Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Makubaliano ya Amani ya St. Sylvester, DRC

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali ya kisiasa na kijamii nchini DRC!

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali tete ya kisiasa na kijamii nchini DRC.

Papa Francisko anaendelea kufuatilia kwa karibu hali tete nchini DRC

14/04/2018 16:31

Baba Mtakatifu Francisko kwa nyakati mbali mbali ameonesha masikitiko makubwa pamoja na kuguswa na hali tete ya wananchi wa DRC wanaoendelea kuteseka kutokana na vita pamoja na mpasuko wa kisiasa na kijamii. Vatican inaiomba Jumuiya ya Kimataifa kusimamia mchakato wa uchaguzi DRC.

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linataka: uhuru, usalama na demokrasia ya kweli!

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linaitaka Serikali iliyoko madarakani kuhakikisha kwamba, watu wanakuwa na uhuru wa kujieleza, wanapatiwa ulinzi na usalama wa maisha na mali zao pamoja na kuwa na demokrasia inayozingatia utawala wa sheria.

Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki DRC: Uhuru, Usalama & Demokrasia

21/02/2018 07:20

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC katika tamko lake kuhusu hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini mwao, linapenda kukazia kwa namna ya pekee kabisa uhuru wa watu kujieleza kama sehemu ya haki zao msingi; ulinzi na usalama wa raia na mali zao pamoja na demokrasia inayoheshimu utawala wa sheria.

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa DRC inashutumiwa kwa kuvunja haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa DRC inashutumiwa kwa kuvunja haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

DRC: Haki msingi za binadamu na utawala wa sheria viko mashakani!

14/02/2018 08:09

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Watu wa Congo imeshindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati yake na vyama vya upinzani nchini humo kuhusu mustakabali wa nchi hiyo na matokea yake haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria vinaendelea kuvunjwa kila kukicha!