Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Mafumbo ya Kanisa

Papa Francisko: mahali ya shukrani, sadaka na umoja wa Kanisa

Papa Francisko asema, maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu ni mahali pa kumtolea Mungu shukrani ka kutambua kwamba, maisha ni zawadi ili hatimaye, kujenga na kudumisha umoja wa Kanisa.

Papa Francisko: Kipindi cha Mageuzo ni kiini cha Ibada ya Misa!

07/03/2018 15:20

Baba Mtakatifu Francisko anasema Sala ya Ekaristi Takatifu ni sehemu muhimu sana ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu! Ni kiini na utangulizi unaowawezesha waamini kushiriki kikamilifu Fumbo la Ekaristi Takatifu kama Kristo Yesu alivyofanya siku ile ya Alhamisi Kuu kabla ya mateso yake!

Karamu ya harusi ni kielelezo cha Fumbo la Ekaristi Takatifu, chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa.

Karamu ya harusi ni kielelezo cha Fumbo la Ekaristi Takatifu, chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa, humo waamini wanalishwa kwa Neno la Mkate wa uzima wa milele.

Itikieni wito wa Kimungu kwa kuwa na vazi la harusi!

14/10/2017 09:26

Kristo Yesu, katika Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili XXVIII anaelezea Ufallme wa Mungu kama harusi ya maisha ya uzima wa milele, kielelezo cha matumaini na furaha ya watu wake. Harusi ni kielelezo pia cha Fumbo la Ekaristi Takatifu ambamo waamini wanalishwa kwa Neno na Mkate wa uzima!

Papa Francisko katika Barua yake Binafsi "Magnum Principium" anakazia umuhimu wa tafasiri sahihi ya vitabu vya liturujia ya Kanisa.

Papa Francisko katika Barua yake binafsi "Motu Proprio: Magnum Principium" anakazia umuhimu wa kutafasiri vitabu vya liturujia kwa watu wa Mungu.

Barua Binafsi kuhusu: Mwendelezo wa Mageuzi ya Maisha ya Liturujia

13/09/2017 10:19

Baba Mtakatifu Francisko ameandika Barua Binafsi "Magnum Principium" kuhusu mwendelezo wa mchakato wa mageuzi katika maisha ya Liturujia ya Kanisa yaliyoanzishwa na Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican kwa kubadilisha Sheria za Kanisa namba 838 kuhusu tafsiri ya lugha ya vitabu vya liturujia

Kuna umuhimu wa kuzingatia Mwongozo wa Malezi ya Kipadre.

Kuna umuhimu wa kuzingatia Mwongozo wa Malezi ya Kipadre.

Malezi na majiundo endelevu ya Kipadre ni muhimu sana!

13/07/2017 14:51

Kardinali Beniamino Stella anaendelea kukazia umuhimu wa kuzingatia Mwongozo wa Malezi ya Kipadre uliochapishwa hivi karibuni ili kuliwezesha Kanisa kupata watendaji kazi wema, watakatifu, waadilifu, wachamungu na wachapakazi; watu ambao wanaweza kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa Kanisa!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa mwezi Juni!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay, Mwezi Juni 2017 linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu.

Mwezi wa kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa

19/06/2017 14:27

Kanisa Katoliki nchini Uruguay limeutenga mwezi Juni, 2017 kuwa ni mwezi wa kuombea miito mbali mbali ndani ya Kanisa: wito wa Upadre, ili Kanisa liweze kupata Mapadre: wema, watakatifu na wachamungu; watawa watakaojisadaka kwa ajili ya huduma makini na familia kama Kanisa dogo ya nyumbani.

Roho Mtakatifu anawawezesha waamini kuwa ni vyombo na mashuhuda wa matumaini na ujasiri!

Roho Mtakatifu anawawezesha waamini kuwa ni vyombo na mashuhuda wa ujasiri na matumaini.

Roho Mtakatifu awatie nguvu na ujasiri wa kuwa mashuhuda amini!

01/06/2017 09:30

Roho Mtakatifu ni mhimili mkuu katika mchakato mzima wa uinjilishaji mpya unaofumbatwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Roho Mtakatifu anayo dhamana ya kuwafundisha, kuwakumbusha na kuwaelekeza waamini kwenye ukweli wote, ili hatimaye, waweze kuwa kweli ni mashuhuda wake.

Papa Francisko anawaalika wakleri na watawa kuiga mfumo na mtindo wa maisha ya Yesu katika wito na majukumu yao ya kila siku.

Papa Francisko anawaalika wakleri na watawa kuiga mfano bora wa maisha ya Kristo Yesu katika utekelezaji wa dhamana na utume wao ndani ya Kanisa.

Vigezo msingi katika utekelezaji wa maisha ya kipadre na kitawa!

28/05/2017 14:19

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kuhakikisha kwamba, wanazingatia mambo msingi katika maisha na utume wao, kwa kufanya mambo kwa nidhamu na utulivu wa hali ya juu; kwa kukutana na kuzungumza na watu; kwa ibada na maisha ya sala na tafakari kama alivyofanya Yesu.

Mihimili ya Uinjilishaji wa kina inapaswa kuwa ni mashuhuda wa Injili ya huduma, upendo, haki na amani!

Mihimili ya Uinjilishaji wa kina inapaswa kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya huduma, upendo, haki, amani na mshikamano wa dhati.

Dhamana na wajibu wa mihimili ya uinjilishaji ndani ya Kanisa!

23/05/2017 15:55

Kardinali Fernando Filoni anaitaka mihimili ya uinjilishaji kuwa kweli ni vyombo na mashuhuda wa uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili! Wawe ni watu wanaojisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya ujenzi, ustawi na maendeleo ya Kanisa mahalia, mfano bora wa kuigwa!