Mitandao ya kijamii:

RSS:

App:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Matendo ya Huruma: Kiroho na Kimwili

Mitume na mashuhuda wa huruma ya Mungu ni wale walioguswa kwa Fumbo la Msalaba, wakawa tayari kuishuhidia huruma ya Mungu kwa jirani zao!

Mitume na mashuhuda wa huruma ya Mungu ni watu walioguswa na Fumbo la Msalaba, wakawa tayari kuandika Injili ya huruma ya Mungu katika uhalisia wa maisha yao ya kila siku!

Jifunzeni huruma ya Mungu kutoka kwa Kristo na mashuhuda wake!

22/04/2017 10:11

Maadhimisho ya Jumapili ya huruma ya Mungu imekuwa ni nafasi muafaka sana kwa mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania kutembelea Kituo cha hija cha Kiabakari Jimbo Katoliki Musoma kwa ajili ya kushiriki novena, hija, mkesha na hatimaye, maadhimisho ya Jumapili ya huruma ya Mungu!

 

Mwaka wa huruma ya Mungu umewawezesha watu wengi kuguswa na huruma na upendo wa Mungu kutoka kwa Kristo  na Kanisa lake!

Mwana wa huruma ya Mungu umewawezesha watu wengi kuguswa na huruma na upendo wa Mungu unaobubujika kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake anasema Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania.

Matunda ya Maadhimisho ya Mwaka wa huruma, Jimbo kuu la Mwanza!

20/04/2017 11:00

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania anasema, baada ya familia ya Mungu Jimbo kuu la Mwanza kukitumia vyema kipindi cha maadhimisho pamoja na nyongeza yake, Jumapili ya huruma ya Mungu, tarehe 23 Aprili 2017 wanaufunga rasmi mwaka wa huruma, lakini...!

Huruma ya Mungu ndiyo msingi thabiti wa uhai wa Kanisa.

Huruma ya Mungu ndiyo msingi thabiti wa uhai wa Kanisa.

Jumapili ya huruma ya Mungu

19/04/2017 12:14

Baba Mtakatifu Francisko anasema, huruma ya Mungu ndiyo sababu ya mahangaiko ya upendo wake kwa binadamu. Mwenyezi Mungu anajisikia kuwajibika kwa maana kwamba, anatamani kumwona mwanadamu akiwa na afya, furaha na amani tele moyoni mwake; mwaliko wa kuwa vyombo vya huruma!

 

Askofu mkuu Ruwaichi anawaalika waamini kujiandaa vyema ili kushiriki kikamilifu Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu.

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza anawaalika waamini kujiandaa vyema kuadhimisha Fumbo la Pasaka,yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu.

Jiandaeni vyema kuadhimisha Fumbo la Pasaka

12/04/2017 10:40

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi anawaalika waamini kujiandaa kikamilifu katika maadhimisho ua Fumbo la Pasaka; kwa toba na wongofu wa ndani; kwa sala na tafakari ya kina ya Neno la Mungu; Sakramenti za Kanisa na matendo ya huruma, ili kufundwa a kugangwa na neema ya Mungu katika maisha!

Baada ya maadhimisho ya mwaka wa huruma ya Mungu muhimu: wongofu wa kimissionari, majiundo na matendo ya huruma

Baada ya maadhimisho ya Mwaka wa huruma ya Mungu, sasa kuna haja ya kukazia wongofu wa kimissionari unaofumbatwa katika kutangaza na kushuhudia huruma ya Mungu, majiundo makini pamoja na matendo ya huruma: kiroho na kimwili.

Baada ya Mwaka wa huruma ya Mungu mambo msingi ya kuzingatia!

15/03/2017 09:27

Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu imekuwa ni fursa makini ya kutafakari mambo msingi ya imani ya Kikristo yaani huruma ya Mungu! Sasa kuna haja ya kuendeleza wongofu wa kimissionari, majiundo makini na endelevu pamoja na matendo ya huruma: kiroho na kimwili.

Hija ya kwaresima ni mwaliko kwa waamini kujifunza na kumwilisha imani yao katika matendo!

HIja ya Kwaresima ni mwaliko kwa waamini kujifunza kutenda matendo mema na kuyamwilisha katika uhalisia wa maisha kama kielelezo cha imani tendaji!

Papa Francisko: Jifunzeni kutenda mema!

14/03/2017 14:40

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hija ya kipindi cha Kwaresima inajikita katika toba na wongofu wa ndani unaofumbatwa katika ukujifunza kutenda mema kwa vitendo na wala si kwa maneno kwani maneno matupu kamwe hayawezi kuvunja mfupa! Matendo ni kielelezo cha imani kwa Kristo na Kanisa lake!

Baba Mtakatifu Francisko katika waraka wake wa kitume anakazia umuhimu wa mshikamano na upendo kama tunu msingi za maisha ya kijamii!

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa kitume Huruma na amani anakazia umuhimu wa upendo na mshikamano kama tunu msingi za maisha ya kijamii.

Huruma ya Mungu kama tunu msingi ya maisha ya kijamii!

09/03/2017 15:55

Matendo ya huruma yanayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu sehemu mbali mbali za dunia ni kielelezo cha uwepo endelevu wa kazi ya ukombozi iliyoanzishwa na Kristo Yesu, kazi inayofanywa na Mama Kanisa kwa wakati huu, kumbe, waamini wanapaswa kuwa ni mashuhuda wa huruma!

 

Ghana inaadhimisha Kumbu kumbu ya Miaka 40 ya Uhusiano wa kidiplomasia na Vatican na Miaka 60 ya Uhuru wake

Ghana inaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia na Vatican na miaka 60 ya uhuru kutoka kwa Waingereza kunako tarehe 6 Machi 1957.

Familia ya Mungu Ghana yawekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu!

07/03/2017 08:04

Kardinali Giuseppe Bertello, mwakilishi maalum wa Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Kumbu kumbu ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ghana na Vatican sanjari na kumbu kumbu ya miaka 60 ya uhuru wa Ghana, ameiweka Ghana wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.