Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mashuhuda wa Injili ya Kristo

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja!

Wakristo wanahamasishwa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kwa pamoja.

Papa Francisko: Wakristo wanapaswa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana

21/06/2018 17:38

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Kiekumene, amekazia kwa namna ya pekee kabisa umuhimu wa Wakristo kutembea, kusali na kushirikiana, ili kuwapeleka watu kwa Kristo Yesu; kwa kujenga na kudumisha umoja na udugu katika sala na huduma kwa maskini!

Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo Yesu na ufunuo mkamilifu wa Fumbo la Utatu Mtakatifu.

Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo Yesu na ufunuo mkamilifu wa Fumbo la Utatu Mtakatifu.

Sherehe ya Pentekoste: Utatu Mtakatifu unafunuliwa kikamilifu!

17/05/2018 07:00

Mababa wa Kanisa wanafundisha na kusadiki kwamba, Sherehe ya Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo kwa kummimina Roho Mtakatifu, ambaye ametolewa na kushirikishwa kama nafsi ya Mungu. Hii ni siku ambayo Fumbo la Utatu Mtakatifu limefunuliwa kikamilifu, tayari kutangaza Ufalme wa Mungu.

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawaachia wakristo wajibu wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawachia Wakristo wajibu na dhamana ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.

Leo mnatumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

11/05/2018 16:11

Ee Mungu Mwenyezi, utufanye tuwe na furaha takatifu na shukrani; kwa maana kupaa kwake Kristo Yesu, Mwanaoni mfano wetu; na huko alikotangulia yeye kichwa chetu, ndiko tunakotumaini kufika sisi tulio mwili wake. Leo ubinadamu wetu umetukuzwa mbinguni!

Askofu mkuu Rastislav akazia umuhimu wa Maandiko Matakatifu, Mapokeo ya Kanisa na Utamadunisho katika majadiliano ya kiekumene.

Askofu mkuu Rastislav akazia umuhimu wa Maandiko Matakatifu kama njia ya kumtambua Kristo Yesu, Mapokeo ya Kanisa na Utamadunisho.

Askofu mkuu Rastilav akutana na kuzungumza na Papa Francisko!

11/05/2018 15:03

Askofu mkuu Rastilav wa Jimbo kuu la Presov, Kiongozi mkuu wa Kanisa la Kiorthodox wa nchi ya Czech na Slovakia katika hotuba yake amekazia umuhimu wa Maandiko Matakatifu, Mapokeo ya Kanisa na Utamadunisho kama njia muafaka za kuendeleza majadiliano ya kiekumene kati ya Wakristo!

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Kristo Yesu akishakuinuliwa juu, atawavuta wote kwake!

10/05/2018 16:31

Kristo Yesu peke yake ndiye aliyetoka kwa Baba na anaweza kurudi tena kwa Baba. Hakuna mtu aliyepaa mbinguni ile Yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa mtu! Ubinadamu ukiachiwa katika nguvu zake za maumbile hauwezi kufika kwenye nyumba ya Baba, kwenye uzima na furaha ya milele!

 

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni.

Sherehe ya Bwana Kupaa Mbinguni!

10/05/2018 15:23

Mama Kanisa anasadiki na kufundisha kwamba, Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi, atarudi kuwahukumu wazima na wafu na wala ufalme wake hautakuwa na mwisho: Ubinadamu wa Yesu unamficha mbele ya macho ya watu. Yesu amewatangulia waja wake katika Ufalme wa utukufu

Kristo Yesu ni Mzabibu wa kweli, Baba yake ni Mkulima na wafuasi wake ni matawi!

Kristo Yesu ni Mzabibu wa kweli, Baba yake ni Mkulima na wanafunzi wake wote ni matawi yanayopaswa kubaki yameshikamana na Mzabibu ili yaweze kuzaa matunda ya wongofu na utakatifu wa maisha.

Kumbukeni kwamba, Mimi ni Mzabibu nanyi ni matawi!

27/04/2018 15:49

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya V ya Kipindi cha Pasaka inaweka mbele ya macho ya waamini uhusiano wa dhati uliopo kati yao, Kristo Yesu na Mwenyezi Mungu. Kristo Yesu ndiye Mzabibu wa kweli na Baba yake wa mbinguni ndiye mkulima na wafuasi wake ni matawi, kumbe wanapaswa kushibana.

 

Yesu ni mzabibu wa kweli na Baba yake ndiye mkulima!

Yesu ni mzabibu wa kweli na Baba yake ndiye mkulima!

Msipoungana na Kristo Yesu, mtazaa Zabibu mwitu!

27/04/2018 07:56

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya V ya Kipindi cha Pasaka inamwonesha Kristo Yesu akijitambulisha kuwa ni Mzababu wa kweli na Baba yake wa mbinguni ndiye mkulima! Waamini wakikaa na kuungana naye, hapo waweza kuzaa matunda ya haki, amani, ukweli na upatanisho!