Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mwenyeheri Paulo VI

Kardinali Angelo Amato ameng'atuka kutoka madarakani.

Kardinali Angelo Amato ameng'atuka kutoka madarakani kutokana na umri.

Kwa heshima ya Kardinali Angelo Amato!

19/07/2018 07:43

Watakatifu ni mifano bora ya kuigwa katika maisha na utume wa Kanisa. Hawa ni wadhambi waliotubu na kumwongokea Mungu katika safari ya maisha yao. Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kanisa linaundwa na watakatifu na wadhambi wanaojitahidi kutubu na kumwongokea Mungu ili wawe watakatifu!

Askofu mkuu Protase Rugambwa: AMECEA msikubali kutumbukia katika ukabila na udini usiokuwa na mvuto wa mashiko kwa maendeleo ya watu wa Mungu.

Askofu mkuu Protase Rugambwa: Amewataka Mababa wa AMECEA kutokubali kutumbukizwa katika sera za ukabila na udini usiokuwa na mvuto wala mashiko kwa ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu Barani Afrika.

AMECEA: Msikubali ukabila na udini viwapekenyue na kusababisha maafa

17/07/2018 14:00

Askofu mkuu Protase Rugambwa, amewataka Mababa wa AMECEA kujenga na kudumisha umoja, udugu na mshikamano kama dira na mwongozo wa watu wa Mungu Barani Afrika. Usawa na utofauti kati ya watu ni sehemu ya mpango wa Mungu, ili kutajirishana na kushirikishana: karama, fadhila na wema!

Mwenyeheri Nunzio Sulprizio, kijana mleo na mfanya kazi ni mfano bora wa kuigwa kwa vijana wa kizazi kipya katika maisha na utakatifu.

Mwenyeheri Nunzio Sulprizio ì, kijana na mwamini mlei ni mfano bora wa kuigwa na vijana wa kizazi kipya kwa maisha na utakatifu wake.

Mwenyeheri Nunzio Sulprizio: kijana mlei na mchapakazi, mfano bora!

17/07/2018 08:20

Baba Mtakatifu Francisko anataka kuwawekea vijana wa kizazi kipya mbele yao mfano wa Mwenyeheri Nunzio Sulprizio, kijana mlei na mchapakazi, aliyepata ulemavu na majanga katika maisha, lakini akasimama imara katika imani, matumaini na mapendo, leo hii ni mfano bora wa kuigwa na vijana wenzake!

Siku ya Sala ya Kiekumene imekuwa na mafanikio makubwa katika maisha na utume wa Kanisa.

Siku ya Sala ya Kiekumene imekuwa na mafanikio makubwa katika maisha na utume wa Kanisa kwa sasa na kwa siku za usoni.

Siku ya Sala ya Kiekumene Bari: Mageuzi makubwa katika uekumene!

09/07/2018 16:07

Professa Andrea Riccardi Muasisi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio anasema, Siku ya Sala ya Kiekumene kwa ajili ya kutafakari, kusali na kuombea amani huko Mashariki ya Kati imekuwa na mafanikio makubwa katika mchakato wa uekumene wa sala na huduma miongoni mwa Wakristo!

Papa Francisko katika Nia zake  za Jumla kwa Mwezi Julai 2018 anasema anaguswa sana na upweke na mahangaiko ya Mapadre wake!

Papa Francisko katika Nia zake za Jumla kwa Mwezi Julai, 2018 anasema kwamba, anaguswa sana upweke pamoja na mahangaiko ya mapadre wake!

Papa Francisko aguswa na upweke na mahangaiko ya Mapadre wake!

05/07/2018 09:14

Mapadre ni wahudumu wa Neno na Sakramenti za Kanisa. Ni wagawaji wa Mafumbo ya Kanisa na wahudumu wa Jumuiya waliyokabidhiwa, lakini zaidi ni wandani wa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii! Lakini, wakati mwingine wanakabiliwa na "majanga ya maisha! Wanahitaji sala!

Waraka wa Mwenyeheri Paulo VI kwa Mapadre Duniani ulioandikwa kunako mwaka 1967.

Waraka wa Mwenyeheri Paulo VI kwa Mapadre Duniani, tarehe 30 Juni 1967.

Waraka wa Mwenyeheri Paulo VI kwa Mapadre Duniani

03/07/2018 08:44

Mwenyeheri Paulo VI kwa kusoma alama za nyakati kutokana na changamoto zilizojitokeza katika maisha na utume wa Mapadre baada ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, aliamua kuwaandikia Mapadre Waraka maalum akionesha tasaufi ya Daraja Takatifu, dhamana na changamoto zake ulimwenguni!

Watakatifu Petro na Paulo ni miamba wa imani ya Kanisa la Kristo!

Watakatifu Petro na Paulo ni miamba wa imani ya Kanisa la Kristo!

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo, Miamba wa imani ya Kanisa

30/06/2018 07:47

 Mtakatifu Petro alimkiri Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu aliye hai, zawadi ya ufunuo wa Fumbo la Utatu Mtakatifu! Kwa njia hii, Kristo Yesu anamkabidhi Mtakatifu Petro dhamana na wajibu wa kulitunza na kuliendeleza Kanisa lake, Sakramenti ya wokovu wa binadamu na alama ya umoja na Baba wa milele!

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican, 2018.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican kwa mwaka 2018.

Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda: maisha, utume na changamoto zake

19/06/2018 07:14

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 18 Juni 2018 alikutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda ambalo kwa sasa liko mjini Vatican kama sehemu ya utekelezaji wa hija ya kitume inayofanyika walau mara moja kila baada ya miaka mitano! Ni nafasi ya kusali na kutafakari.