Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Msemaji Mkuu wa Vatican

Papa Francisko amedhamiria kukutana na kuzungumza na wahanga wa nyanyaso za kijinsia.

Papa Francisko amedhamiria kukutana na kuzungumza na wahanga wa nyanyaso za kijinsia.

Papa kukutana na wahanga wa nyanyaso za kijinsia kutoka Chile

26/04/2018 16:12

Baba Mtakatifu Francisko amedhamiria kukutana na kuzungumza na wawakilishi wa wahanga wa nyanyaso za kijinsia kutoka Chile kwa faragha katika hali ya udugu na kwamba, Baba Mtakatifu anapenda kutumia fursa hii kuwaomba msamaha kutokana na kashfa hii ambayo imechafua maisha na utume wa Kanisa.

Baraza la Makardinali Washauri chini ya Papa Francisko limehitimisha mkutano wake wa XXIV.

Baraza la Makardinali Washauri chini ya Papa Francisko limehitimisha mkutano wake wa XXIV.

Baraza la Makardinali Washauri lahitimisha mkutano wake wa XXIV

26/04/2018 15:56

Baraza la Makardinali Washauri chini ya Baba Mtakatifu Francisko limehitimisha mkutano wake wa XXIV uliojikita katika kupitia muswada wa Katiba mpya ya kitume itakayokuwa ni dira na mwongozo wa maisha na utume wa Sakretarieti kuu ya Vatican kama chombo cha huduma kwa Papa na Makanisa mahalia.

Tarehe 5 Aprili 2018 Chama cha kitume cha Ukatekumeni Mpya kinaadhimisha Jubilei ya miaka 50, Jimbo kuu la Roma.

Tarehe 5 Aprili 2018 Chama Cha Kitume cha Ukatekumeni Mpya kinaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 ya maisha na utume wake Jimbo kuu la Roma.

Papa Francisko kuzindua Mwezi wa Rozari Takatifu, "Divino Amore"

11/04/2018 14:52

Ratiba elekezi ya maadhimisho mbali mbali yatakayohudhuriwa na Baba Mtakatifu Francisko yanaonesha kwamba, Mei Mosi, 2018 atazindua Mwezi wa Rozari Takatifu kwa kusali kwenye Madhabahu ya "Divino Amore", Roma pamoja na kushiriki Jubilei ya miaka 50 ya Jumuiya ya Ukatekumeni mpya.

Papa Francisko kutembelea Nchi za Baltic kuanzia tarehe 22-25 Septemba 2018.

Papa Francisko kutembelea Nchi za Baltic kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 25 Septemba 2018.

Papa Francisko mwezi Septemba 2018 kutembelea nchi za Baltic!

12/03/2018 12:33

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Maaskofu Katoliki kutoka Lithuania, Latvia na Estonia kwa kushirikiana na viongozi wao la kutaka atembelee katika nchi zao. Hija hii itakuwa hapo tarehe 22 hadi 25 Septemba 2018. Familia ya Mungu katika eneo hili inampongeza Papa!

Papa Francisko akutana na waathirika wa nyanyaso za kijinsia Chile!

17/01/2018 15:09

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa viongozi wa serikali, wanadiplomasia na viongozi wa vyama vya kiraia amekemea vikali na kulaani nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo zilizofanywa na viongozi wa Kanisa nchini Chile. Amekutana na waathirika wa nyanyaso hizi na kuwafariji!

 

Papa Francisko anatembelea Myanmar na Bangaladesha kuanzia tarehe 27 Nov. hadi tarehe 2 Desemba 2017.

Papa Francisko anatembelea Myanmar na Bangaladesh kuanzia tarehe 27 Novemba hadi tarehe 2 Desemba 2017.

Papa Francisko kutembelea Myanmar na Bangaladesh 27 Nov -2 Des. 2017

28/08/2017 14:03

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini Myanmar na Bangaladesh kuanzia tarehe 27 Novemba hadi tarehe 2 Desemba 2017. Anatembelea nchini Myanmar kama mjumbe wa upendo na amani; nchini Bangaladesha kama mjumbe wa utulivu na amani duniani!

Dr. Joaquin Navarro-Valls, gwiji na nguli wa tasnia ya habari, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Dr. Joaquin Navarro-Valss, gwiji na nguli wa habari amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Dr. Navarro-Valls, gwiji na nguli wa tasnia ya habari amefariki dunia

06/07/2017 13:52

Dr. Joaquin Navarro-Valls, mwamini mlei, daktari wa magonjwa ya afya ya akili aliyeacha taaluma yake hiyo akabobea katika tasnia ya habari, kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 2006 akavunja rekodi ya kuwa ni msemaji mkuu wa Vatican! Amewahudumia Yohane Paulo II na Papa Mstaafu Benedikto XVI.