Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre Reginald Mrosso

Yesu ni kielelezo cha mchungaji mwema, anayeona, anayehurumia na kuamua kutenda bila ya kujibakiza.

Kristo Yesu ni kielelezo cha mchungaji mwema, anayeona, anayehurumia na kuamua kutenda bila ya kujibakiza hata kidogo!

Kristo Yesu ni kielelezo cha mchungaji mwema na mwaminifu

19/07/2018 15:36

Uaminifu, huruma, ulinzi na urafiki ni kielelezo makini cha mchungaji mwema anayejisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu Mungu. Leo, Liturujia ya Neno la Mungu inakemea udhalimu unaofanywa na viongozi wa Kanisa ambao wamegeuka kuwa kama mbwa mwitu!

 

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu inayofumbatwa katika toba, wongofu na utakatifu wa maisha.

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu inayosimikwa katika ushuhuda wa maisha, toba, wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha!

Mnatumwa kuwa mashuhuda wa furaha ya Injili ya Kristo kwa Mataifa!

14/07/2018 06:58

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, ushuhuda wa Kikristo unafumbatwa katika uhalisia wa maisha na majadiliano katika nyanja mbali mbali za maisha ya mwanadamu. Ni ushuhuda wa upendo unaojikita katika toba na wongofu wa ndani kama chachu ya kuyatakatifuza malimwengu!

 

Wakristo wanapaswa kushika imani, kuiungama, kuishuhudia, kuitangaza na kuwashirikisha wengine!

Wakristo wanapaswa kushika imani, kuitangaza, kuishuhudia na kuwashirikisha wengine, wakiwa tayari hata kubeba Misalaba ya maisha yao, tayari kumfuasa Kristo Yesu.

Yesu Kristo anakataliwa nyumbani kwao Nazareti! Maamuzi mbele!

06/07/2018 07:46

Mkristo hatakiwi kushika imani tu na kuiishi, bali anapaswa kuitangaza, kuishuhudia na kuieneza pamoja na kuwa tayari kumfuasa Kristo Yesu katika Njia ya Msalaba, kati ya madhulumu ambayo hayakosekani kamwe katika Kanisa! Huduma na ushuhuda ni muhimu sana kwa wokovu wa binadamu!

 

Kwa njia ya Fumbo la Pasaka, Kristo Yesu ameshinda dhambi, kifo na mauti!

Kwa njia ya Fumbo la Msalaba, Kristo Yesu ameshinda dhambi, kifo na mauti!

Kristo Yesu ameshinda dhambi, kifo na mauti!

30/06/2018 17:18

Kwa njia ya maisha, mahubiri na matendo yake yote, Yesu anatangaza na kushuhudia kwa njia ya miujiza, maajabu na ishara nyingi kwamba, ndani mwake kuna Ufalme wa Mungu na kwamba, yote haya yanashuhudia kuwa Yesu ndiye Masiha aliyetangazwa, ambaye ameshinda dhambi, kifo na mauti!

 

Yohane Mbatizaji: ni kiungo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya; Alitambua Ujio wa Kristo, Akamtambulisha kuwa ni Mwanakondoo wa Mungu!

Yohane Mbatizaji: Ni kiungo muhimu kati ya Manabii wa Agano la Kale na Agano Jipya, Alitambua ujio wa Kristo Yesu, Akambatiza na kumtambulisha hadharani kuwa ni Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu.

Sherehe ya Kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji!

20/06/2018 16:27

Mtakatifu Yohane Mbatizaji, ni mtangulizi wa karibu wa Bwana, aliyetumwa kumtayarishia njia. "Nabii wa Aliye juu" ni Mkuu kuliko manabii wote na wa mwisho. Anazindua Injili, anashangilia ujio wa Kristo toka tumboni mwa mama yake, anamtambulisha kama Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za dunia.

 

Kristo Yesu ni nahodha shupavu wa Kanisa lake, licha ya mawimbi mazito, lakini daima liko mikononi mwa kiongozi makini!

Kristo Yesu ni nahodha shupavu wa Kanisa lake, hata pale linapokumbana na dhoruba kali, bado liko mikononi mwa kiongozi makini.

Wekezeni matumaini yenu kwa Mungu! Inalipa!

19/06/2018 15:52

Imani ni fadhila ya kimungu ambayo kwayo tunamsadiki Mungu na kila kitu alichokisema na anachotufunulia, na ambacho Kanisa takatifu latutaka tukisadiki, kwa sababu Yeye ndiye ukweli wenyewe! Licha ya dhoruba mbali mbali zinazolikumba Kanisa, lakini bado linasonga mbele! Kristo ni nahodha!

 

Ufalme wa Mungu hukua polepole na kuzaa matunda kwa wakati wake!

Ufalme wa Mungu hukua pole pole na kuzaa matunda kwa wakati wake, kila mwamini anaalikwa kushiriki katika ujenzi wake.

Ufalme wa Mungu: Unakua pole pole na kuzaa matunda kwa wakati wake!

15/06/2018 08:09

Mwenyezi Mungu anawaalika waja wake kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu unaosimikwa katika: kweli na uzima; utakatifu na neema; haki, upendo na amani. Ufalme hukua pole pole lakini uzaa matunda kwa wakati wake. Jambo la msingi ni kila mwamini kushiriki kikamilifu kuujenga!

 

Yesu anaonesha kuwa ana nguvu ya kuvunjilia mbali utawala wa Ibilis, shetani na kwamba, ndugu zake ni wale wote wanaosikia na kutekeleza Neno lake!

Yesu anaonesha kuwa ana nguvu ya kuweza kuvunjilia mbali utawala wa Ibilisi, shetani na kwamba, ndugu na jamaa zake ni wale wote wanaosikia na kumwilisha Neno lake katika uhalisia wa maisha yao!

Dhamiri ni mahali patakatifu panapopaswa kuheshimiwa!

07/06/2018 14:59

Dhamiri ni hukumu ya akili ambamo mwanadamu hutambua sifa adilifu ya tendo halisi analoelekea kulitenda, angali akilifanya au amekwisha kulitekeleza. Mwanadamu anapaswa kufuata kile ambacho ni haki na sahihi na kwamba, mwanadamu anaweza kutambua sheria ya Mungu kwa njia ya dhamiri nyofu!