Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mwaka wa huruma ya Mungu

Wamisionari wa huruma ya Mungu ni vyombo vya faraja, huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake!

Wamisionari wa huruma ya Mungu ni vyombo vya faraja, huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake.

Papa Francisko: Wamisionari wa huruma ni vyombo vya upendo na faraja

10/04/2018 14:44

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Wamisionari wa huruma ya Mungu ni vyombo na mashuhuda wa huruma, upendo na faraja ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Kwa njia yao waamini wengi wamepata nafasi ya msamaha na maondoleo ya dhambi zao, sasa wanaweza kusonga mbele kwa imani zaidi!

Mama Kanisa anataka kuendeleza tasaufi ya huruma ya Mungu katika maisha na utume wake!

Mama Kanisa anataka kuendeleza tasaufi ya huruma ya Mungu katika maisha na utume wake.

Mchakato wa kuendelea kupyaisha huruma ya Mungu katika maisha!

07/04/2018 10:56

Askofu mkuu Salvatore Rino Fisichella anasema, katika maadhimisho ya Mwaka wa Huruma ya Mungu Baba Mtakatifu aliwateua baadhi ya mapadre na kuwatuma sehemu mbali mbali za dunia kama wamisionari wa huruma ya Mungu, ili kuwaondolea watu dhambi na vikwazo vyao, tayari kuanza upya!

Papa Francisko anataka Mababa wa Sinodi kusikiliza shuhuda za waathirika wa biashara, matumizi na usambazaji wa dawa haramu za kulevya!

Papa Francisko anataka Mababa wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Vijana kusikiliza shuhuda za vijana wanaojihusisha na biashara, matumizi na kusambaza dawa za kulevya, ili Kanisa liweze kuibua mbinu mkakati na sera kwa ajili ya mapambano dhidi utamaduni wa kifo!

Mapambano dhidi ya biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya!

17/03/2018 09:43

Baba Mtakatifu Francisko kwa kutambua mateso na mahangaiko ya vijana wanaofanya biashara, wanaotumia na kusambaza dawa haramu za kulevya, ameamuwa kuwaalika vijana wawili kutoka Italia ili kushuhudia madhara ya matumizi haramu ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana wa kizazi kipya.

Waamini jifunezni tena Injili ya Huruma ya Mungu, ufuno wa Uso na haki ya Mungu kwa binadamu!

Waamini jifunzeni tena Injili ya Huruma ya Mungu ambayo ni Ufunuo wa Uso na haki ya Mungu kwa binadamu!

Jifunzeni kumwilisha Injili ya Huruma ya Mungu katika maisha!

22/02/2018 10:43

Injili ya huruma ya Mungu ni chanda na pete na Furaha ya Injili inayokita mizizi yake katika toba na wongofu wa ndani; upendo na mshikamano wa dhati kama ulivyoshuhudiwa na Baba mwenye huruma. Injili ya huruma ni ufunuo wa Uso na Haki ya Mungu; ni divai ya upendo na uhuru kamili katika ukweli!

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukazia sera na mikakati ya kutangaza na kushuhudia Injili ya familia duniani.

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukuza na kudumisha sera na mikakati ya Injili ya familia duniani inayofumbatwa katika Injili ya uhai na huruma ya Mungu!

Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018, Jimbo kuu la Dublin, Ireland

09/02/2018 07:10

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, baada ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma ya Mungu, Siku ya IX ya Familia Duniani huko Jimbo kuu la Dublin, Ireland itakuwa ni fursa makini ya kumwilisha Injili ya huruma ya Mungu katika maisha na utume wa familia duniani.

Waraka wa Maaskofu Katoliki Chile: Majadiliano, uwajibikaji na huruma kwa ajili ya Chile inayosimikwa katika haki.

Waraka wa Maaskofu Katoliki Chile: Majadiliano, uwajibikaji na huruma kwa ajili ya Chile inayosimikwa katika haki!

Majadiliano, uwajibikaji na huruma kwa ajili ya haki nchini Chile!

15/01/2018 08:12

Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu ilikuwa ni fursa kwa Baraza la Maaskofu nchini Chile kufanya upembuzi yakinifu kuhusu changamoto, fursa na matatizo yaliyokuwa yanawakumba wananchi wa Perù ili yaweze kuvaliwa njuga kadiri ya fursa na nafasi zilizopo! Lakini....!

Ijumaa ya huruma ya Mungu ni siku maalum ya kumwilisha matyendo ya huruma: kiroho na kimwili!

Ijumaa ya huruma ya Mungu ni siku maalum ya kumwilisha matendo ya huruma: kiroho na kimwili.

Papa Francisko: utekelezaji wa Ijumaa ya huruma ya Mungu

23/09/2017 16:22

Ijumaa ya huruma ya Mungu ni siku ambayo ilianzishwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu, ili kumsaidia katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro kumwilisha matendo ya huruma: kiroho na kimwili katika maisha!

Waamini wanahamasishwa kukimbilia katika Mahakama ya huruma ya Mungu  ili kupata maondoleo ya dhambi, huruma, faraja na mapendo!

Waamini wanahamasishwa kukimbilia kwenye Mahakama ya huruma ya Mungu: inayotakasa, huruma inayofariji, huruma inayosamehe na kupyaisha upya!

Msamaha na upatanisho katika kweli na haki ni chemchemi ya furaha!

16/09/2017 09:23

Huruma na msamaha ni utambulisho wa watoto wa Mungu na ushuhuda wa upendo. Msamaha una nguvu inayoleta uponyaji wa ndani katika maisha ya mwamini. Msamaha humweka mtu huru na kuanza mchakato wa ujenzi wa misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano katika ukweli na matumaini!