Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre Celestine Nyanda

Dr. Abdallah Saleh Possi amewataka watanzania kudumisha: amani, umoja, ukweli na uadilifu katika maisha yao!

Dr. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania mjini Vatican amewataka watanzania kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, umoja, ukweli na uadilifu katika maisha yao.

Balozi Possi: Watanzania dumisheni: amani, umoja, ukweli na uadilifu

18/05/2018 14:32

Balozi Abdallah Saleh Possi aliyewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko na kupata nafasi ya kuzungumza na viongozi waandamizi wa Vatican, jioni alikutana na kuzungumza na watanzania wanaoishi Roma na kukazia: amani, umoja, uadilifu, ukweli na uzalendo!

Dr. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania mjini Vatican amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko.

Dr. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania mjini Vatican amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 17 Mei 2018.

Dr. Abdallah Saleh Possi awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican

17/05/2018 17:00

Dr. Abdallah Saleh Possi kutoka Tanzania, Balozi Retselisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho pamoja na Balozi Ali Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia, wote kutoka Barani Afrika ni kati ya Mabalozi wapya waliowasilisha hati zao za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, 17.5.2018.

Maandalizi ya Sinodi ya Vijana yanaendelea kushika kasi hata Barani Afrika.

Maandalizi ya Sinodi ya vijana yanaendelea kushika kasi hata Barani Afrika. Ni wakati kwa viongozi wa Kanisa kujenga utamaduni na sanaa ya kuwasikiliza vijana wa kizazi kipya!

Maandalizi ya Sinodi ya Vijana yanazidi kupamba moto Barani Afrika

30/04/2018 08:15

Maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana itakayoadhimishwa mwezi Oktoba 2018 mjini Vatican yanaendelea kupamba moto sehemu mbli mbali za Bara la Afrika kama sehemu ya ujenzi wa utamaduni na sanaa ya kuwasikiliza na kuwatahamini vijana katika utume wa Kanisa!

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiri katika Jangwa la Maisha yao ya Kiroho, sasa ni wakati wa kudumisha ile neema ya utakaso waliojichotea!

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiriki katika Jangwa la Maisha yao ya kiroho, sasa ni wakati wa kuendelea kuhifadhi ile neema ya utakaso waliojichotea wakati wa Kwaresima!

Dumisheni neema ya Kipindi cha Kwaresima ili kukuza utakatifu!

28/03/2018 09:38

Kwa muda wa siku 40 Wakristo wamefanya safari ya kiroho katika jangwa la maisha yao kwa kufunga na kusali; kwa toba na wongofu wa ndani; kwa kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili! Huu ni muda muafaka wa kuendeleza neema ya utakaso!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira duniani wanaendelea kupukutika kama majani makavu kutokana na ukoloni mamboleo!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira wanaendelea kupukutika kutokana na vita ya ukoloni mamboleo inayoendeshwa kichini chini!

Mashuhuda wa utunzaji bora wa mazingira duniani wanavyopukutika!

07/03/2018 07:29

Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wake wa kitume "Laudato si" anaitaka familia ya Mungu duniani kusimama kidete kulinda, kutetea, kutunza na kuendeleza mazingira nyumba ya wote ili kukuza na misingi ya haki, amani, usawa, utu na heshima ya binadamu wote pasi na ubaguzi!

Dini hazina budi kusaidia mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu kwa kuzingatia kanuni maadili, utu na heshima ya binadamu!

Dini mbali mbali hazina budi kuchangia katika mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu kwa kuzingatia kanuni maadili, utu, heshima na haki msingi za binadamu!

Dini zisaidie mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu!

26/02/2018 14:08

Kardinali Peter Erdo anasema, dini zina mchango mkubwa sana katika mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu, kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano katika jamii. Maendeleo ya sayansi na teknolojia hayana budi kuzingatia kanuni maadili, utu na heshima ya binadamu!

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso na kifo cha Kristo! Msalabani, ili kuonesha toba na wongofu wa ndani!

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso, kifo na ufufuko ili kuonesha toba na wongofu wa ndani, tayari kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha: haki, amani na maridhiano kati ya watu.

Wakristo fungeni na kusali katika roho na kweli!

24/02/2018 09:25

Kwaresima ni kipindi cha kusali, kufunga, kutafakari na kutenda matendo ya huruma kwa maskini na wahitaji zaidi. Hiki ni kipindi muafaka kwa ajili ya maandalizi ya adhimisho la Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka kwa wafu. Hata leo hii kuna bado watu wanateseka!

Ushirikiano kati ya Jimbo kuu la Seoul, Korea ya Kusini na Jimbo kuu la Ouagadougou, Burkina Faso ni mfano bora wa kuigwa katika huduma ya maendeleo!

Ushirikiano kati ya Jimbo kuu la Seoul, Korea ya Kusini pamoja na Jimbo kuu la Ouagadougou, Burkina Faso ni mfano bora wa kuigwa katika mchakato wa huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu yanayogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Ushirikiano na mshikamano katika huduma ya maendeleo endelevu!

20/02/2018 06:59

Jimbo kuu la Seoul, Korea ya Kusini na Ouagadougou, Burkina Faso yamekuwa ni mfano bora wa kuigwa katika kushirikiana na kushikamana katika huduma ya ya maendeleo endelevu, ili kuwawezesha waamini kutoka katika Nchi za Kimisionari kutambua mchango wao katika ustawi wa Kanisa la Kristo!