Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Malezi na Majiundo ya Kipadre

Mwongozo wa malezi ya kipadre: mkazo ni: utu, tasaufi na huduma kwa watu wa Mungu!

Mwongozo wa malezi ya kipadre: mkazo ni utu, tasaufi na huduma kwa watu wa Mungu.

Malezi ya Kipadre yazingatie: Utu, tasaufi na huduma makini!

23/04/2018 09:47

Mwongozo wa Malezi ya Kipadre katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo unakazia umuhimu wa kuwafunda majandokasisi kiutu, ili waweze kukomaa, pili ni tasaufi ya maisha na wito wa kipadre unaowataka kujisadaka bila ya kujibakiza na hatimaye, watambue kwamba, wao ni watu wa huduma.

Papa Francisko awataka viongozi na walezi seminarini kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea imepitwa na wakati!

Papa Francisko anawataka viongozi na walezi seminarini kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea kwani imepitwa na wakati.

Viongozi na walezi seminarini acheni tabia ya kutenda kazi kwa mazoea

08/03/2018 15:36

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kutokana na utandawazi na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia kuna utamaduni mpya unaoibuka na hivyo kuacha changamoto kubwa katika malezi na majiundo ya majandokasisi! Hapa kuna haja ya kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea!

Nchi za AMECEA zinapaswa kujitathimini ili kuangalia ikiwa kama malengo ya waasisi yamefikiwa katika maeneo yao!

Nchi za AMECEA zinapaswa kujitathmini ili kuangalia ikiwa kama malengo ya waasisi wa AMECEA yamefikiwa katika nchi zao!

Nchi za AMECEA zatakiwa kujitathmini ikiwa kama malengo yamefikiwa

09/02/2018 09:17

AMECEA ilianzishwa na Mababa wa Kanisa Afrika Mashariki na Kati ili kuimarisha Imani Katoliki, kuwa na mbinu mkakati kwa ajili ya "Kesho ya Kanisa Barani Afrika. Vyombo vya mawasiliano ya jamii, majiundo makini na endelevu kwa wakleri, elimu ya juu, kujitegemea na kulitegemeza Kanisa!

Jimbo Kuu la Mombasa limezindua Mpango Mkakati wa Maendeleo kwa kipindi cha Miaka kumi kuanzia sasa!

Jimbo kuu la Mombasa, Kenya limezindua Mpango Mkakati wa Shughuli za Maendeleo ya Kichungaji katika kipindi cha miaka kumi, mkazo ni majiundo, miundo mbinu na maboresho ya huduma kwa watu wa Mungu.

Jimbo kuu la Mombasa lazindua mpango mkakati wa kichungaji

08/02/2018 08:30

Jimbo kuu la Mombasa, nchini Kenya hivi karibuni limezindua mpango mkakati wa shughuli za kichungaji unaopaswa kutekelezwa katika kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2018 kwa kuwekeza zaidi katika majiundo makini na endelevu ya wakleri, watawa na waamini pamoja na kuboresha miundombinu!

Papa Francisko: Kanisa linakazia majiundo ya kipadre katika maisha na utume wake!

Papa Francisko: Kanisa linakazia malezi na majiundo ya maisha, wito na utume wa Kipadre kama sehemu muhimu sana ya utume wake kwa watu wa Mungu.

Mwongozo wa Malezi ya Kipadre umeboreshwa kwa kusoma alama za nyakati

10/10/2017 06:58

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican walikazia sana umuhimu wa malezi na majiundo ya Kipadre kwa ajili ya maisha na utume wa Kanisa. Kunako mwaka 1970 Mwongozo wa kwanza ukachapishwa na kufanyiwa marekebisho kunako mwaka 1985 na mwongozo mpya kutolewa mwaka 2016.

Mwongozo wa Malezi ya Kipadre ni sehemu ya harakati za Mama Kanisa kusoma alama za nyakati kwa ajili ya majiundo ya Mapadre wake!

Mwongozo wa Malezi ya Kipadre ni sehemu ya harakati za Mama Kanisa kusoma alama za nyakati kwa ajili ya malezi na makuzi ya Mapadre wake.

Kongamano la Kimataifa: Malezi na mang'amuzi katika maisha ya kipadre

07/10/2017 16:43

Mwongozo wa Malezi ya Kipadre uliochapishwa kunako mwaka 2016 unafafanua kwa kina na mapana tasaufi, maisha, wito na utume wa padre mintarafu dhana ya kimisionari inayokaziwa na Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wa Kanisa! Haya ni malezi awali na endelevu!

Papa Francisko: walezi wakuu wa miito: Mungu, Mapadre, Maaskofu na Watu wa Mungu!

Papa Francisko: walezi wakuu wa miito: Mungu, Mapadre, Maaskofu na Watu wa Mungu.

Walezi wakuu wa miito: Mungu, Mapadre, Maaskofu na Familia ya Mungu

07/10/2017 16:27

Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha Mapadre kwamba, mlezi wa kwanza katika maisha na utume wao wa kipadre ni Mwenyezi Mungu anayewafinyanga na kuwaunda kadiri ya mapenzi yake, wao wenyewe; walezi na maaskofu pamoja na familia ya watu wa Mungu!

Papa Francisko anawaomba Mababa wa Sinodi ya Kanisa la Caldea, kuimarisha upatanisho wa kitaifa, iili kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yao!

Papa Francisko anawaomba Mababa wa Sinodi ya Kanisa la Caldea kuimarisha upatanisho wa kitaifa ili kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yao!

Papa Francisko: Imarisheni upatanisho wa kitaifa ili kujenga Iraq

06/10/2017 06:17

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika Mababa wa Sinodi ya Kanisa la Caldea kujizatiti kikamilifu katika mchakato wa upatanisho wa kitaifa nchini Iraq, ili hatimaye, waweze kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yao kama: uhamiaji wa nguvu dhidi ya Wakristo, ujenzi wa vijiji na miito mitakatifu!