Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Francisko Perù 2018: Umoja wa Matumaini

Papa Francisko asema kipaumbele cha Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji eneo la Amazonia!

Papa Francisko asema, kipaumbele cha kwanza kwa Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji wa kina kwenye eneo la Amazonia.

Papa Francisko: Kipaumbele cha Kanisa Perù: Uinjilishaji wa Amazonia

31/01/2018 07:02

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Maaskofu kuwa karibu zaidi na wakleri wao; kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya Kiinjili ili kupambana na saratani ya rushwa, ufisadi na kumong'onyoka kwa haki msingi, utu na heshima ya binadamu. Maaskofu wathamini majadiliano katika ukweli na uwazi.

Papa Francisko anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kufanikisha hija yake ya kitume Amerika ya Kusini.

Papa Francisko anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kuhitimisha hija ya kitume nchini Amerika ya Kusini.

Papa Francisko ataja yale "yaliyomkuna" huko Amerika ya Kusini

24/01/2018 11:07

Baba Mtakatifu wakati wa katekesi yake, Jumatano tarehe 24 Januari 2018 licha ya kugusia umuhimu wa waamini kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuombea umoja wa Kanisa, amewashirikisha pia waamini na mahujaji kuhusu mambo msingi yaliyojiri wakati wa hija yake ya kitume Amerika ya Kusini!

Papa Francisko katika mahojiano yake na waandishi wa habari amezungumzia masuala mbali mbali ya maisha na utume wa Kanisa Amerika ya Kusini.

Baba Mtakatifu Francisko katika mahojiano maalum na waandishi wa habari akiwa anarejea mjini Vatican amezungumzia imani na ushuhuda wa upendo, changamoto na kufafanua kuhusu kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo nchini Chile.

Yaliyojiri katika mahojiano kati ya Papa Francisko na wanahabari

23/01/2018 13:32

Ushuhuda wa imani ya familia ya Mungu Amerika ya Kusini, ujasiri, moyo wa toba na wongofu wa ndani na ushuhuda wa nguvu ya Injili kwa wafungwa wanaotaka kuandika kurasa mpya, utunzaji wa mazingira na kashfa ya Karadima, vimepembuliwa na Papa Francisko karika mahojiano na wanahabari.

Papa Francisko asikitishwa sana na vurugu zinazoendelea huko nchini DRC na kuwataka wahusika kurejesha utawala wa sheria na demokrasia.

Papa Francisko asikitishwa na uvunjifu wa misingi ya haki, amani na maridhiano nchini Congo DRC na kuwataka viongozi wa Serikali kurejesha utawala wa sheria na demokrasia.

Papa Francisko asikitishwa na mateso ya wananchi wa DRC

22/01/2018 15:33

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jimbo kuu la Lima, nchini Perù ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na vurugu na uvunjaji wa haki msingi za binadamu unaoendelea nchini Jamhuri ya Watu wa Congo na kuwataka viongozi wa serikali kurudisha utawala wa sheria na haki,

Bikira Maria ni mlango wa mbingu, ni mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu.

Bikira Maria ni mlango wa mbingu, ni mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu.

Papa Francisko: Bikira Maria ni mlango, Mama wa huruma na matumaini

21/01/2018 15:18

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Bikira Maria ni mlango wa mbinguni, nyota ya asubuhi; ni Mama wa huruma na matumaini yanayowaongoza watu kwa Kristo Yesu ambaye kimsingi ni Lango la Huruma ya Mungu. Familia yote ya Mungu inapata utambulisho wake kwa Bikira Maria, Mama wa wote!

Huruma na upendo ni chachu ya mchakato wa ujenzi mpya wa matumaini yanayofariji, kuganga na kuponya!

Huruma na upendo ni chachu ya mchakato wa ujenzi mpya wa matumaini yanayofariki, yanayoganga na kuponya madonda ya mwanadamu!

Papa Francisko asema, mshikamano wa upendo ni ushuhuda wa matumaini

21/01/2018 14:50

Moyo wa mshikamano na upendo katika kupambana na matatizo na changamoto za maisha ni kielelezo cha hali ya juu kabisa cha ushuhuda wa Injili ya matumaini inayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu wa Mungu na kwa njia hii, wakristo wanaweza kutambulikana kuwa kweli ni wafuasi wa Yesu.

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na furaha ya utambuzi binafsi; mwaliko wa wito wao na kushirikisha furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na utambuzi binafsi wa wito wao; kutambua na kuthamini mwaliko wa maisha na utume wao pamoja na kuhakikisha kwamba, wanawashirikisha wengine ile furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Wakleri na watawa: zingatieni: utambuzi binafsi, mwaliko na furaha!

21/01/2018 14:05

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kukazia ile furaha ya utambuzi wa mtu binafsi kile anachotenda; pili watambue na kuthamini muda wa mwaliko wa kumfuasa Kristo kwani hii ni kumbu kumbu endelevu katika kumfuasa Kristo na kwamba, wajitahidi kushirikisha furaha ya Injili.

Papa Francisko anaitaka familia ya Mungu nchini Chile kujenga na kudumisha umoja wa matumaini unaofumbata maisha ya vijana na watakatifu wa Amerika.

Papa Francisko anaitaka familia ya Mungu nchini Perù kujenga na kudumisha umoja wa matumaini unaofumbata maisha ya vijana na kushuhudiwa na watakatifu wa Amerika ya Kusini.

Umoja wa matumaini udumishe haki, mshikamano na utunzaji wa mazingira

20/01/2018 12:20

Baba Mtakatifu Francisko anawataka viongozi nchini Perù kuhakikisha kwamba, wanakuza na kudumisha umoja wa matumaini ili kutunza mazingira; kupigania haki msingi za binadamu; kujenga mshikamano katika kukabiliana na majanga na kwamba, vijana ni cheche za matumaini nchini Perù.