Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mashuhuda wa Kristo Mfufuka

Papa Francisko anawataka waamini kuwa huru kabisa katika kumtangaza na kumshuhudia Kristo hata katika mateso!

Papa Francisko anawataka waamini kuwa huru kabisa katika mchakato wa kumtangaza na kumshuhudia Kristo hata katika mateso, dhuluma na nyanyaso!

Papa Francisko: Jitahidini kuwa na uhuru wa kweli hata katika mateso!

13/04/2018 14:58

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini kuhakikisha kwamba, wanakuwa na uhuru wa kweli hata katika shida, mahangaiko na mateso yao, tayari kumshunudia Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu! Mitume Petro na Yohane wawe ni mifano bora ya kuigwa katika kumshuhudia Kristo!

Kristo Mfufuka alijitahidi kuwafunulia wafuasi wake Fumbo la Ufufko na kuwaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu!

Kristo Yesu Mfufuka alijitahidi kuwafunulia Mitume wake Fumbo la Ufufuko kiasi cha kuwaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu.

Kristo Mfufuka ameondoa hofu na mashaka, sasa ni ushuhuda tu!

12/04/2018 15:50

Kristo Mfufuka alijitahidi kuwafafanulia wafuasi wake kuhusu Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wake, kwa kuwashirikisha wafuasi wake uhalisia wa maisha yake kama Mfufuka, akawaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu ili kuonja uwepo wake endelevu kama ilivyo hata katika kuumega mkate.

Papa Francisko asema, furaha ya Pasaka inafumbatwa katika utii na ushuhuda unaomwilishwa katika uhalisia wa maisha.

Papa Francisko asema, furaha ya Pasaka inasimikwa katika utii na ushuhuda unaomwilishwa katika uhalisia wa maisha, kielelezo cha imani tendaji!

Furaha ya Pasaka inafumbatwa katika utii na ushuhuda unaomwilishwa!

12/04/2018 15:08

Baba Mtakatifu Francisko anasema, furaha ya Fumbo la Pasaka inasimikwa katika utii katika kutekeleza mapenzi ya Mungu na ushuhuda wa imani wa imani tendaji inayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu! Wakristo wajitahidi kumwomba Mungu neema na baraka ya kudumu katika imani na matumaini!

Kristo Mfufuka aliwaimarisha wanafunzi wake katika imani, matumaini na mapendo kwa kutembea, kuzungumza, kula pamoja na kuwapatia nafasi ya kumgusa.

Kristo Mfufuka aliwaimarisha wanafunzi wake kwa kutembea pamoja nao njiani, kuwafafanulia Maandiko Matakatifu, kula pamoja na kuwaruhusu kumgusa!

Waamini shindeni woga ili kumtangaza na kumshuhudia Kristo Mfufuka!

11/04/2018 15:44

Yesu Mfufuka alianzisha uhusiano na mafungano ya pekee na wafuasi wake waliokuwa wamegubikwa kwa hofu na mashaka makuu baada ya mateso na kifo chake Msalabani! Akatembea nao njiani ili kuwafafanulia Maandiko Matakatifu, akawaruhusu kumgusa na hatimaye kula chakula pamoja nao, wakamtambua!

 

Papa Francisko: shikamaneni na Kristo katika ubinadamu wake, mwabuduni katika Umungu wake na shibabeni na kulandana na Kristo kwa njia ya Neno!

Papa Francisko: shikamaneni na Kristo katika ubinadamu wake; mwabuduni katika Umungu wake na shikamaneni na kulandana naye kwani ni chemchemi ya maisha ya kiroho.

Papa Francisko: Mapadre na watawa muwe mashuhuda wa furaha ya Injili

10/09/2017 15:03

Papa Francisko anawataka Mapadre na watawa kushikamana na Kristo Yesu katika ubinadamu wake kwa njia ya huduma makini; washikamane na Kristo Yesu katika kuabudu Umungu wake na daima wabaki wakiwa wameshibana na kulandana na Kristo Yesu, chemchemi ya furaha ya Injili kwa watu wake!

Utukufu, ukuu na uweza wa Mungu unafumbatwa katika Fumbo la Msalaba!

Utukufu, ukuu na uweza wa Mungu vinafumbatwa katika Fumbo la Msalaba, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu.

Utukufu, ukuu na uweza wa Mungu unang'ara katika Fumbo la Msalaba

04/08/2017 08:49

Siku kuu ya kung'ara kwa Bwana ni ushuhuda wa ufunuo wa utukufu, ukuu na uweza wa Kristo Yesu, kama sehemu ya maandalizi ya kurejea tena kwa Baba yake wa Mbinguni kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake. Hii ni sherehe inayowafunulia waamini Fumbo la Pasaka; Siku za Mwisho na Maisha ya Kristo!

Papa Francisko anawaalika Wakristo kuwa mashuhuda amini wa Kristo na Kanisa lake na kamwe wasiogope!

Papa Francisko anawaalika Wakristo kuwa mashuhuda amini wa Kristo na Kanisa lake na kamwe wasiogope!

Papa Francisko: Iweni mashuhuda waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake!

26/06/2017 09:11

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika Wakristo kuwa ni mashuhuda amini na waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake, wasiogope: mauaji, mateso, dhuluma na nyanyaso kwani hii ni sehemu yua vinasaba vya maisha na utume wa Kikristo ulimwenguni, watambue kwamba, wanathaminiwa na Kristo Yesu!

Mwenyeheri Askofu mkuu Teofilius Matulionis alimshuhudia Kristo kwa kumwaga damu yake!

Mwenyeheri Askofu mkuu Teofilius Matulionis alimshuhudia Kristo Yesu kwa njia ya mateso makali hadi kuyamimina maisha yake kama kielelezo cha imani yake kwa Kristo na Kanisa lake!

Mwenyeheri Teofilius Matulionis alimshuhudia Kristo kwa kumwaga damu!

23/06/2017 08:52

Mtumishi wa Mungu Askofu mkuu Teofilius Matulionis, aliyemshuhudia Kristo Yesu na Kanisa lake kwa kujisadaka na hatimaye kuyamimina maisha yake kama kielelezo cha imani tendaji anatangazwa kuwa Mwenyheri, ili aendelee kuwa ni mfano bora wa kuigwa katika ushuhuda wa imani kwa Kristo!