Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa

Papa Francisko katika kipindi cha miaka mitano amekazia: Huruma ya Mungu, Maskini; Kutoka kwenda kuinjilisha, Pembezoni mwa Jamii na uwepo wa Ibilisi.

Papa Francisko katika kipindi cha miaka mitano ya maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro amekazia zaidi kuhusu: Huruma ya Mungu, Maskini kama amana na utajiri wa Kanisa, Umuhimu wa kutoka kwenda kuinjilishaji, Pembezoni mwa Jamii na uwepo wa Ibilisi, shetani!

Papa Francisko: Mkazo: Huruma, Maskini, Pembezoni, Kutoka & Ibilisi

14/03/2018 08:20

Baba Mtakatifu Francisko anapoadhimisha kumbu kumbu ya Miaka mitano tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro amekazia zaidi kuhusu; huruma ya Mungu; Maskini kama amana na utajiri wa Kanisa; Ibilisi na Umuhimu wa kutoka na kwenda pembezoni mwa jamii.

Mwenyeheri Paulo VI kutangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 2018

Mwenyeheri Paulo VI kutangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 2018.

Mwenyeheri Paulo VI & Oscar Romero kutangazwa watakatifu mwaka 2018

12/03/2018 12:02

Wakati huu Mama Kanisa anapoendelea kujizatiti zaidi katika kuimarisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, Baba Mtakatifu Francisko ameridhia kwamba, Mwenyeheri Paulo VI aliyesimama kidete kutangaza Injili ya uhai pamoja na Askofu mkuu Oscar Romero watangazwe kuwa watakatifu mwaka 2018

Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa, walengwa wakuu wa Habari Njema ya Wokovu!

Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa, walengwa wakuu wa Habari Njema ya Wokovu!

Kardinali Sèrgio da Rocha: Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa!

15/01/2018 14:05

Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa katika mchakato mzima wa Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili. Kimsingi, maskini ndio walengwa wakuu wa Habari Njema ya Wokovu! Dhana ya umaskini inajikita katika: utu na heshima ya binadamu; kanuni maadili na utu wema!

Tunaalikwa wote kutokuwa na tabia za kiburi, bali kuwa watu wa kawaida na kujikita kwanza katika kumtafuta na kufuata Yesu.

Tunaalikwa wote kutokuwa na tabia za kiburi, bali kuwa watu wa kawaida na kujikita kwanza katika kumtafuta na kufuata Yesu.

Papa:Sisi sote ni ndugu hatuna haja ya kujiona bora zaidi ya wengine!

06/11/2017 10:31

Madaraka yoyote yakitumika vibaya yanaunda ukosefu wa uaminifu na kuleta  vizingiti, lakini mitume wa Yesu wanaalikwa kuwa makini na wasijiweke juu ya wengine kwa hali yoyote badala yake watoe huduma. Haya ni maonyo katika mahubiri ya Baba Mtakatifu wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana

 

 

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua uwepo wa Mungu kati ya maskini.

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua uwepo wa Mungu kati ya maskini.

Kardinali Parolin; jitahidini kumwona Mwenyezi Mungu kati ya maskini

28/08/2017 09:03

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujitahidi kumwona Mungu kati ya maskini! Kanisa linataka kuwekeza kwa elimu makini kwa ajili ya vijana na kwamba, kuna haja ya kudhibiti utandawazi kwa kujenga umoja na mshikamano wa dhati!

Familia ya Mungu Amerika ya Kusini inaadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 300 ya Bikira Maria wa Aparecida

Familia ya Mungu Amerika ya Kusini inaadhimisha Jubilei ya Miaka 300 tangu Sanamu ya Bikira Maria wa Aparecida ilipookotwa na wavuvi, mwanzo wa Ibada kwa Bikira Maria wa Aparecida.

Utenzi wa Bikira Maria unapoimbwa na maskini, utamu wake unaongezeka!

17/08/2017 12:05

Utenzi wa Bikira Maria maarufu kama "Magnificat" unakazia utu, heshima, upendo na mshikamano miongoni mwa binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Ni utenzi unaowatetea wanyonge dhidi ya nyanyaso na ukosefu wa haki msingi za binadamu; huu ni mwaliko wa kushiriki kazi ya ukombozi!

Taarifa zinaonesha kwamba, kuna wakimbizi na wahamiaji ambao kwa sasa wanazamishwa baharini ili kufuta ushahidi dhidi ya wafanya biashara ya binadamu!

Taarifa zinaonesha kwamba, kuna wakimbizi na wahamiaji wanaozamishwa baharini ili kufuta ushahidi dhidi ya wafanyabiashara ya binadamu!

Changamoto mamboleo: fursa za ajira na huduma makini kwa wakimbizi!

11/08/2017 13:45

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linasema, kwa sasa changamoto kubwa inayoikabilia Jumuiya ya Kimataifa ni fursa za ajira kwa wafanyakazi, ili waweze kutekeleza dhamana na wajibu wao barabara sanjari na huduma makini kwa wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta: usalama, hifadhi na maisha bora zaidi.

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: " Kauli mbiu: Tusipende kwa neno bali kwa tende"

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: Kauli mbiu " Tusipende kwa neno bali kwa tendo".

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Kwanza ya Maskini Duniani 2017

13/06/2017 15:34

Siku ya kwanza ya Maskini Duniani iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu itaadhimishwa hapo tarehe 19 Novemba 2017. Kauli mbiu "Tusipende kwa neno bali kwa tendo".