Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Francisko: Wosia: Furahini na kushangilia

Kardinali Parolin anawataka wananchi wa Serbia na Montenegro kudumisha majadiliano ya kidini, kiekumene na utakatifu wa maisha!

Kardinali Parolin anawataka wananchi wa Serbia na Montenegro kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kiekumene pamoja na utakatifu wa maisha!

Yaliyojiri katika ziara ya Kardinali Parolin nchini Montenegro & Serbia

04/07/2018 14:55

Kardinali Pietro Parolin, katibu mkuu wa Vatican kuanzia tarehe 27 Juni hadi tarehe Mosi, Julai 2018 ametembelea nchini Montenegro na Serbia. Amefurahishwa na uhusiano wa kidiplomaisha kati ya nchi hizi mbili; amekazia: majadiliano ya kiekumene na kidini ili kudumisha haki, amani na maridhiano.

 

Papa Francisko: Simameni kidete kupambana na utamaduni wa kifo, utumwa mamboleo na biashara haramu ya binadamu.

Papa Francisko: Simaneni imara kupambana na utamaduni wa kifo, biashara haramu aya binadamu na utumwa mamboleo.

Papa Francisko shikamaneni kupambana na utumwa mamboleo!

15/06/2018 07:28

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo; mambo yanayoendelea kunyanyasa utu, heshima na haki msingi ya binadamu sehemu mbali mbali za dunia.

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu: Ni Siku ya Kuombea Toba, Wongofu na Utakatifu wa Mapadre duniani.

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu: Siku ya Kuombea: Toba, Wongofu na Utakatifu wa Maisha ya Mapadre Duniani.

Siku ya Kuombea Wongofu na Utakatifu wa Mapadre Duniani 2018

07/06/2018 10:22

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kukuza na kudumisha Ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, chemchemi ya huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu! Anawahimiza kusali, kuwaombea na kuwasindikiza Mapadre wao katika utakatifu wa maisha!

Chama cha Waamini Walei wa Mtakatifu Petro ni wamisionari wa upendo, mashuhuda wa huruma na wema wa Mungu kwa waja wake.

Chama cha Waamini Walei wa Mtakatifu Petro ni wamisionari jasiri a upendo wa Kristo na mashuhuda wa huruma na wema wa Mungu; chombo cha faraja kwa maskini na watu waliokata tamaa.

Papa Francisko: Rutubisheni huduma ya upendo kwa sala na tafakari!

12/05/2018 16:58

Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza wanachama wa Chama cha Waamini Walei wa Mtakatifu Petro ambao kwa miaka mingi wamekuwa kweli ni wamisionari wa upendo, mashuhuda wa huruma na wema wa Mungu pamoja na chombo cha faraja kwa maskini na watu waliokata tamaa!

Vyombo vya mawasiliano ya jamii vina wajibu wa kujenga na kudumisha: utu, heshima, udugu na haki msingi za binadamu.

Vyombo vya mawasiliano ya jamii vinayo dhamana na wajibu wa kulinda, kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu sanjari na ujenzi wa udugu na utu wema.

Vyombo vya mawasiliano vilinde na kudumisha utu na heshima ya binadamu

12/05/2018 16:20

Baba Mtakatifu Francisko anasema, vyombo vya mawasiliano ya jamii vina dhamana na wajibu wa kulinda, kutetea na kudumisha utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Vijenge jamii inayomsikwa katika udugu na utu kadiri ya moyo wa Mwenyezi Mungu

Wanajeshi 32 wa vikosi vya ulinzi na usalama vya Vatican maarufu kama "Swiss Guards" wamekula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Wanajeshi 32 wa Vikosi vya Ulinzi na Usala vya Vatican maarufu kama "Swiss Guards" wamekula kiapo cha utii na uaminifu kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Wanajeshi 32 wa vikosi vya ulinzi na usalama vya Vatican wala kiapo!

07/05/2018 16:34

Kiapo cha utii na uaminifu kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ni changamoto katika mchakato mzima wa uwajibikaji na huduma inayotolewa katika moyo wa utii na unyenyekevu kwa wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, Kanisa na kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Huu ni mchakato wa utakatifu wa maisha!

Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing wanapania kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili kama sehemu ya ushuhuda wa furaha ya Injili!

Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing wanapania kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili kama sehemu ya ushuhuda wa furaha ya Injili inayomwilishwa katika matendo!

Maisha na utume wa Masista wa Tutzing, Ndanda, Mtwara, Tanzania!

05/05/2018 15:23

Shirika la Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing lilianzishwa mwaka 1884 huko nchini Ujerumani na Padre Andreas Amrhein ili kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kama sehemu ya mchakato wa uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji mtu mzima: kiroho na kimwili!

Viongozi mbali mbali wa Kanisa wanakipongeza Chama cha Uamsho wa Kikatoliki kwa ushuhuda wake katika maisha na utume wa Kanisa.

Viongozi mbali mbali wa Kanisa wanakipongeza Chama cha Uamsho wa Kikristo kwa ushuhuda wake katika maisha na utume wa Kanisa.

Salam na matashi mema ya viongozi wa Kanisa kwa huduma ya uamsho

03/05/2018 07:00

Viongozi mbali mbali wa ngazi ya juu kutoka Vatican na Baraza la Maaskofu Katoliki Italia wametuma salam na matashi mema kwa wajumbe wa Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki nchini Italia, kinapoadhimisha mkutano wake wa 41 kwa kujikita katika huduma kwa Mungu na jirani kama ushuhuda wa upendo.