Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mafundisho Jamii Kanisa

Ukusanyaji wa kodi ya uchaguzi mkuu 2020 uzingatie misingi ya ukweli, uwazi na uwajibikaji kwa wote!

Ukusanyaji wa kodi ya uchaguzi mkuu nchini Burundi kwa mwaka 2020 uzingatie misingi ya ukweli, uwazi na uwajibikaji wa wote.

Maaskofu Burundi: Ukweli na uwazi katika fedha ya uchaguzi mkuu

16/04/2018 11:28

Baraza la maaskofu Katoliki Burundi linasema, mchakato wa uchaguzi mkuu ni zoezi muhimu sana katika kukuza na kudumisha uhuru wa wananchi na demokrasia, lakini linapaswa kuendeshwa katika misingi ya ukweli na uwazi mintarafu kodi ya uchaguzi mkuu kwa mwaka 2020.

 

Tarehe 12-13 Machi Katika Chuo Kikuu cha Kipapa utafanyika mkutano kuhusu haki ya elimu na mafundisho

Tarehe 12-13 Machi Katika Chuo Kikuu cha Kipapa utafanyika mkutano kuhusu haki ya elimu na mafundisho. Mkutano umetayarishwa na Kitengo cha Sheria ya Kanisa

Tarehe 12-13.3.2018:Mkutano juu ya haki msingi ya elimu na mafundisho!

09/03/2018 15:50

Kuanzia tarehe 12-13 Machi 2018 katika Chuo Kikuu cha Kipapa, Santa Croce Roma,utafanyika mkutano wa Kitengo cha Sheria za Kanisa kuhusu haki msingi ya elimu na mafundisho.Katika mkutano huo ni mada nyingi zitaguswa ambazo zimechaguliwa na  kitengo hicho cha Sheria za Kanisa

 

Tume ya Kikatoliki Kimataifa kwa ajili ya wahamiaji, ICMC imejizatiti katika miaka 65 kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji duniani.

Tume ya Kikatoliki Kimataifa kwa ajili ya Wahamiaji kwa Miaka 65 imejizatiti kuwahudumia na kuboresha maisha ya wakimbizi na wahamiaji sehemu mbali mbali za dunia.

ICMC: Miaka 65 ya huduma makini kwa wakimbizi na wahamiaji duniani!

08/03/2018 15:14

Baba Mtakatifu Francisko anaishukuru na kuipongeza Tume ya Kikatoliki Kimataifa kwa ajili ya Wahamiaji, ICMC, ambayo kwa muda wa miaka 65 imekuwa bega kwa bega katika mchakato wa kupangusa machozi ya wakimbizi na wahamiaji pamoja na kujizatiti kuboresha hali ya maisha na utu wao!

Papa Francisko asema kipaumbele cha Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji eneo la Amazonia!

Papa Francisko asema, kipaumbele cha kwanza kwa Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji wa kina kwenye eneo la Amazonia.

Papa Francisko: Kipaumbele cha Kanisa Perù: Uinjilishaji wa Amazonia

31/01/2018 07:02

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Maaskofu kuwa karibu zaidi na wakleri wao; kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya Kiinjili ili kupambana na saratani ya rushwa, ufisadi na kumong'onyoka kwa haki msingi, utu na heshima ya binadamu. Maaskofu wathamini majadiliano katika ukweli na uwazi.

Caritas Africa inapenda kujielekeza zaidi katika huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu kama asili na utambulisho wa Kanisa

Caritas Africa inapenda kujielekeza katika mchakato wa huduma makini na endelevu kama asili na utambulisho wa Kanisa kati ya Watu wa Mataifa.

Caritas Africa mintarafu asili ya Kanisa na huduma endelevu!

27/12/2017 07:32

Askofu mkuu Martin Musonde Kivuva wa Jimbo kuu la Mombasa katika mahojiano na Radio Vatican ambayo kwa sasa inatambulikana kama "Vatican News" anachambua asili ya Kanisa kama chombo muhimu sana cha huduma mintarafu mchakato wa maendeleo endelevu ya binadamu: kiroho na kimwili!

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kushirikiana kwa dhati ili kukomesha nyanyaso za utu na heshima ya watoto kwenye mitandao ya kijamii!

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kushirikiana kwa dhati ili kupambana na nyanyaso, dhuluma na udhalilishaji wa utu na heshima ya watoto wadogo kwenye mitandao ya kijamii.

Papa Francisko: Mbinu mkakati wa kulinda utu wa watoto mitandaoni!

06/10/2017 15:48

Baba Mtakatifu Francisko anasema, dhamana na wajibu wa kulinda utu na heshima ya watoto mitandaoni ni ya wote bila ubaguzi! Lakini, ili kutekeleza dhamana hii, kuna haja ya vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi na wadau mbali mbali kushirishana: rasilimali watu, ujuzi na mang'amuzi yao!

Vatican inayaangalia matatizo, changamoto na fursa za Jumuiya ya Kimataifa kwa mwanga wa Injili, Mafundisho ya Kanisa na Utume wa Kanisa kwa Mataifa.

Vatican inayaangalia matatizo, changamoto na fursa mbali mbali za kimataifa katika mwanga wa Injili, Mafundisho Jamii ya Kanisa; dhamana, maisha na utume wa Kanisa kwa watu wa Mataifa!

Mchango wa Vatican katika masuala changamani ya Jumuiya ya Kimataifa!

27/09/2017 11:08

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher anasema kwamba, Vatican inayaangalia matatizo, changamoto na fursa mbali mbali zinazojitokeza kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwa mwanga wa Injili, Mafundisho Jamii ya Kanisa sanjari na utume na dhamana ya Kanisa Katoliki katika familia ya binadamu duniani!

Wabunge Wakatoliki wajitahidi kuyafahamu Mafundisho Jamii ya Kanisa, ili wajenge madaraja ya majadiliano!

Wabunge Wakatoliki wajitahidi kuyafahamu Mafundisho Jamii ya Kanisa ili kusaidia kujenga madaraja ya kuwakutanisha watu.

Papa Francisko: Wabunge Wakatoliki jengeni madaraja ya majadiliano

28/08/2017 14:00

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Wabunge Wakatoliki kufahamu vyema Mafundisho Jamii ya Kanisa ili waweze kujenga madaraja ya kuwakutanisha watu katika mchakato wa maamuzi mbali mbali bungeni; kwa kusimamia utu na heshima ya binadamu sanjari na kupinga utamaduni wa kifo!