Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre William Bahitwa

Kwa njia ya Fumbo la Msalaba, Kristo Yesu ameanzisha Ufalme wa Mungu hapa duniani.

Kwa njia ya Fumbo la Msalaba, Kristo Yesu ameanzisha Ufalme wa Mungu hapa duniani na wote wanaalikwa kushiriki kikamilifu.

Ufalme wa Mungu unapata utimilifu wake katika Fumbo la Pasaka!

16/06/2018 06:30

Kristo Yesu kwa kutimiza mapenzi ya Baba yake wa mbinguni, ameanzisha duniani ufalme wa mbinguni. Sasa mapenzi ya Baba, ni kuinua watu wamzunguke, Mwanawe, Kristo Yesu. Kusanyiko hilo ni Kanisahapa duniani, mbegu na mwanzo wa Ufalme wa Mungu. Wote wanaitwa kuingia katika ufalme wa Mungu.

Mwanadamu ana lazima ya kufuataq sheria maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii inaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mtu!

Mwanadamu ana lazima ya kufuata sheria ya maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii yaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mwanadamu!

Dhambi na matokeo ya ufunuo wa mpango wa ukombozi wa mwanadamu

09/06/2018 16:39

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mapendo, mambo yanayojionesha tangu pale Adamu na Eva walipoanguka dhambini na kujikuta wako watupu, kwa kupoteza: urafiki na Mwenyezi Mungu; Uhuru wa kweli; Wema na utakatifu wa maisha! Lakini Mungu anawaahidia ukombozi!

Ekaristi Takatifu ni muhtasari wa Fumbo la Imani na Wokovu wa mwanadamu!

Ekaristi Takatifu ni muhtasari wa Fumbo la Imani na Wokovu wa mwanadamu.

Ekaristi Takatifu ni muhtasari wa imani na Fumbo zima la Wokovu!

02/06/2018 09:35

Ekaristi Takatifu ni jumla na muhtasari wa imani nzima ya Kanisa na kwamba, Fumbo la Wokovu wa mwanadamu vimelala juu ya Ekaristi Takatifu. Hii ni ishara thabiti ya ushirika katika uzima wa Kimungu. Ni chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa, mwendelezo wa uwepo wa Kristo Yesu!

Fumbo la Utatu Mtakatifu ni msingi wa imani, maisha na utume wa Kanisa.

Fumbo la Utatu Mtakatifu ni msingi wa imani, maisha na utume wa Kanisa.

Sherehe ya Utatu Mtakatifu: Umoja, Ukuu, Uweza na Utakatifu wa Mungu

26/05/2018 08:29

Tunasadiki kwa nguvu na tunakiri wzzi kwamba kuna Mungu Mmoja tu, wa kweli, wa milele, Mkuu, asiyebadilika, asiyetambulika, Mwenye uwezo wote, asiyeelezeka, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu: Nafsi Tatu, lakini uwapo mmoja tu, uwamo mmoja tu au asili moja tu!

Roho Mtakatifu anaendelea kujifunua katika Maandiko Matakatifu, Sakramenti za Kanisa, na katika maisha na utume wa Kanisa.

Roho Mtakatifu anaendelea kujifunua kwa njia ya Maandiko Matakatifu, Sakramenti za Kanisa na kwa namna ya pekee kabisa Sakramenti ya Kipaimara na katika maisha na utume wa Kanisa.

Pentekoste ni nafasi ya kumtafakari Roho Mtakatifu!

18/05/2018 15:35

Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu ndiye anayelitakatifuza Kanisa na kwamba, anayo nafasi muhimu sana katika maisha na utume wa Kanisa. Ni tunda la upendo wa Baba na Mwana! Roho Mtakatifu ni moyo wa Kanisa na kifungo cha umoja na kikolezo cha ushuhuda wa imani!

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawaachia wakristo wajibu wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawachia Wakristo wajibu na dhamana ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.

Leo mnatumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

11/05/2018 16:11

Ee Mungu Mwenyezi, utufanye tuwe na furaha takatifu na shukrani; kwa maana kupaa kwake Kristo Yesu, Mwanaoni mfano wetu; na huko alikotangulia yeye kichwa chetu, ndiko tunakotumaini kufika sisi tulio mwili wake. Leo ubinadamu wetu umetukuzwa mbinguni!

Leo Mama Kanisa anapenda kuwarejesha tena watoto wake kwenye shule ya upendo mkamilifu!

Leo Mama Kanisa anapenda kuwarejesha watoto wake kwenye shule ya upendo mkamilifu unaopata chimbuko lake kwa Mungu Baba ambaye ni upendo wenyewe!

Leo Mama Kanisa anawarudisha watoto wake kwenye shule ya upendo!

05/05/2018 07:30

Katika historia, Mwenyezi Mungu amejifunua kwa watu wake kwa sababu ya upendo wake mkuu usiokuwa na kifani; akawachagua kati ya mataifa kwa sababu ya upendo huo huo, akawakoa kutokana na ukaidi wao kwa sababu ya upendo! Kwa hakika, Mungu ni upendo na upendo wake ni wa milele!

Kristo Yesu ni Mzabibu wa kweli na Baba yake ndiye Mkulima, wafuasi wake wanapaswa kuwa mashuhuda kwa njia ya umoja, upendo na mshikamano.

Kristo Yesu ni Mzabibu wa kweli na Baba yake ndiye Mkulima, kumbe, wafuasi wake wanapaswa kuwa ni mashuhuda wake katika umoja, upendo na mshikamano wa dhati!

Yesu ni Mzabibu wa kweli unaoshuhudiwa katika umoja na upendo!

28/04/2018 07:48

Kristo Yesu ni Mzabibu wa kweli kwa sababu ameungana na kushibana sana na Baba yake wa mbinguni ambaye ndiye Mkulima. Hivyo wafuasi wake wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa umoja, upendo na mshikamano wa dhati unaomwilishwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko!