Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Miito Mitakatifu

Shirika la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili la Watawa wa Armenia linamehitimisha kilele cha miaka 170 ya uwepo na utume wake kati ya maskini!

Shirika la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi la Asili limehitimisha kilele cha maadhimisho ya miaka 170 ya uwepo na utume wake miongoni mwa watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na huduma ya elimu kwa vijana wa kizazi kipya.

Watawa waadhimisha kilele cha kumbu kumbu ya miaka 170 ya utume!

05/06/2018 14:30

Shirika la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili la Watawa wa Armenia, linaadhimisha kilele cha kumbu kumbu ya miaka 170 tangu kuanzishwa kwake na kuanza kujikita katika ukarimu kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na elimu makini kwa vijana!

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi ya kiutu, kijamii na maisha ya kiroho.

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi na majiundo ya kiutu, maisha ya kiroho na kitamaduni.

Askofu Kassala: familia ni chemchemi ya malezi na majiundo ya kiutu

19/05/2018 14:10

Familia ni Kanisa dogo la nyumbani, shule ya utakatifu, haki, amani, upendo na maridhiano. Ni mahali pa kwanza kabisa pa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya kiutu, maisha ya kiroho, kijamii na kitamaduni. Familia ni mahali pa kutakatifuzana katika ndoa! Ni shule ya huruma na upendo.

 

Miito mingi ya kikuhani na utawa inazidi kuongezeka nchini Bangladesh

Miito mingi ya kikuhani na utawa inazidi kuongezeka nchini Bangladesh

Bangladesh miito inaongezeka na jimbo la Sylhet seminari mpya kuzinduliwa!

29/01/2018 14:22

Miito ya kitawa inazidi kuongezeka katika maeneo ya makabila huko Bangladesh.Kwa siku zilizo pita imezinduliwa seminari ya Jimbo la Sylhet,Kaskazini ya nchi.Ni Seminari ya Mtakatifu Yohane iliyofadhiliwa na Jimbo Katoliki la Suwon nchini Korea ya Kusini,ambayo itawakaribisha waseminari 60.

 

Vijana wanahitaji kusindikizwa ili wasikosee mang'amuzi ya miito yao

Vijana wanahitaji kusindikizwa ili wasikosee mang'amuzi ya miito yao

Kardinali Bassetti anasema vijana wasaidiwe katika miito yao ya maisha!

04/01/2018 14:57

Kwa vijana inahitajika kuwasha cheche za matumaini ya kujitoa na si kujifunga binafsi.Kujitwika mzigo kwa upendo na kuwasaidia wengine: bahati mbaya kadiri siku zinavyokwenda mbele,upo utambuzi kwamba,wapo vijana ambao ni kama sehemu za pembezoni,wenye kuhitaji msaada wa maisha.

 

Papa amekutana na kuuzungumza na washiriki wa Mkutano  Mkuu wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu na mwanzilishi Padre Jean Jules Chevalier

Papa amekutana na kuuzungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu na mwanzilishi Padre Jean Jules Chevalier miaka 150 iliyopita

Msiogope kushirikisha utajiri wa tasaufi ya Shirika lenu kwa walei

16/09/2017 16:39

Baba Mtakatifu amekutana na kuzungumza na wanashirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, katika tukio la Mkutano Mkuu wa Shirika lililoanzishwa na Padre Jean Jules Chavalier. Baba Mtakatifu anasema kauli mbiu  yao "Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa" ni muhimu katika maisha yao ya utume

 

 

Papa Francisko anasema, wito wa kweli unapatikana kwa mwamini kukutana na Kristo Yesu katika hija ya maisha yake!

Papa Francisko anasema, wito wa kweli unapata chimbuko lake kwa mwamini kukutana na Kristo Yesu katika hija ya maisha yake kama ilivyokuwa kwa mitume wake wa mwanzo mwanzo!

Wito wa kweli unapata chimbuko lake kwa kukutana na Kristo Yesu!

30/08/2017 15:11

Baba Mtakatifu Francisko anasema, wito wa kweli unapata chimbuko lake kwa kukutana na Kristo Yesu katika maisha na hivyo kuanza ujenzi wa urafiki na upendo wa dhati kiasi hata cha kujisikia "nyumbani" kama ilivyokuwa kwa Mitume wa Yesu wa kwanza walionesha udadisi na hatimaye kumfuasa Kristo!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa mwezi Juni!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay, Mwezi Juni 2017 linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu.

Mwezi wa kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa

19/06/2017 14:27

Kanisa Katoliki nchini Uruguay limeutenga mwezi Juni, 2017 kuwa ni mwezi wa kuombea miito mbali mbali ndani ya Kanisa: wito wa Upadre, ili Kanisa liweze kupata Mapadre: wema, watakatifu na wachamungu; watawa watakaojisadaka kwa ajili ya huduma makini na familia kama Kanisa dogo ya nyumbani.