Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mashuhuda wa huruma

Papa Francisko anawataka viongozi wa Kanisa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa huduma kwa familia ya Mungu!

Papa Francisko anawataka viongozi wa Kanisa kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huduma kwa familia ya Mungu.

Papa Francisko ataja sifa za kiongozi bora!

22/06/2017 17:27

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican amefafanua kwa kina na mapana sifa za kiongozi bora: ni mtu anayejitosa bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma; mtu anayethubutu kujisadaka na mwenye mang'amuzi makini katika maisha.

Papa Francisko anawataka wakleri kuachana na tabia ya kupinga kila jambo; kujenga mahusiano mema na watu na kumwilisha huduma katika uhalisia wa watu.

Papa Francisko anawataka wakleri kuachana na tabia ya kupinga kila jambo, kujenga mahusiano mema na watu wanaowahudumia pamoja na kuhakikisha kwamba, huduma za kiroho zinamwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu.

Padre Primo Mazzolari, alikuwa ni Baba wa maskini na waliotelekezwa!

20/06/2017 16:48

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwaonya Mapadre kuachana na tabia ya kupinga kila jambo linalojitokeza mbele yao! Kuepuka tabia ya kufanya kazi nyingi bila kujenga mahusiano mema na watu wanaowahudumia; tatu washughulikie mambo ya kiroho kwa kushuka katika uhalisia wa maisha ya watu!

 

Papa Francisko anawaalika waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya faraja na huduma ya Mungu kwa jirani zao!

Papa Francisko anawaalika waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya faraja na huduma ya Mungu kwa jirani zao!

Waamini wanahamasishwa kuwa ni vyombo vya faraja na huduma kwa jirani

12/06/2017 15:55

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuwa ni vyombo na mashuhuda wa faraja na huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kwa kujikita katika Heri za Mlimani, muhtasari wa Mafundisho Makuu ya Yesu!

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo mitume walitoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kuhusu: mateso, kifo na ufufuko wa Yesu.

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo Mitume walishukiwa na Roho Mtakatifu, wakatoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kwamba, Kristo Yesu aliyeteswa, akafa amefufuka kwa wafu! Hiki ni kiini cha imani na matumaini ya Kanisa.

Siku kuu ya Pentekoste, Siku ya kuzaliwa kwa Kanisa!

01/06/2017 14:40

Pentekoste ni Siku ambayo Kanisa linaadhimishwa kuzaliwa kwake kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwashukia Mitume na hivyo kuwapatia nguvu, ujasiri, ari na moyo mkuu wa kuweza kutoka kifua mbele kutangaza na kushuhudia kwamba, Yesu aliyeteswa, akafa, akafufuka amepaa mbinguni! Kiini cha imani yetu!

Sifa za mmissionari wa kweli: mtu huru, mwepesi anayejikita katika toba na wongofu wa ndani; ni maskani ya Kristo na Roho Mtakatifu. anayewafundisha!

Sifa za mmissionari wa kweli: mtu huru, anayejitaabisha kwa toba na wongofu wa ndani kwa ajili ya wongofu wa shughuli za kitume. Ni maskani ya Yesu na Roho Mtakatifu.

Papa Francisko: Jitoeni kwa Mungu ili kuwa yote kwa ajili ya jirani!

26/05/2017 15:03

Baba Mtakatifu Francisko anasema, mmissionari anapaswa kuwa ni mtu huru asiyemezwa na malimwengu; mwepesi kwa kujitaabisha kwa ajili ya wongofu wa kichungaji kwa toba na wongofu wa ndani; ni mtu anayeyasimika maisha yake kwa Roho Mtakatifu ili kukumbushwa, kufundishwa na kuelekezwa!

Kardinali Filoni anaonya waamini wa Jimbo jipya la Vinayong wasipande magugu mabaya katika shamba la Bwana,kwa maana ,kueneza vurugu,chuki,masengenyo

Kardinali Filoni anaonya waamini wa Jimbo jipya la Vinayong wasipande magugu mabaya katika shamba la Bwana,kwa maana ya kueneza vurugu,chuki,masengenyo

Kard. Filoni: Kila mbatizwa atoe ushuhuda wa kutangaza Yesu mfufuka

22/05/2017 14:11

Kama alivyo fanya Mtakatifu Filipo huko Samaria, ndivyo ilivyokuwa miaka ya1645 ndugu Wafranciskani Wakapuchini wa kwanza walifika Equatorial Guinea ya sasa.Hawa ni kama wamisionari wengine waliofuatia Mapadri wa Jimbo la Toledo,Wayesuiti na zaidi Waklaretiani,walihubiri Yesu katika ardhi hii 

 

Mwongozo mpya wa malezi na majiundo ya kipadre unakazia: ukomavu wa maisha ya kiroho na kiutu: kwa kuzingatia: utu, tasaufi na huduma makini!

Mwongozo mpya wa malezi ya kipadre unazingatia ukuaji wa mtu mzima: kiroho na kuiutu; kwa kujikita zaidi katika ukomavu wa dhamiri, tasaufi na kwamba, mapadre ni vyombo na mashuhuda wa huduma makini kwa familia ya Mungu!

Mwongozo Mpya wa Malezi na Majiundo ya Kipadre

03/05/2017 06:53

Kardinali Beniamino Stella anasema, malezi na majiundo ya kipadre yanapaswa kupyaishwa, kuendelezwa na kupewa kipaumbele cha pekee katika maisha na utume wa Kanisa. Malezi yazingatie ukuaji wa mtu mzima: kiroho na kimwili; yakazie: utu katika ukomavu; tasaufi na dhamiri nyofu pamoja na huduma!

Ibada kwa huruma na Mungu na kwa Bikira Maria ni nyenzo muhimu katika kutafuta na kuambata utakatifu wa maisha!

Ibada ya huruma ya Mungu na kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa ni nyenzo muhimu sana katika kuchuchumilia na kuambata utakatifu wa maisha!

Ibada kwa Bikira Maria na Huruma ya Mungu ni nyenzo msingi kiroho

24/04/2017 06:30

Ibada kwa Bikira Maria na huruma ya Mungu ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya kiroho: ili kuchuchumilia na kuambata utakatifu wa maisha! Hii ni changamoto ambayo imetolewa kwenye Kituo cha Hija Kiabakari Jimbo Katoliki Musoma wakati wa mkesha wa maadhimisho ya Jumapili ya huruma!