Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre Joseph Peter Mosha

Kristo Yesu ni mfano bora wa kuigwa kama Mchungaji mwema!

Kristo Yesu ni mfano bora wa kuigwa kama Mchungaji mwema.

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili XVI ya Kipindi cha Mwaka B.

20/07/2018 15:44

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya XVI ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa inaonesha umuhimu wa viongozi kuona na kuguswa na mahitaji msingi ya watu wao pamoja na kutenda kwa ajili  ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi! Viongozi wawe ni vyombo vya huruma, upendo, umoja na mshikamano.

Ufukara wa Kiinjili uwawezeshe Wakristo kutangaza na kushuhudia Injili kwa watu wa Mataifa.

Ufukara wa kiinjili uwawezeshe wakristo kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo kwa watu wa Mataifa!

Ufukara wa Kiinjili uwawajibishe kutangaza na kushuhudia Injili!

13/07/2018 07:11

Yesu Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu ndicho kiini cha Habari Njema ya Wokovu inayopaswa kutangazwa na kushuhudiwa katika uhalisia wa maisha ya Wakristo! Kumbe, ufukara wa Kiinjili ni nyenzo msingi katika mchakato wa kumwilisha Injili ya upendo kwa maskini na wahitaji zaidi!

Kristo Yesu ni kielelezo cha hekima, nguvu na uweza wa Mungu wa kumwongoa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Kristo Yesu ni kielelezo cha hekima, nguvu na uweza wa Mungu wa kumwongoa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Tafakari ya Neno la Mungu: Hekima ya Mungu iwe dira na mwongozo wetu!

06/07/2018 07:07

Mungu Baba Mwenyezi amefunua uweza wake wote kwa namna ya ajabu sana kwa kujinyenyekesha kwa hiari na kwa Ufufuko wa Mwanawe, ambao kwa huo alishinda ubaya. Hivyo Kristo Msulubiwa ni nguvu na hekima ya Mungu. Kwa njia ya Fumbo la Pasaka, Mungu ameonesha nguvu na uweza wake!

Waamini wanahimizwa kujikita katika imani kwa Kristo na Kanisa lake, hasa nyakati za majaribu na majanga ya maisha!

Waamini wanahimizwa kujikita katika imani kwa Kristo na Kanisa lake hasa wakati wa majaribu na majanga ya maisha!

Utukufu wa Mungu na ukuu wa binadamu katika kazi ya uumbaji!

29/06/2018 11:12

Dunia imeumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kielelezo makini cha upendo wake usiokuwa na kifani. Mwenyezi Mungu yuko juu ya Uumbaji na yupo kwa ajili yake ili kuvihifadhi na kuvidumisha vitu vyote! Pamoja na uzuri wa kazi ya uumbaji, lakini pia kuna ubaya unaojitokeza, yaani uwepo wa dhambi!

Mtakatifu Yohane Mbatizaji ni Nabii wa Aliye Juu!

Mtakatifu Yohane Mbatizaji ni Nabii wa Aliye Juu

Sherehe ya Kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji: Nabii wa Aliye Juu!

22/06/2018 07:44

Mtakatifu Yohane Mbatizaji ni mtangulizi, aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kumwandalia njia Masiha na Mkombozi wa ulimwengu. Yohane Mbatizaji ni Nabii wa Aliye Juu; Ni rafiki wa Bwana Arusi aliyethubutu kumtambulishwa kwa watu kuwa ndiye "Mwanakondoo wa Munguanayeondoa dhambi za ulimwengu"

Ufame wa Mungu unasimikwa katika: kweli na uzima; utakatifu na neema; haki, upendo na amani.

Ufalme wa Mungu unasimikwa katika: kweli na uzima; Utakatifu na neema; Haki, amani na upendo.

Jitahidini kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu

12/06/2018 13:30

Tafakari ya Neno la Mungi, Jumapili ya XI ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu unaosimikwa katika ukweli na uzima; Utakatifu na neema; Haki, amani na upendo!

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo linalomrejeshea mwanadamu wito wake wa asili, yaani ile sura na mfano wa Mungu.

Maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalomrejeshea tena mwanadamu ule wito wake wa asili, yaani sura na mfano wa Mungu

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo kuu!

06/06/2018 15:09

Mama Kanisa anafundisha kwamba, maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalojumlisha yote. Yote Yesu aliyofanya, kutenda na kuteseka yalikuwa na lengo la kumrudisha mtu aliyeanguka katika wito wake wa awali; yaani kwa kuwa ni sura na mfano wa Mungu pamoja na kuwarejeshea tena ushirika na Mungu!

Ekaristi Takatifu ni: Sakramenti ya Sadaka: Shukrani, Kumbu kumbu na Uwepo!

Ekaristi Takatifu ni: Sakramenti ya Sadaka: Shukrani, Kumbu kumbu na uwepo!

FUMBO LA EKARISTI TAKATIFU: Yesu: Kuhani, Altare na Sadaka!

01/06/2018 08:36

Mama Kanisa anawakumbusha watoto wake kwamba, Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya Sadaka ya shukrani na masifu kwa Baba wa milele; Ni kumbu kumbu ya Sadaka ya Kristo ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa. Ni uwepo wa Kristo kwa nguvu ya Neno lake na Roho Mtakatifu! Hili ni Fumbo la Imani!