Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Njia ya Msalaba Kuzunguka Magofu ya Colosseo

Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba anaadhimisha Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu.

Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba anaadhimisha Siku kuu ya kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, kielelezo cha huruma, upendo, msamaha na hekima ya Mungu kwa binadamu!

Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba wa Yesu: Utakatifu, huruma na upendo

14/09/2017 07:00

Kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba, Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya kutukuka kwa Msalaba wa Kristo, kielelezo cha mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kwa wafu; ufunuo wa utakatifu, ukuu, huruma, upendo na msamaha unaobubujika kutoka katika hekima ya Baba wa milele kwa ajili ya binadamu!

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo amegusia: kashfa ya mateso, imani na matumaini kwa huruma ya Kristo!

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo amegusia kashfa ya mateso ya watu sehemu mbali mbali za dunia; imani na matumaini kwa huruma na upendo wa Yesu kwa waja wake!.

Papa Francisko: Njia ya Msalaba katika uhalisia wa maisha ya watu!

15/04/2017 08:32

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo mjini Vatican, Ijumaa kuu tarehe 14 Aprili 2017 ametafakari kuhusu kashfa ya mateso na mahangaiko ya binadamu ulimwenguni pamoja na imani na matumaini kwa huruma na upendo wa Kristo Yesu!

Jengeni utamaduni wa amani kwa kukataa kishawishi cha ubaguzi na kulipizana kisasi!

Jengeni utamaduni wa amani kwa kukataa kishawishi cha kutaka kulipizana kisasi!

Rithisheni vijana wa kizazi kipya utamaduni wa haki na amani duniani

10/04/2017 11:17

Baba Mtakatifu Francisko anaitaka familia ya Mungu nchini Marekani na hasa zaidi Jimbo kuu la Chicago kuhakikisha kwamba, inajikita katika kujenga na kudumisha utamaduni wa amani kwa kuondokana na vishawishi vya kutaka kulipizana kisasi, hali ambayo inaendeleza chuki na uhasama kati ya watu.

Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa Mwaka 2017 ni mwaliko wa kuguswa na mahangaiko ya watu mbali mbali ili kudumisha utu na heshima yao!

Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa Mwaka 2017 ni mwaliko wa kusimama kidete kusikiliza kilio cha mahangaiko ya watu mbali mbali tayari kusimama kidete kulinda na kudumisha utu na heshima yao kama binadamu!

Tafakari ya Njia ya Msalaba Ijumaa kuu 2017: Wanawake wa Injili

10/04/2017 08:35

Tafakari ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo yaliyoko mjini Roma, Ijumaa kuu kwa mwaka 2017: ni kielelezo cha huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu, ni chemchemi ya haki, amani, upendo na msamaha wa kweli unaopaswa kufumbatwa katika maisha ya waamini wote!

Prof. Anne-Marie Pelletier kuandika tafakari ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colloseo kwa Ijumaa kuu kwa mwaka 2017

Prof. Anne-marie Pelletier kuandika tafakari ya Njia ya Msalaba Ijumaa kuu kwa mwaka 2017.

Prof. Anne-Marie Pelletier kutunga tafakari ya Njia ya Msalaba, 2017

01/04/2017 11:09

Papa Francisko amemteua Professa Anne Marie Pelletier, mtaalam wa Sayansi ya Maandiko Matakatifu, Mtafiti na mwandishi mashuhuri wa vitabu na majarida, mwanamke wa kwanza kuwahi kupokea Tuzo la Joseph Ratzinger, Papa Benedikto XVI kuandika Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa mwaka 2017.