Mitandao ya kijamii:

RSS:

App:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mtakatifu Yohane Paulo II

Askofu mkuu Alesandro D'Errico ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Malta.

Askofu mkuu Alesandro D'Errico ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Malta.

Askofu mkuu D'Errico ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Malta

27/04/2017 17:27

Askofu mkuu Alesandro D'Errico aliyezaliwa kunako mwaka 1950 na kupewa Daraja Takatifu ya Upadre mwaka 1974 na hatimaye, kuteuliwa kuwa Askofu mwaka 1998 na kuwekwa wakfu mwaka 1999 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malta!

 

Jumapili ya huruma ya Mungu ni mwaliko kwa waamini kukumbatia na kuambata huruma ya Mungu katika maisha yao.

Jumapili ya huruma ya Mungu ni mwaliko kwa waamini kukumbatia na kuambata huruma ya Mungu katika maisha yao, ili waweze kuitolea ushuhuda katika maisha.

Papa Francisko: Endeleeni kukumbatia na kuambata huruma ya Mungu!

24/04/2017 10:59

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba, Jumapili ya Pili ya Kipindi cha Pasaka inajulikana kama "Jumapili Nyeupe" siku ambayo waamini waliobatizwa katika mkesha wa Pasaka walikuwa wanavua nguo zao nyeupe na kuvijika utu mpya; ni Jumapili ya huruma ya Mungu iliyoanzishwa na Mt. Yohane Paulo II.

Kardinali Attilio Nicora, Jembe la kazi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

kardinali Attilio Nicora, Jembe la kazi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kujisadaka kwa maisha na utume wake katika nyadhifa mbali mbali ndani ya Kanisa.

Kardinali Attilio Nicora, "Jembe mahiri la kazi" amefariki dunia!

24/04/2017 08:26

Mama Kanisa anaomboleza kifo cha Kardinali Attlio Nicora kilichotokea tarehe 22 Aprili 2017 mjini Roma. Alizaliwa kunako mwaka 1937. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre mwaka 1964. Akateuliwa na kuwekwa wakfu kama Askofu mwaka 1977 kama Askofu msaidizi, Mwaka 1992 akapelekwa Verona.

Ibada kwa huruma na Mungu na kwa Bikira Maria ni nyenzo muhimu katika kutafuta na kuambata utakatifu wa maisha!

Ibada ya huruma ya Mungu na kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa ni nyenzo muhimu sana katika kuchuchumilia na kuambata utakatifu wa maisha!

Ibada kwa Bikira Maria na Huruma ya Mungu ni nyenzo msingi kiroho

24/04/2017 06:30

Ibada kwa Bikira Maria na huruma ya Mungu ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya kiroho: ili kuchuchumilia na kuambata utakatifu wa maisha! Hii ni changamoto ambayo imetolewa kwenye Kituo cha Hija Kiabakari Jimbo Katoliki Musoma wakati wa mkesha wa maadhimisho ya Jumapili ya huruma!

Mitume na mashuhuda wa huruma ya Mungu ni wale walioguswa kwa Fumbo la Msalaba, wakawa tayari kuishuhidia huruma ya Mungu kwa jirani zao!

Mitume na mashuhuda wa huruma ya Mungu ni watu walioguswa na Fumbo la Msalaba, wakawa tayari kuandika Injili ya huruma ya Mungu katika uhalisia wa maisha yao ya kila siku!

Jifunzeni huruma ya Mungu kutoka kwa Kristo na mashuhuda wake!

22/04/2017 10:11

Maadhimisho ya Jumapili ya huruma ya Mungu imekuwa ni nafasi muafaka sana kwa mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania kutembelea Kituo cha hija cha Kiabakari Jimbo Katoliki Musoma kwa ajili ya kushiriki novena, hija, mkesha na hatimaye, maadhimisho ya Jumapili ya huruma ya Mungu!

 

Yesu Kristo ni ufunuo wa Uso wa huruma ya Mungu inayoadhimishwa katika Sakramenti na kushuhudiwa katika matendo ya huruma kiroho na kimwili!

Yesu Kristo ni ufunuo wa Uso wa huruma ya Mungu inayoadhimishwa katika Sakramenti na kushuhudiwa katika maisha kwa njia ya matendo ya huruma: kiroho na kimwili!

Jumapili ya kutangaza Injili ya: Huruma, Imani, Amani na Matumaini!

22/04/2017 09:33

Maadhimisho ya Jumapili ya Pili ya Kipindi cha Pasaka, maarufu kama Jumapili ya huruma ya Mungu ni nafasi nyingine kwa waamini kutangaza na kushuhudia Injili ya huruma ya Mungu inayofumbatwa katika Sakramenti na matendo ya huruma; kwa kujikita katika imani, amani na matumaini!

Jumapili 23 Aprili 2017 Kanisa katoliki linasheherekea  Sikukuu ya Huruma ya Mungu,iliyo anzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II

Jumapili 23 Aprili 2017 Kanisa katoliki linasheherekea Sikukuu ya Huruma ya Mungu,iliyo anzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II

Huruma ya Mungu kuunganisha Mt. Yohane Paulo II na Papa Francisko

21/04/2017 13:24

Monsinyo Oder amesema,huwezi kufikiria huruma ya Mungu bila uwepo wa ufufuko wa Bwana,kwasababu ufufuko wa Bwana yaani Pasaka ya Bwana ndiyo utambulisho wa huruma ya Mungu,ndiyo ufunguo wa maisha,na maisha ya milele.Ni zawadi ya Mungu anayo itoa kwa binadamu kwa njia ya Kristo.

 

Huruma ya Mungu imefunuliwa kwa njia ya: Fumbo la Umwilisho, Mahubiri, Miujiza, Mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka kwa wafu!

Huruma ya Mungu imefunuliwa kwa binadamu kwa njia ya: maisha, mafundisho, miujiza, mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka kwa wafu!

Ninyi ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya huruma ya Mungu!

21/04/2017 07:00

Iweni na huruma kama Baba yenu wa mbinguni ndiyo kauli mbiu iliyoongoza maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu! Ibada ya huruma ya Mungu ilianzishwa na Mtakatifu Faustina Kowalska na kutangazwa rasmi na Papa Yohane Paulo II; Papa Francisko ameivalia njuga zaidi!