Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Miaka 70 Baraza la Makanisa Ulimwenguni

Yaliyojiri wakati wa mahojiano kati ya Papa Francisko na Waandishi wa Habari wakiwa njiani kutoka Geneva, Uswiss, 21 Juni 2018.

Yaliyojiri katika mahojiano maalum kati ya Papa Francisko na waandishi wa habari wakati akiwa njiani kutoka Geneva Uswiss, tarehe 21 Juni 2018.

Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Papa Francisko na Wanahabari!

23/06/2018 16:00

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hija yake ya kiekumene nchini Uswiss imemwezesha kukutana na viongozi mbali mbali wa Kanisa wanaoendelea kujizatiti kwa ajili ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika kutembea, kusali na kushirikiana kama ushuhuda wa uinjilishaji mpya!

Papa Francisko amewaishukuru kwa dhati familia ya Mungu nchini Uswiss kwa mapokezi na ukarimu wake!

Papa Francisko ameishukuru kwa dhati familia ya Mungu nchini Uswiss kwa mapokezi maito na ukarimu wao kwake na kuwataka waendelee kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene!

Papa Francisko aonesha moyo wa shukrani nchini Uswiss!

22/06/2018 17:12

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anarejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kiekumene nchini Uswiss, ameishukuru familia ya Mungu nchini humo kwa mapokezi makubwa na moyo wa ukarimu, akawatakia wananchi wa Italia, heri, baraka na ustawi, baada ya kukutana mahujaji wa kiekumene!

Papa Francisko katika Ibada ya Misa Takatifu ametafakari kuhusu: Sala ya Baba Yetu Uliye mbinguni.

Papa Francisko katika Ibada ya Misa Takatifu mjini Geneva ametafakari kuhusu: Sala ya Baba Yetu uliye mbinguni.

Papa Francisko: Sala ya Baba Yetu: Baba! Chakula na Msamaha wa kweli!

22/06/2018 10:00

Baba Mtakatifu Francisko katika Ibada ya Misa Takatifu mjini Geneva, amefafanua kwa kina na mapana Sala ya Baba Yetu kwa kukazia: Baba Yetu kuwa ni ufunguo wa Sala kuu aliyofundisha Kristo Yesu; Umuhimu wa kuomba mahitaji ya kila siku pamoja na kusamehe kama sharti la kupokea msamaha na neema.

Papa Francisko anaishukuru sana familia ya Mungu nchini Uswiss kwa moyo wa upendo na ukarimu!

Papa Francisko anaishukuru sana familia ya Mungu nchini Uswiss kwa moyo wa upendo na ukarimu.

Papa Francisko aishukuru familia ya Mungu Uswiss kwa moyo wa ukarimu

22/06/2018 09:47

Mji wa Geneva nchini Uswiss una umaarufu wake katika medani za kimataifa kwani huu ni mji ambamo kuna Makao makuu ya Mashirika ya Kimataifa. Baba Mtakatifu amelitaja Shirika la Kazi Duniani ambalo mwaka 2019 linaadhimisha Jubilei ya Miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, lakini changamoto zipo kibao!

Hija ya kiekumene ya Papa Francisko nchini Uswiss ni kuimarisha majadiliano ya kiekumene pamoja na kukutana na Wakatoliki kutoka Uswiss.

Hija ya Kiekumene ya Papa Francisko nchini Uswiss ni kutaka kuimarisha majadiliano ya kiekumene pamoja na kukutana na waamini wa Kanisa Katoliki.

Hija ya Kiekumene ya Papa Francisko yawasha moto wa kiekumene Geneva!

21/06/2018 17:55

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kiini cha hija yake ya kiekumene nchini Uswiss inayoongozwa na kauli mbiu: "Kutembea, kusali na kushirikiana" ni kumwezesha kukutana na Wakatoliki ndani na nje ya Uswiss, lakini zaidi, kuimarisha mchakato wa majadiliano ya kiekumene kati ya Makanisa!

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja!

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja.

Papa Francisko: Wakristo wanapaswa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana

21/06/2018 17:38

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Kiekumene, amekazia kwa namna ya pekee kabisa umuhimu wa Wakristo kutembea, kusali na kushirikiana, ili kuwapeleka watu kwa Kristo Yesu; kwa kujenga na kudumisha umoja na udugu katika sala na huduma kwa maskini!

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho!

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni, WCC. Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho kama alama na kielelezo makini cha uinjilishaji.

WCC: Ulimwengu uliomeguka unahitaji alama na ushuhuda wa nguvu!

21/06/2018 17:20

Walimwengu waliogawanyika na kusambaratika juu ya uso wa dunia, wanahitaji alama na ushuhuda wenye mvuto na mashiko, changamoto na mwaliko kwa Wakristo kujipatanisha, kudumisha umoja, kulinda maisha na kutunza mazingira nyumba ya wote, daima haki msingi za binadamu zikipewa kipaumbele!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko asema, Wakristo wanahimizwa kuenenda katika Roho!

21/06/2018 16:56

Baba Mtakatifu Francisko katika Ibada ya sala ya toba, upatanisho na umoja wa Makanisa amewataka Wakristo kuenenda katika Roho kwa kutambua kwamba, binadamu hapa duniani ni hujaji na kwamba, kuenenda katika Roho ni kiini cha wito na maisha ya Kikristo; ni kujikita katika msamaha na huduma!