Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Neno la Mungu

Mama Kanisa anapenda kuwahimiza watoto wake kujenga utamaduni wa kusikiliza, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika maisha yao!

Mama Kanisa anapenda kuwahimiza watoto wake kusoma, kulitafakari na kulimwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao ya kila siku!

Askofu Salutaris Libena: waamini kuzeni moyo wa Ibada na uchaji!

10/01/2018 14:44

Askofu Salutaris Libena anawataka waamini kujenga na kudumisha utamaduni wa Ibada na Uchaji wa Mungu kwa njia ya: Sala, Tafakari ya Neno la Mungu, Sakramenti za Kanisa bila kusahau Sala za Kanisa kama njia ya kuyatakatifuza malimwengu pamoja na Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu!

Askofu mkuu Anthony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kudumisha upendo, umoja na amani!

Askofu mkuu Athony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujenga na kudumisha umoja, upendo, mshikamano na amani kama njia muafaka ya kuadhimisha Noeli ya Bwana!

Ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kutoka kwa Askofu mkuu Muheria, Kenya

23/12/2017 08:49

Katika Sherehe ya Noeli, Mama Kanisa anaadhimisha kwa shangwe kubwa Fumbo la Umwilisho, Neno wa Mungu, Nafsi ya Pili ya Fumbo la Utatu Mtkatifu alipofanyika mwili kwa njia ya Roho Mtakatifu kwake Bikira Maria. Huu ni muungano wa ajabu wa asili ya Kimungu na asili ya kibinadamu ndani ya Kristo Yesu

Mara baada ya Katekesi Papa amewasalimia kikundi cha Wasanii kutoka Cuba

Mara baada ya Katekesi Papa amewasalimia kikundi cha Wasanii kutoka Cuba

Papa:Katika Katekesi,Baba Mtakatifu amechambua sehemu za Liturujia

20/12/2017 15:47

Leo hii ninataka kuingia mbashala katika maadhimisho ya Ekaristi.Mada hii ni mwendelezo wa Katekesi juu ya Misa:Misa imegawanyika katika sehemu kuu mbili:ya kwanza ni liturujia ya Neno na ya pili Liturujia ya Ekaristi,Papa anathibitisha kuwa sehemu hizi zinakwenda sambamba hazigawanyiki

 

Papa Francisko anawahimiza waamini kujenga utamaduni wa kusoma, kulitafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao!

Papa Francisko anawahimiza waamini kujenga utamaduni wa kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao.

Unafiki ni sumu inayowafanya watu kushindwa kusikiliza Neno la Mungu

17/10/2017 15:54

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujenga utamaduni wa kusoma, kulitafakari na hatimaye kulimwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha; ili kuonja huruma na upendo wa Mungu unaojifunua kwa njia ya Maandiko Matakatifu.

Waamini wanapaswa kukita maisha yao kwenye Injili ya Kristo Yesu, ili waweze kukua na kukomaa katika imani, matumaini na mapendo.

Waamini wanapaswa kukita maisha yao katika Injili ya Kristo Yesu, ili waweze kukua na kukomaa katika imani, matumaini na mapendo.

Kanisa limejengwa katika msingi wa imani ya Mitume wa Yesu!

20/09/2017 07:09

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anawahamasisha kukita maisha yao katika Habari Njema ya Wokovu, ili waweze kukua na kukomaa katika msingi ya imani, matumaini na mapendo kwa Mungu na jirani. Waamini kwa njia ya ushuhuda wao wajitahidi kuzima kiu ya haki na amani kati ya watu!

 

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kushikamana na Kristo Yesu katika maisha yao, kamwe wasijitafute wenyewe na kusahau uwepo wa Kristo!

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kujishakamanisha na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao na kamwe wasijitafute wenyewe watazama ndani ya tumbo la maji kama risasi.

Usiposhikamana na Kristo Yesu, utazama kama jiwe majini!

09/08/2017 13:23

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya XIX ya Mwaka A wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini kujishikamanisha na Kristo Yesu, aliye njia, ukweli na uzima! Pale wanaposhindwa kumwambata Kristo, watazama majini na kutoweka kama ndoto ya mchana! Kwa kushikamana na Yesu, amani inapatikana!

Papa Francisko anawataka waamini kung'oa vilema vya maisha kwa toba na wongofu wa ndani; kwa Sakramenti ya Upatanisho, Sala na Matendo ya huruma!

Papa Francisko anawataka waamini kung'oa vilema katika maisha yao kwa toba na wongofu wa ndani; kwa kukimbilia huruma na upendo kwa njia ya Sakramenti ya Upatanisho; kwa sala na matendo ya huruma.

Papa Francisko: Ng'oeni vilema, ili Neno lipate kuzaa matunda!

17/07/2017 09:08

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kung'oa vilema katika maisha yao ya kiroho, ili kweli Neno la Mungu lililopandwa ndani ya mioyo yao liweze kuzaa matunda ya toba, wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha kwa kuambata Sakramenti ya Upatanisho.

Kanisa linawahimiza waamini kusoma, kulitafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika maisha yao ya kila siku!

Kanisa linawahimiza waamini kusoma, kutafakari na kulimwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao ya kila siku!

Msilichakachue Neno la Mungu likashindwa kuzaa matunda yanayokusudiwa

12/07/2017 15:05

Maandiko Matakatifu yanategemeza maisha na utume wa Kanisa pamoja na kuyatia nguvu. Kwa wanakanisa ni uimara wa imani, lishe na chemchemi ya maisha ya kiroho. Ni kiini cha maisha ya kiroho, kitaalimungu na mahubiri ya kichungaji. Neno la Mungu ni taa na mwanga wa njia ya waamini!