Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Papa Francisko Chile 2018: Amani Yangu Nawapa

Papa Francisko anawashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka usiku na mchana ili kufanikisha hija yake ya kitume nchini Chile.

Papa Francisko anawashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba, anafanikisha hija yake ya kitume nchini Chile kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 Januari 2018.

Papa Francisko anawashukuru wote waliojisadaka kwa ajili ya hija yake

18/01/2018 15:42

Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru viongozi wa Kanisa na Serikali pamoja na umati mkubwa wa watu wa Mungu waliojisadaka usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba, hija yake ya kitume inafanikiwa huko nchini Chile kwa kujenga utamaduni wa watu kukutana na kuadhimisha Mafumbo ya Kanisa.

Papa Francisko anawataka waamini kujenga utamaduni wa mshikamano na upendo kwa kusikiliza na kujibu kilio cha jirani zao.

Papa Francisko anawataka waamini kujenga na kudumisha utamaduni wa upendo kwa kusikiliza na kujibu kilio cha jirani zao

Papa: Tangazeni Injili ya furaha kwa kudumisha haki msingi za binadamu

18/01/2018 15:15

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hata leo hii kuna watu "hawana divai" kwa kukosa fursa za ajira ili kuhudumia familia zao; kuna ukosefu mkubwa wa haki msingi za binadamu na utumwa mamboleo unaonyanyasa utu na heshima ya binadamu; haki za wahamiaji ziko rehani; waamini wasimame kidete kuwatetea!

Papa Francisko asema, vijana ni chachu ya mageuzi ya kijamii, upyaisho wa Kanisa na kiini cha maisha na utume wa Kanisa.

Papa Francisko anasema vijana ni chachu ya mageuzi na upyaisho wa KanisA; Niini cha maisha na utume wa Kanisa.

Vijana ni chachu ya mageuzi na kiini cha maisha na utume wa Kanisa!

18/01/2018 08:15

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwahakikishia vijana kwamba, wao ni sehemu muhimu sana ya mageuzi ya kijamii na chachu inayolipyaisha Kanisa! wao ni kiini cha maisha na utume wa Kanisa, ndiyo maana ameitisha Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ili Kanisa liweze kujifunza kutoka kwa vijana!

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja, mshikamano, maridhiano na kusikilizana.

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja, mshikamano na maridhiano kwa kuheshimiana, kuthaminiana na kukamilisha katika maisha.

Papa Francisko: Jengeni utamaduni wa umoja, upatanisho na kusikilizana

17/01/2018 14:48

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja unaofumbatwa katika zawadi ya amani unaowawezesha watu kusikilizana, kushikamana, kutegemeana na kukamilishana ili kuimarisha upatanisho dhidi ya nguvu zinazotishia Injili ya matumaini!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro kwa kutubu, kuongoka na kutakaswa na Kristo Yesu katika maisha na utume wao!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro aliyeteleza na kuanguka katika udhaifu wake, akasamehewa dhambi zake na kutakaswa kwa huruma ya Kristo, na hivyo kusonga mbele katika ushuhuda wa huduma kwa watu wa Mungu!

Petro mtume aliyeanguka, akasamehewa na kutakaswa awe mfano wa Kanisa

17/01/2018 11:06

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kumwangalia Mtakatifu Petro, Mtume aliyeanguka kutokana na udhaifu wake wa kibinadamu kiasi hata cha kumkana Yesu; Petro, aliyesamehewa mapungufu yake na Petro mtume, aliyetakaswa kwa huruma ya Kristo Yesu, awe mfano wa kuigwa!

Papa Francisko asema hata gerezani wafungwa wanaweza kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini inayosimikwa katika toba na wongofu wa ndani!

Papa Francisko asema, hata gerezani wafungwa wanaweza kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini katika toba na wongofu wa ndani!

Papa Francisko asema, hata wafungwa bado wanayo ndoto ya matumaini!

17/01/2018 06:00

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwenye Gereza kuu la wanawake la "san Joaquin" nchini Chile amewapongeza wafungwa kwa ujasiri na unyenyekevu wao wa kutambua kwamba, wameteda dhambi na kutindikiwa neema ya Mungu katika maisha, mwanzo wa matumaini mapya katika Kristo!

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya haki, amani na upatanisho wa kitaifa!

Papa Francisko anawataka waanchi wa Chile kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki, amani na upatanisho wa kitaifa!

Papa: Heri wapatanishi na wenye kiu ya haki, wataitwa wana wa Mungu!

16/01/2018 15:49

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wananchi wa Chile kuwa ni vyombo na mashuhuda wa upatanisho ili kujenga amani na umoja wa kitaifa, chemchemi ya kweli katika maisha. Wale wote wanaotamani amani, wanapaswa kujizatiti kuitafuta na kuimwilisha katika haki inayozingatia utu na heshima ya binadamu!

Papa Francisko awataka viongozi wa Chile kusikiliza na kujibu kilio cha maskini na wanyonge ndani ya jamii!

Papa Francisko awataka viongozi kusikiliza na kujibu kilio cha maskini na wanyonge ndani ya jamii!

Papa Francisko awataka viongozi nchini Chile kusikiliza kilio cha watu

16/01/2018 15:07

Baba Mtakatifu Francisko katika hija yake ya kitume nchini Chile, amewataka viongozi wa Serikali na vyama vya kiraia kusikiliza sauti ya wanyonge na maskini katika jamii! Amesitishwa na kashfa pamoja na nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo nchini Chile!