Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mons. Antoine Camilleri

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Estonia

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Estonia.

Waziri Mkuu wa Estonia akutana na Papa Francisko mjini Vatican

10/02/2018 17:08

Vatican na Estonia inaridhishwa na kiwango cha mahusiano wa kidiplomasia kilichofikiwa kati ya nchi hizi mbili bila kusahau mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wengi wa Estonia. Haya ni kati ya mambo makuu yaliyozungumzwa kati ya Papa na Waziri mkuu wa Estonia

Vietnam na Vatican zinaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa ajili ya mafao ya wengi.

Vietnam na Vatican zinaendelea kuimarisha uhusiano wa kidplomasia kwa ajili ya magao ya pande hizi mbili.

Vietnam na Vatican kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia

27/01/2018 14:15

Vietnam na Vatican tangu zilipounda Kikosi kazi kunako mwaka 2009 kumekuwepo na maendeleo makubwa ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya pande hizi mbili. Kwa pamoja wanapania kuendelea ushirikiano huu kwa kupanua wigo zaidi katika masuala ya elimu, ustawi na mafao ya wengi.

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Perù mwaka 2018 inapania kuimarisha mafungamano ya kijamii.

Hija ya Papa Francisko nchini Perù kwa mwaka 2018 inapania kuimarisha mafungamano ya kijamii.

Hija ya Papa Francisko nchini Perù kuimarisha mafungamano ya kijamii

23/09/2017 17:13

Baba Mtakatifu Francisko, mwaka 2018 anatarajia kufanya hija ya kitume inayopania kuimarisha mahusiano na mafungamano ya kidiplomasia kati ya Vatican na familia ya Mungu nchini Perù. Hadi sasa kuna uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, lakini hija ya kitume itayakuza zaidi!

Tume ya kudumu kati ya Vatican na Israeli iliyoanzishwa kunako mwaka 1993 inasema, imeridhwa na hatua iliyofikiwa katika majadiliano kati yao!

Tume ya Kudumu kati ya Vatican na Israeli iliyoanzishwa kunako mwaka 1993 inasema imeridhishwa na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo baina yake na kwamba, kuna matumaini kwa siku za hivi karibuni kutiwa sahihi Mkataba kati ya mchi hizi mbili.

Tume ya kudumu ya Vatican na Israeli yaridhishwa na maendeleo yake

15/06/2017 16:14

Wajumbe wa Tume ya Kudumu ya Vatican na Israeli wameridhishwa na mafanikio makubwa yaliyokwisha kupatikana tangu majadiliano baina ya serikali hizi mbili yalipoanzishwa kunako mwaka 1993 na kwamba, kuna matumaini ya pande hizi mbili kutia sahihi mkataba wa ushirikiano mapema iwezekanavyo!

Papa Francisko anasema, silaha za nyuklia zinatishia: ulinzi, usalama, amani na maendeleo endelevu ya binadamu!

Papa Francisko anasema, silaha za nyuklia zinatishia: ulinzi, usalama, amani na maendeleo endelevu ya binadamu.

Papa Francisko: fanyeni maamuzi magumu dhidi ya silaha za nyuklia

28/03/2017 15:51

Baba Mtakatifu Francisko anasema katika kipindi cha karne ya 21 kumekuwepo na matukio ambayo yanaendelea kuhatarisha ulinzi, usalama na amani duniani hasa kutokana na vitendo vya kigaidi, vita, ukosefu wa usalama kwenye mitandao ya mawasiliano ya jamii, mabadiliko ya tabianchi na umaskini.

Wajumbe wa Tume ya kazi ya kudumu kati ya Vatican na Israeli watakutana tena mjini Vatican mwezi Machi 2017.

Wajumbe wa Tume ya kazi ya kudumu kati ya Vatican na Israeli watakutana tena mjini Vatican mwezi Machi 2017.

Wajumbe wa Vatican na Israeli kukutana tena Machi 2017

20/01/2017 16:08

Wajumbe wa Tume ya kazi ya kudumu kati ya Vatican na Israeli wamehitimisha mkutano wao wa mwanzo wa mwaka huko Yerusalemu kwa kuridhishwa na maendeleo ya mazungumzo yaliyofikiwa kati ya pande hizi mbili hadi wakati huu na kwamba, watakutana tena mwezi Machi 2017 mjini Vatican. 

 

Serikali ya Vietnam itaendelea kushirikiana kwa karibu na Vatican kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini humo!

Serikali ya Vietnam itaendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na Vatican kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini Vietnam.

Vatican na Vietnam kuendelea kushirikiana kwa karibu zaidi!

28/10/2016 09:15

Kikosi kazi kati ya Vatican na Serikali ya Vietnam kinasema, pande hizi mbili zitaendelea kushirikiana kwa karibu zaidi kama sehemu ya mchakato wa majadiliano ya ushirikiano wa kimataifa yaliyoanzishwa kunako mwaka 2014, kwa ajili ya ustawi, mafao na maendeleo endelevu ya Vietnam.

 

Moneyval inaipongeza Vatican katika kudhibiti utakatishaji wa fedha haramu.

Moneyval inaipongeza Vatican katika udhibiti wa mchakato wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili kwa vitendo vya kigaidi.

Moneyval yaipongeza Vatican kwa kudhibiti utakatishaji wa fedha chafu!

10/12/2015 09:34

Vatican inaendelea kujifunga kibwebwe ili kuhakikisha kwamba, inadhibiti mchakato wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili kwa vitendo vya kigaidi unaoweza kutumiwa na taasisi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, maadili, weledi; ukweli na uwazi katika masuala ya fedha.