Mitandao ya kijamii:

RSS:

App:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Francisko Misri, 28- 29 Aprili 2017

Wakleri, watawa na majandokasisi wanamshukuru Papa Franciko kwa kuendelea kuwatia moyo katika maisha na utume wao licha ya changamoto kubwa zilizopo!

Wakleri, watawa na majandokasisi wanamshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa uwepo na tunza yake ya kibaba kwa wakleri, watawa na majandokasisis licha ya changamoto zilizoko.

Wakleri, watawa na majandokasisi wamshukuru Papa Francisko!

30/04/2017 12:45

Wakleri, watawa na majandokasisi wakati wa sala na Baba Mtakatifu, wamemshukuru kwa uwepo wake miongoni mwao na kumwomba aendelee kuwasindikiza katika dhamana, maisha na utume wao katika malezi na majiundo ya familia ya Mungu nchini Misri kwa kutambua changamoto zilizopo.

 

Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji linasaidia miradi mingi katika bara la Afrika, lakini pia hata Baraza la Kipapa kwa Huduma ya Maendeleo

Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji linasaidia miradi mingi katika bara la Afrika, lakini pia hata Baraza la Kipapa kwa Huduma ya Maendeleo ya Binadamu kwenye mpango wa Impact Investiment linajihusisha kutafuta fedha za mmiundo mbinu ya kanisa

Afrika imefadhiliwa tangu zamani na wamisionari kutoka Ulaya!

29/04/2017 16:52

Kardinali Turkson amesema pamoja na Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji kusaidia miradi mingi katika bara la Afrika,lakini hata Baraza la Kipapa Huduma ya Maendeleo endelevu ya Binadamu katika mpango Impact Investiment linajihusisha, kuhakikisha upatikanaji wa fedha kwa miundo mbinu

 

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni mashuhuda na wajenzi wa amani duniani!

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni mashuhuda na wajenzi wa amani duniani.

Vijana ni jeuri ya Kanisa na Jamii katika ujumla wake!

29/04/2017 16:15

Baba Mtakatifu Francisko akiwa kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Misri, Ijumaa jioni alipata bahati ya kukutana na kusalimiana na mahujaji vijana wapatao 3000 waliokuwa mjini Cairo kwa ajili ya kushiriki katika hija ya maisha ya kiroho pamoja na Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa Uwanjani.

 

Kanisa la Kikoptik limeguswa na kutikiswa sana na vitendo vya kigaidi, linataka kuendelea kuwa ni chemchemi ya haki na amani.

Kanisa la Kikoptik nchini Misri limeguswa na kutikiswa sana, lakini linataka kuendelea kuwa ni chemchemi ya haki, amani upendo na mshikamano wa kweli!

Misri inataka kuwa ni chemchemi ya amani duniani!

29/04/2017 15:53

Papa Tawadros II anampongeza na kumshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwa kweli ni Baba wa maskini, mjumbe wa amani na majadiliano ya kidini na kiekumene ili kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano, upendo na mshikamano kati ya watu wa Mataifa, changamoto kwa wote!

Uekumene wa damu uwafungamanishe Wakristo kushuhudia imani yao, kutetea haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Uekumene wa damu uwafungamanishe wakristo kusimama kidete kushuhudia imani yao, kutetea haki msingi za binadanu na kudumisha amani duniani.

Uekumene wa damu udumishe umoja na mshikamano wa Wakristo duniani!

29/04/2017 15:33

Wakristo wanaunganishwa kwa namna ya pekee katika imani moja inayobubujika kutoka katika Sakramenti ya Ubatizo! Uekumene wa damu uwajenge na kuwaimarisha Wakristo katika kumshuhudia Kristo na Kanisa lake sanjari na kusimama kidete kulinda haki msingi za binadamu na amani duniani!

Familia ya Mungu nchini Misri inampongeza na kumshukuru Papa Francisko mjumbe wa amani na Baba wa maskini!

Familia ya Mungu nchini Misri inamshukuru na kumpongeza Papa Francisko mjumbe wa amani na Baba wa maskini duniani.

Familia ya Mungu Misri inampongeza Papa Francisko mjumbe wa amani

29/04/2017 14:55

Familia ya Mungu nchini Misri inampongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kujitahidi kufuata nyayo za Mtakatifu Francisko wa Assisi katika maisha yanayojikita katika ufukara, mchakato wa kutafuta, kulinda na kudumisha amani duniani sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa Takatifu mjini Cairo, Misri amewataka waamini kuwa kweli ni mashuhuda wa Kristo Mfufuka kwa matendo!

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa Takatifu mjini Cairo amewataka waamini kuwa kweli ni mashuhuda wa imani juu ya Kristo Mfufuka, imani inayomwilishwa katika matendo!

Papa Francisko: Ni nafasi ya kutafakari: Kifo, Ufufuko na Maisha!

29/04/2017 14:28

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri wakati wa hija yake ya kitume nchini Misri amekazia umuhimu wa waamini kutafakari Fumbo la Kifo, Ufufu na Maisha mapya yanapyaishwa kwa kukutana na Kristo Yesu katika kusikiliza Neno lake pamoja na maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu!

Papa Francisko anaitaka Misri kusimama kidete kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu huko Mashariki ya Kati!

Papa Francisko anaitaka Misri kusimama kidete kulinda na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu huko Mashariki ya Kati!

Papa Francisko: Misri ina dhamana ya ujenzi wa amani duniani!

28/04/2017 18:13

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Misri inao mchango mkubwa katika kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba, sheria zilizopo zinatekelezwa kikamilifu kwa kuzingatia utu na heshima ya binadamu bila ubaguzi wala misimamo mikali.