Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Majadiliano ya kiekumene

Makanisa hayana budi kushikamana ili kukabiliana na changamoto mamboleo katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Makanisa hayana budi kushikamana ili kukabiliana na changamoto mamboleo katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Mshikamano wa Makanisa katika kukabiliana na changamoto mamboleo

18/08/2017 15:53

Viongozo wa Makanisa wanasema kuna mambo mengi ambayo yanawaunganisha Wakristo ikilinganishwa na mambo ambayo yanawagawa na kutaka kuwasambaratisha! Makanisa hayana budi kuendeleza majadiliano ya kiekumene katika: sala na maisha ya kiroho; ushuhuda wa damu na huduma makini.

Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe ni shuhuda wa utume na upendo kwa jirani hata katika kifo!

Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe ni shuhuda wa utume na upendo kwa jirani hata katika kifo!

Mtakatifu Maximilian Kolbe mfano bora wa utume na upendo kwa jirani

14/08/2017 08:55

Kanisa ni sakramenti ya wokovu ndiyo maana linapenda kujibidisha katika mchakato wa kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano kati ya watu! Changamoto inayopaswa kuvaliwa njuga na vijana wa kizazi kipya ili waweze kuwa ni mashuhuda wa amani duniani!

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anatembelea Russia kuanzia tarehe 20- 24 Agosti 2017 kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na uekumene!

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kuanzia tarehe 20-24 Agosti ili kuimarisha uhusiano wa kidplomasia na Russia pamoja na kuendeleza majadiliano ya kiekumene.

Kardinali Parolin anatembelea Russia kuanzia tarehe 20-24 Agosti 2017

10/08/2017 11:19

Ziara ya kikazi ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican nchini Russia kuanzia tarehe 20 - 24 Agosti 2017 inapania kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Russia sanjari na kuendeleza majadiliano ya kiekumene katika: sala na maisha ya kiroho; katika damu na huduma!

Watakatifu ni wasindikizaji wema na wazuri; wao ni wanandani wa hija ya maisha ya kiekumene!

Watakatifu ni wasindikizaji wema na wazuri na ni wanandani wa hija maisha ya kiekumene duniani.

Watakatifu ni wasindikizaji wa mchakato wa majadiliano ya kiekumene!

28/07/2017 15:16

Mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayosimikwa katika sala, maisha ya kiroho ni muhimu sana katika kukuza na kudumisha utakatifu wa watu wa Mungu wenye kiu ya kuona Kanisa limeungana chini ya Kristo Yesu, Mchungaji mkuu. Hii ni dhana inayopaswa kukuzwa na kuendelezwa na wote!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anawapongeza viongozi wa Makanisa walioanzisha mchakato wa uekumene miaka 50 iliyopita!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anawapongeza viongozi wa Makanisa walioanzisha mchakato wa majadiliano ya kiekumene miaka 50 iliyopita.

Miaka 50 ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene ndani ya Kanisa!

26/07/2017 14:39

Mwenyeheri Paulo VI anasema, mwanga wa upendo wa Wakristo na udugu walionao wao kwa wao, unawasaidia kutambua umuhimu wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake. Patriaki Athenagora anahimiza viongozi kujitahidi kuunganisha kile ambacho kimetenganishwa kwa kukazia imani na uongozi.

Misimamo mikali ya kidini na kiimani inasababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao sehemu mbali mbali za dunia.

Misimamo mikali ya kidini na kiimani inasababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao.

Majadiliano ya kidini na kiekumene yasaidie kuzima kiu ya amani!

24/07/2017 13:45

Misimami mikali ya kidini na kiimani inaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao, umefika wakati kwa familia ya Mungu Barani Afrika kushikamana katika kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi!

Amani ya kweli inajengwa katika majadiliano yanayofumbatwa katika ukweli na uwazi; ustawi na maendeleo ya wengi.

Amani ya kweli inajengwa kayika majadiliano yanayofumbatwa katika ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, hali inayoonesha utashi wa kisiasa.

WCC: Amani ya kweli inapatikana kwa njia ya majadiliano!

21/07/2017 07:00

Vita na machafuko ni madonda ambayo yanachukua muda mrefu kuweza kutibiwa na kuponywa! Amani ya kweli inasimikwa katika majadiliano yanayofumbatwa kwenye ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi  kwa kuonesha utashi wa kisiasa! Vinginevyo ni bure kabisa!

Kardinali Tauran inaitaka familia ya Mungu Barani Afrika kujikita katika machakato wa majadialiano ya kidini, kitamaduni na kiekumene!

Kardinali Tauran anaitaka familia ya Mungu Barani Afrika kujikita katika mchakato wa majadiliani ya kidini, kiekumene na kitamaduni kwa ajili ya ustawi, maendeleo na ustawi wa wengi.

Familia ya Mungu Barani Afrika: Dumisheni majadiliano ya kidini!

10/07/2017 09:29

Kardinali Jean Louis Tauran anaialika familia ya Mungu Barani Afrika kujika zaidi na zaidi katika mchakato wa majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni katika ukweli na uwazi, ili kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo, udugu na mshikamano kati ya watu wa Mataifa!