Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Francisko: Ujumbe Siku ya Wakimbizi 2018

Kanisa litaendelea kuwapokea, kuwalinda, kuwaendeleza na kuwahusisha wakimbizi na wahamiaji katika sera na mikakati yake ya kichungaji!

Kanisa litaendelea kuwapokea, kuwalinda, kuwaendeleza na kuwahusisha wakimbizi na wahamiaji katika sera na mikakati ya shughuli zake za kichungaji.

Kardinali Parolin: Kanisa litaendelea kuwahudumia wakimbizi!

07/03/2018 15:00

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu ndilo ambalo limepewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza sera na mikakati ya shughuli za kichungaji kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji duniani kwa kukazia: umuhimu wa: kuwapokea, kuwalinda, kuwaendeleza na kuwahusisha!

Wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji ni changamoto pevu katika ulimwengu mamboleo kutokana na chuki na uhasama dhidi ya watu hawa!

Wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji ni changamoto pevu katika ulimwengu mamboleo kutokana na baadhi ya wanasiasa kueneza chuki na uhamasa dhidi yao kwa kisingizio cha usalama wa taifa, raia na mali zao!

Jengeni utamaduni wa upendo na mshikamano na maskini!

07/03/2018 15:00

Kardinali Pietro Parolin anasema, chuki dhidi ya wakimbizi na wahamiaji ni kati ya changamoto kubwa inayoendelea kujitokeza katika ulimwengu mamboleo! Wakimbizi na wahamiaji wanaangaliwa kwa "jicho la kengeza" kama watu wanaohatarisha usalama wa raia na mali zao na kikwazo cha maendeleo!

Kuna madhara makubwa kwa watoto wakimbizi na wahamiaji kuwekwa vizuizini!

Kuna madhara makubwa kwa watoto wakimbizi na wahamiaji kuwekwa vizuizini.

Watoto wakimbizi na wahamiaji kuwekwa vizuizini kuna madhara makubwa

05/03/2018 08:00

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu linasema, watoto wakimbizi na wahamiaji kuwekwa vizuizini kuna madhara makubwa sana katika malezi na ukuaji wao kwa sasa na kwa siku za usoni! Kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kutafuta mbinu mbadala ya kuwahudumia!

Tarehe 2 Februari ni siku ya watawa duniani, siku iliyo anzishwa na Mt. Yohane Paulo II miaka 22 iliyopita

Tarehe 2 Februari ni siku ya watawa duniani, siku iliyo anzishwa na Mt. Yohane Paulo II miaka 22 iliyopita

Ni watawa 31,000 nchini Poland wanao mtumikia Mungu na jirani!

02/02/2018 15:04

Hotuba ya Askofu Jacek Kiciński na mwenyekiti wa Tume kwa ajili ya Taasisi,mashirika na vyama vya kitume wa Baraza la Maaskofu wa Poland,anasema,watawa katika dunia ni gurudumu la kuhamasisha upendo wa Mungu kati ya watu na wajenzi wa utamaduni wa umoja

 

 

Wakimbizi, wahamiaji na watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa, Jumapili tarehe 14 Januari 2018 wamelipamba Kanisa kuu la Mt. Petro kwa uwepo na ushiriki

Wakimbizi,wahamiaji na watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa, tarehe 14 Januari, Siku ya wakimbizi na wahamiaji duniani kwa mwaka 2018 wamelipamba Kanisa kuu la Mt. Petro mjini Vatican kwa uwepo na ushiriki wao.

Wakimbizi na wahamiaji wapamba Kanisa kuu la Mt. Petro mjini Vatican

14/01/2018 14:37

Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2018 na kuhudhuria na umati mkubwa wa wakimbizi, wahamiaji, watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa na wadau mbali mbali wanaoshiriki katika huduma na maisha ya wakimbizi.

 

Papa Francisko: Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2019 ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko: Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji kwa mwaka 2019 ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko sasa Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Kuadhimishwa Sept.

14/01/2018 13:46

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kutokana na sababu za kichungaji kuanzia mwaka 2019, Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniania yatafanyika Jumapili ya Pili ya Mwezi Septemba kila mwaka. Kumbe, maadhimisho haya kwa mwaka 2019 yatakuwa ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko anawaalika waamini kujenga utamaduni wa kuwaalika watu, kufahamiana na kujitambulisha kati ya watu!

Papa Francisko anawaalika waamini kujenga utamaduni wa kualika, kufahamiana na kujitambulisha kati ya watu.

Papa: Jitahidini kualika, kufahamiana na kujitambulisha na watu!

14/01/2018 11:15

Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2018 imekuwa ni nafasi kwa Baba Mtakatifu Francisko kutoa mwaliko kwa waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, wanatoa mwaliko, wanafahamiana na kujitambulisha kati ya watu kama ushuhuda amini!

Baraza la Maaskofu Katoliki Ufaransa linasema, wanasukumwa na imani kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji!

Baraza la Maaskofu Katoliki Ufaransa linasema, linasukumwa na imani kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji kadiri ya uwezo wake.

Maaskofu: Imani inatuwajibisha kuwapokea wakimbizi na wahamiaji!

12/01/2018 15:49

Baraza la Maaskofu Katoliki Ufaransa linasema, hata kama Serikali haitaki kuwajibika kuwapokea na kuwakirimia wakimbizi, lakini, Wakristo wanasukumiwa na kuwajibishwa na imani yao kuhakikisha kwamba, wanawapokea na kuwakirimia wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta hifadhi, amani na usalama!