Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Padre Agapiti Amani, ALCP/OSS

Papa Francisko anasema uchafuzi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni dalili za kupooza kwa upendo!

Papa Francisko anasema, uchafuzi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni dalili za kupoa kwa upendo duniani.

Papa Francisko: Uharibifu wa mazingira ni alama ya kupoa kwa upendo

08/02/2018 07:37

Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake wa Kwaresima kwa Mwaka 2018 anasema, hata mazingira yanashuhudia kupoa kwa upendo kwa kazi ya uumbaji kunakosababishwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira, utupaji wa taka ngumu baharini pamoja na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi.

Watanzania wanahimizwa juu ya utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote!

Watanzania wanahimizwa juu ya utanzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.

Utunzaji wa mazingira ni wajibu wa binadamu!

15/05/2017 14:11

Nchini Tanzania katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na ukame mkubwa ambao umetishia maisha ya watu kutokana na baa la njaa! Baadaye, kumekuwepo na mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko makubwa na hivyo kuharibu makazi ya watu na miundo mbinu! Hatari kubwa!

Tazameni mtu! Ecce homo!

Tazameni mtu! Ecce homo!

Tazameni mtu! Ecce homo!

14/04/2017 17:19

Maadhimisho ya Juma kuu yanawaingiza Wakristo katika kuadhimisha Mafumbo makuu ya imani inayofumbatwa katika Fumbo la Pasaka yaani: Mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu. Waamini wanahamasishwa kumwangalia Yesu Msalabani, tayari kumkimbilia kwa toba na wongofu wa ndani!

Uchafuzi wa mazingira umesababisha madhara makubwa kwa binadamu kiasi hata cha kukosa furaha! Haya ni matokeo ya dhambi ya asili!

Uchafuzi wa mazingira umesababisha madhara makubwa kwa mwanadamu kiasi hata cha kukosa furaha ya kweli katika maisha! Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linasema haya ni madhara ya dhambi ya asili.

Dhambi ya asili na matokeo yake kwa wanadamu na maumbile!

29/03/2017 16:56

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake wa Kipindi cha Kwaresima linachambua kwa kina na mapana dhana ya dhambi ya asili kama kosa la kutomtii Mwenyezi Mungu ambalo limepelekea madhara makubwa kwa mwanadamu na katika kazi ya uumbaji. Dhambi inampunguzia mtu furaha ya kweli.

Yesu aliwaimarisha mitume wake katika imani ili hatimaye, wawe ni vyombo na mashuhuda wa Fumbo la Msalaba!

Yesu aliwaimarisha mitume wake katika imani ili hatimaye, waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Fumbo la Msalaba, kielelezo cha hali ya juu cha huruma na upendo wa Mungu katika maisha ya mwanadamu!

Kwaresima ni kipindi cha kuimarisha: imani, matumaini na mapendo

23/03/2017 15:14

Yesu katika maisha na utume wake alipenda kuwaimarisha Mitume wake katika imani, matumaini na mapendo kwa Mungu na jirani ili kuweza kuikabilia kwa imani thabiti Fumbo la Msalaba, yaani mateso, kifo na ufufuko wake, ili hatimaye, waweze kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Fumbo la Pasaka!

Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wake wa kitume anakazia umuhimu wa mshikamano na upendo kama tunu msingi za maisha ya kijamii!

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa kitume Huruma na amani anakazia umuhimu wa upendo na mshikamano kama tunu msingi za maisha ya kijamii.

Huruma ya Mungu kama tunu msingi ya maisha ya kijamii!

09/03/2017 15:55

Matendo ya huruma yanayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu sehemu mbali mbali za dunia ni kielelezo cha uwepo endelevu wa kazi ya ukombozi iliyoanzishwa na Kristo Yesu, kazi inayofanywa na Mama Kanisa kwa wakati huu, kumbe, waamini wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa huruma!

 

Ndoa ni zawadi kubwa ambayo Mwenyezi Mungu amewakirimia wanadamu na kwa neema ya Kristo Yesu wanaweza kuishi kwa amani, upendo na uvumilivu mkuu!

Ndoa ni zawadi ambayo Mwenyezi Mungu amemkirimia mwanadamu na kwa njia ya neema ya Kristo wanandoa wanaweza kuishi kwa amani, upendo na uvumilivu huku wakisaidiana katika mchakato wa kujitakatifuza!

Familia ni mahali muafaka pa kumwilisha: huruma, upendo na msamaha!

08/03/2017 10:41

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa kitume: Huruma na amani anasema, ndoa ni zawadi kubwa ambayo Mwenyezi Mungu amewakirimia wanadamu na wito ambao kwa njia ya neema inayobubujika kutoka kwa Kristo na Kanisa lake wanandoa wanaweza kuwa na upendo, uaminifu na uvumilivu.

Kwaresima ni kipindi cha huduma ya upendo kwa jirani!

Kwaresima ni kipindi cha huduma ya upendo kwa jirani kama kielelezo cha imani tendaji!

Kwaresima: Kipindi cha kutunza mazingira na huduma kwa jirani!

07/03/2017 08:34

Kwaresima ni muda muafaka wa kulinda, kutunza na kudumisha mazingira bora nyumba ya wote! Ni wakati kusoma, kulitafakari na kulimwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili; ni wakati wa kutafakari sehemu ya Injili ya Maskini Lazaro na tajiri asiyeguswa na shida za watu!