Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Madhulumu ya kidini

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso na kifo cha Kristo! Msalabani, ili kuonesha toba na wongofu wa ndani!

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso, kifo na ufufuko ili kuonesha toba na wongofu wa ndani, tayari kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha: haki, amani na maridhiano kati ya watu.

Wakristo fungeni na kusali katika roho na kweli!

24/02/2018 09:25

Kwaresima ni kipindi cha kusali, kufunga, kutafakari na kutenda matendo ya huruma kwa maskini na wahitaji zaidi. Hiki ni kipindi muafaka kwa ajili ya maandalizi ya adhimisho la Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka kwa wafu. Hata leo hii kuna bado watu wanateseka!

Uhuru wa kuabudu ni nguzo msingi ya haki zote za binadamu, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kwa sasa!

Uhuru wa kuabudu ni nguzo msingi ya haki zote msingi za binadamu, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa katika ulimwengu mamboleo!

Uhuru wa kuabudu ni changamoto kubwa kwa Jumuiya ya Kimataifa!

03/02/2018 08:50

Baba Mtakatifu Francisko anaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa macho dhidi ya "Haki Mpya" zinazoibuliwa na baadhi ya nchi kiasi cha kupingana na mila, desturi, utu na heshima ya binadamu! Uhuru wa kuabudu ni changamoto kubwa kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa nyakati hizi!

Kanisa litakumbuna na dhoruba kali katika historia, maisha na utume wake, lakini daima Kristo Yesu ataliokoa  kwa wakati muafaka!

Kanisa litambuna na dhoruba pamoja na mawimbi makali katika historia, maisha na utume wake, lakini Kristo Yesu, ataliokoa kwa wakati muafaka na kulifikisha bandari salama! Jambo la msingi ni imani kwa Kristo Mwana wa Mungu aliye hai!

Kanisa linatumwa na Kristo kuwa ni shuhuda wa Injili ya matumaini!

12/08/2017 09:45

Jumuiya ya Wakristo wa mwanzo, walimwona Petro mtume kuwa ni kiongozi aliyetumwa na Kristo Yesu kuliongoza Kanisa katika historia ya mwanadamu inayokumbana na mawimbi mazito, dhuluma na nyanyaso, lakini jambo la msingi ni kuendelea kushikamana na Kristo katika sala na ushuhuda wa imani.

Papa Francisko anasema, matumaini ya Kikristo ni nguvu ya mashuhuda wa imani!

Papa Francisko anasema, matumaini ya Kikristo ni nguvu ya mashuhuda wa imani.

Papa Francisko: Matumaini ya Kikristo ni nguvu ya mashuhuda wa imani!

28/06/2017 15:25

Baba Mtakatifu Francisko anasema, utangazaji, ushuhuda na ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani una changamoto na magumu yake kutokana na kukithiri kwa dhambi hali inayoshuhudiwa na ukosefu wa haki msingi za binadamu, ubinafsi wa hali ya juu na watu kupenda mno malimwengu!

Papa Francisko anawaalika Wakristo kuwa mashuhuda amini wa Kristo na Kanisa lake na kamwe wasiogope!

Papa Francisko anawaalika Wakristo kuwa mashuhuda amini wa Kristo na Kanisa lake na kamwe wasiogope!

Papa Francisko: Iweni mashuhuda waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake!

26/06/2017 09:11

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika Wakristo kuwa ni mashuhuda amini na waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake, wasiogope: mauaji, mateso, dhuluma na nyanyaso kwani hii ni sehemu yua vinasaba vya maisha na utume wa Kikristo ulimwenguni, watambue kwamba, wanathaminiwa na Kristo Yesu!

Kanisa katika mahangaiko na wasi wasi zinazomwandama binadamu anajibu kwa kujikita katika Injili ya matumaini kwa Kristo Yesu.

Kanisa katika mahangaiko na wasi wasi zinazomkumba mwanadamu katika ulimwengu mamboleo anajibu kwa kutangaza na kushuhudia Injili ya matumaini kwa Kristo Yesu!

Ukimya wa Kanisa nyakati za madhulumu!

31/10/2016 16:58

Tafakari ya kina iliyotolewa hivi karibuni mintarafu ukimya wa Kanisa nyakati za majaribu na madhulumu ni cheche zinazopania kufungua akili na nyoyo za watu ili kuangalia kwa imani na matumaini, hofu inayoendelea kuugubika ulimwengu mamboleo kutokana na ugaidi, vita, nyanyaso na majanga asilia.

Vitendo vya kigaidi, misimamo mikali ya kidini na ubaguzi ni kati ya mambo yanayoendelea kusababisha mauaji makubwa kwa wakristo!

Vitendo vya kigaidi, misimamo mikali ya kidini na kiimani; ubaguzi, nyanyaso na dhuluma ni kati ya mambo yanayoendelea kusababisha mauaji makubwa ya Wakristo sehemu mbali mbali za dunia.

Kanisa letu ni Kanisa la mashuhuda!

16/03/2016 08:36

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican anasema pengine leo hii kuna mashuhuda wengi wa imani kuliko hata ilivyokuwa wakati wa Kanisa la mwanzo kutokana na chuki za kidini na misimamo mikali ya kiimani!

Hija ya kitume ya Papa Francisko Barani Afrika itaendelea kama ilivyopangwa!

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko Barani Afrika itaendelea kama ilivyopngwa!

Hija ya Baba Mtakatifu Francisko Barani Afrika inaendelea kama ilivyopangwa!

18/11/2015 12:08

Hija ya Baba Mtakatifu Francisko Barani Afrika pamoja na maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu yataendelea kama yalivyopangwa na wala hakuna sababu za msingi za kuhailishwa wala kufutwa kwa matukio haya, jambo la msingi ni ulinzi na usalama.