Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mtakatifu Petro

Tarehe 13 Februari Misa ya  asubuhi ya Papa ameiadhimisha na Patriaki wa Antiokia, Youssef Absi na Sinodi yake yote

Tarehe 13 Februari Misa ya asubuhi ya Papa ameiadhimisha na Patriaki wa Antiokia, Youssef Absi na Sinodi yake yote

Misa ya Papa Francisko Katika kanisa la Mt Marta na Patriaki wa Antiokia!

13/02/2018 16:19

Asubuhi ya tarehe 13 Februari 2018,kama kawaida ya Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican,lakini hakuhubiri,bali ametoa maelezo kuhusu uwepo wa Patriaki wa Kanisa la Antiokia wa Kigiriki-Melkiti Youssef Absi na Ujumbe wake wote katika misa

 

 

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro kwa kutubu, kuongoka na kutakaswa na Kristo Yesu katika maisha na utume wao!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro aliyeteleza na kuanguka katika udhaifu wake, akasamehewa dhambi zake na kutakaswa kwa huruma ya Kristo, na hivyo kusonga mbele katika ushuhuda wa huduma kwa watu wa Mungu!

Petro mtume aliyeanguka, akasamehewa na kutakaswa awe mfano wa Kanisa

17/01/2018 11:06

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kumwangalia Mtakatifu Petro, Mtume aliyeanguka kutokana na udhaifu wake wa kibinadamu kiasi hata cha kumkana Yesu; Petro, aliyesamehewa mapungufu yake na Petro mtume, aliyetakaswa kwa huruma ya Kristo Yesu, awe mfano wa kuigwa!

Baba Mtakatifu katika katekesi yake amesema tufikirie mwana mpotevu, Mtakatifu Petro, mfarisayo na mtoza ushuru, mwanamke msamaria na Daudi

Baba Mtakatifu katika katekesi yake amesema tufikirie mwana mpotevu, Mtakatifu Petro, mfarisayo na mtoza ushuru, mwanamke msamaria na Daudi

Papa Francisko: Dhambi inamtenganisha mwamini na Mungu na jirani

03/01/2018 15:35

Papa amesema,tuendelee na katekesi yetu kuhusu maadhimisho ya ekaristi kwa kufikiria leo hii katika mantiki za liturujia ya utangulizi kwa tendo la kuungama.Hii inasaidia kujiweka tayari ili kustahili kuadhimisha mafumbo matakatifu na kutambua dhambi zetu mbele ya Mungu na ndugu zetu

 

Yesu anawaalika wafuasi wake kujikana wenyewe, kuubeba vyema Msalaba na kuanza kumfuasa!

Yesu anawaalika wafuasi wake kujikana wenyewe, kuubeba vyema Msalaba na kuanza kumfuasa!

Jitoeni sadaka kusimamia, kutangaza na kushuhudia ukweli!

30/08/2017 18:22

Mama Kanisa anawaalika watoto wake kutambua ukweli, ili waweze kuusimamia kikamilifu, kuutangaza na kuushuhudia kati ya watu wa Mataifa! Ukweli wenyewe ni Yesu Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu, mwaliko kwa kila mwamini kujikana mwenyewe na kuubeba vyema Msalaba wake!

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye hai! Jibu makini kutoka kwa Mkristo, mwamba wa imani kwa Kristo Yesu na Kanisa lake.

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye Hai, Jibu makini kutoka kwa Mkristo, mwamba thabiti wa imani kwa Kristo na Kanisa lake!

Kristo Yesu anataka kujenga Kanisa lake juu ya mwamba wa imani yako!

23/08/2017 12:18

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya XXI ni mwaliko kwa kila Mkristo kujibu swali la msingi, Je, Kristo ni nani katika maisha yake! Je, anayo imani thabiti ambayo Kristo Yesu anaweza kuitumia kujenga msingi wa Kanisa lake, msingi unaofumbatwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko?

 

Kristo Yesu alitambua fika karama, uwepo, udhaifu na mapungufu ya Mtakatifu Petro, lakini akampatia uongozi wa kondoo wake.

Kristo Yesu alitambua fika karama, uwepo, udhaifu na mapugunfu ya Mtakatifu Petro, lakini bado aliweza kumdhaminisha kazi ya kuliongoza na kulichunga kundi lake.

Watu wa Mungu wanapaswa kuongozwa kwa upendo na moyo wa unyenyekevu

02/06/2017 15:41

Yesu Kristo alimfahamu vyema Mtakatifu Petro; akatambua karama na mapaji yake, udhaifu na mapungufu yake ya kibinadamu, kiasi hata cha kumdhaminisha kuongoza na kulichunga kundi la Kristo kwa upendo mkuu, ari na moyo wa unyenyekevu, kwa kutambua kwamba, ameonja pendo la Kristo!

Papa Francisko anawaalika waamini kumsikiliza, kumfuasa na kumtii Kristo Mchungaji mwema!

Papa Francisko anawaalika waamini kumsikiliza, kumfuasa na kumtii Kristo Yesu, Mchungaji mwema katika maisha yao.

Papa Francisko: Imani inapaswa kukua, kukomaa, kuenea na kushuhudiwa!

08/05/2017 14:53

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini kuwa macho na makini zaidi ili wasitumbukie katika dhambi kwa kupingana na Roho Mtakatifu anayeendelea kutenda kazi ndani ya Kanisa, bali wawe makini kumsikiliza Roho Mtakatifu ili kung'amua yale anayotaka yatendeke kwa ajili ya Ufalme wa Mungu!

Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa Mwaka 2017 ni mwaliko wa kuguswa na mahangaiko ya watu mbali mbali ili kudumisha utu na heshima yao!

Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa Mwaka 2017 ni mwaliko wa kusimama kidete kusikiliza kilio cha mahangaiko ya watu mbali mbali tayari kusimama kidete kulinda na kudumisha utu na heshima yao kama binadamu!

Tafakari ya Njia ya Msalaba Ijumaa kuu 2017: Wanawake wa Injili

10/04/2017 08:35

Tafakari ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo yaliyoko mjini Roma, Ijumaa kuu kwa mwaka 2017: ni kielelezo cha huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu, ni chemchemi ya haki, amani, upendo na msamaha wa kweli unaopaswa kufumbatwa katika maisha ya waamini wote!