Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mwana Kondoo wa Mungu

Injili ya siku ya Mtakatifu Yohane inaeleza mazungumzo ya mwisho kati ya Bwana Yesu na Mtakatifu Petro. Katika mahubiri ametafsiri mtindo wa kufuata

Injili ya siku ya Mtakatifu Yohane inaeleza mazungumzo ya mwisho kati ya Bwana Yesu na Mtakatifu Petro. Katika mahubiri ametafsiri mtindo wa dhati, ambao mitume wanapaswa kuwa nao katika kumfuasa Yesu.

Kupenda,kuchunga na kujiandaa kubeba msalaba ndiyo dira ya mfuasi wa Yesu!

18/05/2018 16:09

Kupenda,kuchunga na kujiandaa katika msalaba, zaidi ili kutoangukia katika vishawishi vya kuweka pua katika maisha ya wengine. Ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu aliowapatia wakati wa mahubiri yake tarehe 18 Mei 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatacan akifafanua Injili ya Siku ya Mt.Yohane

 

 

Yesu akiinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake, kielelezo cha utii na utimilifu na mwanzo wa Agano Jipya na la milele!

Kristo Yesu akiinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha utii kwa Baba yake wa mbinguni, mwanzo wa Agano Jipya na la milele.

Kristo Yesu akishakuinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake!

13/03/2018 14:46

Saa ya Kristo Yesu kadiri ya mafundisho ya Mwinjili  Yohane ni Fumbo la Pasaka, yaani: Mateso, Kifo na Ufufuko wa Kristo unaomkirimia mwanadamu ukombozi. Hiki ni kielelezo cha hali ya juu kabisa cha Utii kwa Baba yake wa milele na utimilifu wa Agano Jipya na la Milele linalofumbata Sadaka yake!

 

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na furaha ya utambuzi binafsi; mwaliko wa wito wao na kushirikisha furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na utambuzi binafsi wa wito wao; kutambua na kuthamini mwaliko wa maisha na utume wao pamoja na kuhakikisha kwamba, wanawashirikisha wengine ile furaha ya kukutana na Kristo Yesu.

Wakleri na watawa: zingatieni: utambuzi binafsi, mwaliko na furaha!

21/01/2018 14:05

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kukazia ile furaha ya utambuzi wa mtu binafsi kile anachotenda; pili watambue na kuthamini muda wa mwaliko wa kumfuasa Kristo kwani hii ni kumbu kumbu endelevu katika kumfuasa Kristo na kwamba, wajitahidi kushirikisha furaha ya Injili.

Papa Francisko: Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2019 ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko: Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji kwa mwaka 2019 ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko sasa Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Kuadhimishwa Sept.

14/01/2018 13:46

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kutokana na sababu za kichungaji kuanzia mwaka 2019, Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniania yatafanyika Jumapili ya Pili ya Mwezi Septemba kila mwaka. Kumbe, maadhimisho haya kwa mwaka 2019 yatakuwa ni tarehe 8 Septemba 2019.

Papa Francisko anawaalika waamini kujenga utamaduni wa kuwaalika watu, kufahamiana na kujitambulisha kati ya watu!

Papa Francisko anawaalika waamini kujenga utamaduni wa kualika, kufahamiana na kujitambulisha kati ya watu.

Papa: Jitahidini kualika, kufahamiana na kujitambulisha na watu!

14/01/2018 11:15

Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2018 imekuwa ni nafasi kwa Baba Mtakatifu Francisko kutoa mwaliko kwa waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, wanatoa mwaliko, wanafahamiana na kujitambulisha kati ya watu kama ushuhuda amini!

Wakristo wanaitwa na wanatumwa, kumtangaza na kumshuhudia Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu kiini cha imani na wito wao!

Wakristo wanaitwa, wanatumwa kumtangaza na kumshuhudia Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu kiini cha imani na wito wao katika maisha ya Kikristo!

Wakristo: Mnaitwa na kutumwa kumtangaza na kumshuhudia Mwana Kondoo

13/01/2018 10:24

Liturujia la Neno la Mungu, Jumapili ya II ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa inajielekeza zaidi katika mchakato wa wito na ushuhuda! Wakristo kwanza kabisa wanaitwa kuchuchumilia utakatifu unaoshuhudiwa katika mchakato mzima wa maisha ya mwamini: kiroho na kimwili! Ushuhuda wenye mvuto na mashiko!

Familia ya Mungu inamhitaji kiongozi mwenye mvuto na mashiko atakayeshuhudia huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake!

Familia ya Mungu inamhitaji kiongozi mwenye mvuto na mashiko atakayewafunulia waja wake upendo na huruma ya Mungu

Familia ya Mungu inahitaji viongozi wenye mvuto na mashiko!

12/01/2018 10:08

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya II ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa inaonesha hitaji msingi la familia ya Mungu kuwa na kiongozi mwenye mvuto na mashiko, atakayejisadaka kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia: huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake kama ilivyo kwa Kristo Yesu!

 

Wito wa kwanza ni utakatifu wa maisha unaomwilishwa katika ushuhuda wa maisha!

Wito wa kwanza ni utakatifu wa maisha unaomwilishwa katika ushuhuda wa maisha yenye mvuto na mashiko!

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili II: Mnaitwa na kutumwa kushuhudia

12/01/2018 08:50

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili II ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini kusikiliza vyema sauti ya Mungu katika maisha yao na hivyo kuwa tayari kuijibu kwa ari na moyo wa ukarimu, tayari kushuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha, kielelezo cha imani tendaji!