Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre Richard A. Mjigwa

Hija ya kiekumene ya Papa Francisko nchini Uswiss ni kuimarisha majadiliano ya kiekumene pamoja na kukutana na Wakatoliki kutoka Uswiss.

Hija ya Kiekumene ya Papa Francisko nchini Uswiss ni kutaka kuimarisha majadiliano ya kiekumene pamoja na kukutana na waamini wa Kanisa Katoliki.

Hija ya Kiekumene ya Papa Francisko yawasha moto wa kiekumene Geneva!

21/06/2018 17:55

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kiini cha hija yake ya kiekumene nchini Uswiss inayoongozwa na kauli mbiu: "Kutembea, kusali na kushirikiana" ni kumwezesha kukutana na Wakatoliki ndani na nje ya Uswiss, lakini zaidi, kuimarisha mchakato wa majadiliano ya kiekumene kati ya Makanisa!

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja!

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja.

Papa Francisko: Wakristo wanapaswa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana

21/06/2018 17:38

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Kiekumene, amekazia kwa namna ya pekee kabisa umuhimu wa Wakristo kutembea, kusali na kushirikiana, ili kuwapeleka watu kwa Kristo Yesu; kwa kujenga na kudumisha umoja na udugu katika sala na huduma kwa maskini!

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho!

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni, WCC. Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho kama alama na kielelezo makini cha uinjilishaji.

WCC: Ulimwengu uliomeguka unahitaji alama na ushuhuda wa nguvu!

21/06/2018 17:20

Walimwengu waliogawanyika na kusambaratika juu ya uso wa dunia, wanahitaji alama na ushuhuda wenye mvuto na mashiko, changamoto na mwaliko kwa Wakristo kujipatanisha, kudumisha umoja, kulinda maisha na kutunza mazingira nyumba ya wote, daima haki msingi za binadamu zikipewa kipaumbele!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko asema, Wakristo wanahimizwa kuenenda katika Roho!

21/06/2018 16:56

Baba Mtakatifu Francisko katika Ibada ya sala ya toba, upatanisho na umoja wa Makanisa amewataka Wakristo kuenenda katika Roho kwa kutambua kwamba, binadamu hapa duniani ni hujaji na kwamba, kuenenda katika Roho ni kiini cha wito na maisha ya Kikristo; ni kujikita katika msamaha na huduma!

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi ateuliwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi ameteuliwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Askofu mkuu Ruwaichi ateuliwa kuwa Askofu mwandamizi mrithi, Dar!

21/06/2018 12:01

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Saalam, Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Ruwaichi alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza! Hii ndiyo Breaking News!

Papa Francisko anawaalika waamini na wadau mbali mbali kuwa na mtazamo uliopyaisha kuhusu wakimbizi na wahamiaji  ili kuejenda udugu na mshikamano.

Papa Francisko anawaalika waamini pamoja na watu mbali mbali kuwa na mtazamo uliopyaishwa ili kujenga na kudumisha umoja, upendo na mshikamano na wakimbizi pamoja na wahamiaji.

Mshikamano wa upendo na udugu kwa wakimbizi na wahamiaji!

20/06/2018 15:30

Baba Mtakatifu Francisko analipongeza Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis kwa kuendesha kampeni inayopania kuragibisha haki msingi za wakimbizi na wahamiaji katika ngazi ya kimataifa. Lengo ni kujenga na kudumisha mtazamo uliopyaishwa!

Tarehe 21 Juni 2018 Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Ugonjwa wa SLA! Baadhi ya wagonjwa wamekutana na Papa Francisko.

Tarehe 21 Juni 2018 Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Wagonjwa wa SLA duniani.

Siku ya Kimataifa ya Mfumo wa Ugonjwa wa Neva mwaka 2018

20/06/2018 15:14

Jumuiya ya Kimataifa kila mwaka ifikapo tarehe 21 Juni inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ugonjwa wa Mfumo wa Neva. Huu ni ugonjwa hatari sana na takwimu zinaonesha kwamba, duniani kuna wagonjwa zaidi milioni 450 wanaoteseka kutokana na ugonjwa huu, baadhi yao wamekutana na Papa Francisko.

Papa Francisko asema, Amri za Mungu ni njia kuelekea uhuru kamili wa watoto wa Mungu.

Papa Francisko asema, Amri za Mungu ni njia ya kuelekea uhuru kamili wa watoto wa Mungu.

Amri za Mungu ni safari inayoelekea kwenye uhuru kamili!

20/06/2018 14:57

Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutekeleza Amri za Mungu wakiwa na moyo wa waana wa Mungu na kuachana na mwelekeo wa kutekeleza Amri hizi kwa woga na wasi wasi, kwani Amri za Mungu ni njia kuelekea uhuru kamili wa watoto wa Mungu.