Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu 2018

Papa Francisko amebaianisha mambo makuu yanayopaswa kukaziwa katika malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya Jimbo kuu la Roma.

Papa Francisko amebainisha mambo msingi yanayopaswa kukaziwa katika malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya Jimbo kuu la Roma.

Papa Francisko abainisha mambo msingi katika malezi ya vijana!

20/06/2017 11:33

Baba Mtakatifu Francisko, amefungua rasmi kongamano la Jimbo kuu la Roma kwa kukazia: umuhimu wa familia jijini Roma; umuhimu wa kujenga na kudumisha mshikamano; kuandamana na vijana; elimu endelevu, jinsi ya kukabiliana na changamoto za vijana na umuhimu wa maisha ya kiroho!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa mwezi Juni!

Kanisa Katoliki nchini Uruguay, Mwezi Juni 2017 linasali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu.

Mwezi wa kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa

19/06/2017 14:27

Kanisa Katoliki nchini Uruguay limeutenga mwezi Juni, 2017 kuwa ni mwezi wa kuombea miito mbali mbali ndani ya Kanisa: wito wa Upadre, ili Kanisa liweze kupata Mapadre: wema, watakatifu na wachamungu; watawa watakaojisadaka kwa ajili ya huduma makini na familia kama Kanisa dogo ya nyumbani.

Tovuti kwa maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ipo hewani

Tovuti kwa maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ipo hewani

Tovuti ya Sinodi ya Maaskofu kwa Vijana

15/06/2017 14:52

Sekretariat kuu ya Sinodi ya Maaskofu, imefungua tovuti kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi ya Vijana inayotarajiwa kufanyika mjini Vatican mnamo Oktoba 2018, fomu za maswali dodosa zapatikana kwa lugha kadhaa, tembelea http//youth.synod2018.va

Baraza la Maaskofu Katoliki Austria lapania Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana

Baraza la Maaskofu Katoliki Austria lapania Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana katika kuwakuza kiimani na kung'amua miito yao

Baraza la Maaskofu Katoliki Austria jicho kodo Sinodi ya vijana

08/06/2017 13:37

Baraza la Maaskofu katoliki nchini Austria linapokutana katika mkutano mkuu kuanzia tarehe 12 - 14 Juni 2017, linanuia kujadili zaidi maandalizi juu ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana inayotarajiwa kufanyika mjini Vatican mwezi Oktoba 2018.

Papa Francisko anasema, hata leo hii kuna vijana wengi wanaovutiwa kujisadaka kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo!

Papa Francisko anasema, hata leo hii kuna vijana wa kizazi kipya wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo katika medani mbali mbali za maisha ya mwanadamu!

Achana na wito! Kutoka ufundi Seremala hadi kufundisha Chuo Kikuu!

08/06/2017 09:41

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa Siku ya Kimissionari Duniani kwa Mwaka 2017 anasema, bado Injili inaendelea kuwa na mvuto hata kwa vijana wa kizazi kipya, wanaotaka kujisadaka na kujitosa katika maisha, wito na utume wa Kipadre kama ilivyotokea kwa Padre Josephat Muhoza, SDS.

Utume ni kiini cha imani ya Kikristo ndiyo kauli mbiu inayoongoza ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani.

Utume ni kiini cha imani ya Kikikristo ndiyo kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani kwa mwaka 2017.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani 2017

06/06/2017 14:33

Utume wa Kanisa unaelekezwa kwa watu wote wenye mapenzi mema na unasimikwa katika msingi wa Injili inayoleta mabadiliko; inayoshirikisha furaha kwani ni chemchemi ya maisha mapya yanayobubujika kutoka kwa Kristo Mfufuka aliyewapelekea Roho Mtakatifu, hivyo Yesu ni njia, ukweli na uzima!

Kardinali Bagnasco anasema, vijana wana imani na matumaini ya Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kardinali Angelo Bagnasco anasema, vijana wana imani na matumaini kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Vijana wana imani na matumaini kwa Kanisa la Kristo!

28/05/2017 14:00

Kardinali Angelo Bagnasco, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la genova, Italia anasema kwamba, vijana wengi wa kizazi kipya Jimboni mwake wana imani na matumaini kwa Khalifa wa Mtakatfu Petro na Kanisa la Kristo na kwamba, wanataka kujenga mshikamano wa dhati katika maisha na utume wao.

Papa Francisko anawaalika vijana kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika maisha yao ili awagange na kuwaponya katika mahangaiko yao.

Papa Francisko anawaalika vijana wa kizazi kipya kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao ili aweze kuwaganga na kuwaponya katika shida na mahangaiko yao.

Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana wa kizazi kipya!

28/05/2017 13:44

Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa kizazi kipya kujenga na kudumishaz utamaduni wa sala, tafakari na matendo ya huruma kwa jirani zao! Ikiwa kama kweli wanataka kuwa ni wamissionari wanapaswa kuwapenda, kuwathamini na kujisadaka kwa ajili ya vijana wenzao wenye shida na mateso!