Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Madonda Matakatifu ya Yesu

Kristo Mfufuka alijitahidi kuwafunulia wafuasi wake Fumbo la Ufufko na kuwaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu!

Kristo Yesu Mfufuka alijitahidi kuwafunulia Mitume wake Fumbo la Ufufuko kiasi cha kuwaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu.

Kristo Mfufuka ameondoa hofu na mashaka, sasa ni ushuhuda tu!

12/04/2018 15:50

Kristo Mfufuka alijitahidi kuwafafanulia wafuasi wake kuhusu Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wake, kwa kuwashirikisha wafuasi wake uhalisia wa maisha yake kama Mfufuka, akawaruhusu kugusa Madonda yake Matakatifu ili kuonja uwepo wake endelevu kama ilivyo hata katika kuumega mkate.

Papa Francisko urithi na amana kutoka kwa Padre Pio: Sala, Unyenyekevu na Hekima ya maisha!

Papa Francisko urithi na amana kutoka kwa Padre Pio ni: Maisha ya sala, unyenyekevu na hekima katika maisha inayofumbata Fumbo la Msalaba.

Papa Francisko urithi wa Padre Pio: Sala, unyenyekevu na hekima!

19/03/2018 10:09

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kanisa linapofanya kumbu kumbu ya miaka hamsini tangu alipofariki dunia Padre Pio wa Pietrelcina na miaka mia moja tangu alipopata Madonda Matakatifu, urithi na amana yake kwa Kanisa ni: maisha ya sala, unyenyekevu na hekima katika maisha ya kawaida!

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni kielelezo cha: huruma, upendo na maisha mapya!

19/03/2018 09:54

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa mateso na kifo cha Mwana mpendwa wa Mungu, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa binadamu wa nyakati zote! Kwa njia ya Madonda yake Matakatifu watu wameponywa!

Papa Francisko awataka viongozi na walezi seminarini kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea imepitwa na wakati!

Papa Francisko anawataka viongozi na walezi seminarini kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea kwani imepitwa na wakati.

Viongozi na walezi seminarini acheni tabia ya kutenda kazi kwa mazoea

08/03/2018 15:36

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kutokana na utandawazi na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia kuna utamaduni mpya unaoibuka na hivyo kuacha changamoto kubwa katika malezi na majiundo ya majandokasisi! Hapa kuna haja ya kuachana na tabia ya kutenda kazi kwa mazoea!

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kudumisha maisha ya kijumuiya, Ibada kwa Madonda Matakatifu na Injili ya huduma kwa maskini.

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kudumisha maisha ya kijumuiya, ibada kwa Madonda Matakatifu ya Kristo Yesu na Injili ya upendo kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Shirika la Madonda Matakatifu kuzeni: Udugu, ibada na huduma!

12/02/2018 09:17

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Wanashirika la Madonda Matakatifu kuhakikisha kwamba, linakuza na kudumisha: udugu katika maisha ya kijumuiya, sala, uhuru na ukweli; kwa kukuza na kuendeleza Ibada kwa Madonda Matakatifu ya Kristo Yesu, Ibada inayomwilishwa katika Injili ya upendo!

Papa Francisko kutembelea S. Giovanni Rotondo, tarehe 17 Machi 2018.

Papa Francisko kutembelea S. Giovanni Rotondo tarehe 17 Machi 2018.

Papa Francisko kutembelea S. Giovanni Rotondo 17 Machi 2018

19/12/2017 13:40

Kama sehemu ya kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 50 tangu Padre Pio wa Pietrelcina alipopata Madonda Matakatifu na hatimaye, kufariki dunia, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kufanya hija ya kichungaji katika Madhabahu ya San Giovanni Rotondo, huko Benevendto, tarehe 17 Machi 2018.