Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mkesha wa Sala Kuombea Amani Mashariki ya Kati

Viongozi wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo wamekazia uekumene wa sala, huduma, ushuhuda, umoja na amani duniani.

Viongozi wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo wamekazia uekumene wa sala, huduma, ushuhuda, haki, amani, umoja na mshikamano wa wakristo!

Siku ya Sala ya Kiekumene Bari: Uekumene wa sala, umoja na amani!

08/07/2018 08:48

Siku ya Sala ya Kiekumene huko Bari, Kusini mwa Italia, imehudhuriwa na viongozi wakuu wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo huko Mashariki ya Kati kwa kukazia asili ya maisha na utume wa Kanisa; umuhimu wa kukuza na kudumisha uekumene wa sala, huduma, ushuhuda, umoja na amani duniani!

Viongozi wakuu wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo wanaitaka Jumuiya ya Kimataifa kusikiliza kilio cha watoto Mashariki ya Kati!

Viongozi wa Makanisa na Jumuiya za Kikristo wanaitaka Jumuiya ya Kimataifa kusikiliza kilio cha watoto wanaoteseka huko Mashariki ya Kati kutokana na vita, nyanyaso na dhuluma.

Papa Francisko: Kilio cha watoto Mashariki ya Kati kisute dhamiri zenu

08/07/2018 08:20

Baba Mtakatifu Francisko kwa niaba ya viongozi wa Makanisa na Jumuiya ya Kikristo katika hotuba yake ya kufunga Siku ya Sala ya Kiekumene iliyofanyika Bari, Italia, amewataka watu kuguswa katika dhamiri zao na kilio cha watoto wanaoteseka kutokana na vita, kiasi cha kukosa mahitaji msingi!

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI limepewa dhamana ya kuandaa mkesha wa Sala ya Kiekumene kwa ajili ya amani na umoja Mashariki ya Kati.

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI limepewa dhamana ya kuandaa mkesha wa sala ya kuombea amani na umoja huko Mashariki ya Kati.

Mkesha wa Sala ya Kiekumene kuombea amani na umoja Mashariki ya Kati

05/07/2018 16:51

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI limechukua dhamana ya kuandaa Mkesha wa sala ya Kiekumene kwa ajili ya kuombea amani na umoja huko Mashariki ya Kati utakaofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Nicholaus wa Bari, Ijumaa tarehe 6 Julai 2018. Wakuu wa Makanisa wanakutana 7 Julai 2018.