binadamu.

Makanisa ulimwenguni yanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa uinjilishaji na utamadunisho; haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.

Makanisa Ulimwenguni yawe ni: vyombo vya haki, amani na upendo!

13/03/2018 08:10

Mkutano mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni uliokuwa unatimua vumbi kwenye kilima cha Ngurdoto, Jijini, Arusha Tanzania kuanzia tarehe 8 -13 Machi 2018 imekuwa ni nafasi murua kwa Makanisa kusali, kutafakari na kushirikishana changamoto na vipaumbele katika mchakato wa uinjilishaji kwa nyakati hizi!