Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Laudato Si

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Estonia

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Estonia.

Waziri Mkuu wa Estonia akutana na Papa Francisko mjini Vatican

10/02/2018 17:08

Vatican na Estonia inaridhishwa na kiwango cha mahusiano wa kidiplomasia kilichofikiwa kati ya nchi hizi mbili bila kusahau mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wengi wa Estonia. Haya ni kati ya mambo makuu yaliyozungumzwa kati ya Papa na Waziri mkuu wa Estonia

Papa Francisko analitaka Shirika la Posta Italia kuboresha sera, mikakati na miundo mbinu daima likilenga kutoa huduma makini kwa wananchi wa Italia.

Papa Francisko analitaka Shirika la Posta Italia kuboresha sera, mikakati na miundo mbinu daima likiendelea kua aminifu kwa lengo msingi ambalo ni huduma makini kwa wananchi wa Italia.

Boresheni miundo mbinu na teknolojia daima mkizingatia huduma makini

10/02/2018 16:40

Baba Mtakatifu Francisko anawataka viongozi pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Posta Italia kuhakikisha kwamba, wanajikita katika mchakato wa maboresho ya sera, mikakati, miundo mbinu na teknolojia lakini dama huduma makini kwa wananchi ikipewa kipaumbele cha kwanza katika sera zao!

Nchi za AMECEA zinapaswa kujitathimini ili kuangalia ikiwa kama malengo ya waasisi yamefikiwa katika maeneo yao!

Nchi za AMECEA zinapaswa kujitathmini ili kuangalia ikiwa kama malengo ya waasisi wa AMECEA yamefikiwa katika nchi zao!

Nchi za AMECEA zatakiwa kujitathmini ikiwa kama malengo yamefikiwa

09/02/2018 09:17

AMECEA ilianzishwa na Mababa wa Kanisa Afrika Mashariki na Kati ili kuimarisha Imani Katoliki, kuwa na mbinu mkakati kwa ajili ya "Kesho ya Kanisa Barani Afrika. Vyombo vya mawasiliano ya jamii, majiundo makini na endelevu kwa wakleri, elimu ya juu, kujitegemea na kulitegemeza Kanisa!

Papa Francisko anasema uchafuzi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni dalili za kupooza kwa upendo!

Papa Francisko anasema, uchafuzi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni dalili za kupoa kwa upendo duniani.

Papa Francisko: Uharibifu wa mazingira ni alama ya kupoa kwa upendo

08/02/2018 07:37

Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake wa Kwaresima kwa Mwaka 2018 anasema, hata mazingira yanashuhudia kupoa kwa upendo kwa kazi ya uumbaji kunakosababishwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira, utupaji wa taka ngumu baharini pamoja na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi.

Hali ya usimamizi mbaya wa fedha na madeni umegeuka kuwa mkubwa kwa ngazi  ya nchi ya Italia  na kwa ulimwengu  mzima

Hali ya usimamizi mbaya wa fedha na madeni umegeuka kuwa mkubwa kwa ngazi ya nchi ya Italia na kwa ulimwengu mzima.

Ni lazima kutazama kwa upya halisi ya umaskini na madeni duniani!

31/01/2018 16:00

Madeni duniani ni kutokana na matumizi mabaya ya fedha yanayosababisha hali ya ukosefu wa haki sawa,umaskini na ugumu wa hali nyingi za wahamiaji.Hayo ni maelezo ya Askofu Mkuu Valentinetti wa Pescara-Penne Italia,  wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano,tarehe 27 Januari

 

 

Papa Francisko asema kipaumbele cha Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji eneo la Amazonia!

Papa Francisko asema, kipaumbele cha kwanza kwa Kanisa nchini Perù ni utamadunisho na uinjilishaji wa kina kwenye eneo la Amazonia.

Papa Francisko: Kipaumbele cha Kanisa Perù: Uinjilishaji wa Amazonia

31/01/2018 07:02

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Maaskofu kuwa karibu zaidi na wakleri wao; kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya Kiinjili ili kupambana na saratani ya rushwa, ufisadi na kumong'onyoka kwa haki msingi, utu na heshima ya binadamu. Maaskofu wathamini majadiliano katika ukweli na uwazi.

Papa Francisko asema, ukoloni mamboleo unaofumbatwa katika nguvu ya kiuchumi unatishia usalama, maisha, ustawi na maendeleo ya Amazonia.

Papa Francisko asema, ukoloni mamboleo unaofumbatwa katika nguvu ya kiuchumi unatishia ustawi, maisha na maendeleo ya Amazonia.

Papa: Ukoloni mamboleo unatishia usalama, maisha na ustawi wa Amazonia

19/01/2018 17:00

Baba Mtakatifu Francisko anasikitika kusema kwamba, ukoloni mamboleo unaojikita katika nguvu ya kiuchumi: kwa uchimbaji wa mafuta na gesi asilia; kilimo cha mashamba makubwa ili kukidhi mahitaji ya mali ghafi ya viwanda; ni mambo yanayotishia usalama, maisha, ustawi na maendeleo ya Amazonia.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Perù ni chemchemi ya furaha na matumaini!

Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Perù ni chemchemi ya furaha na matumaini!

Papa Francisko nchini Perù: chemchemi ya furaha na matumaini

04/01/2018 08:20

Kardinali Juan Luis Ciprian Thorne anasema, Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Perù ni chemchemi ya furaha na matumaini; ni changamoto na mwaliko wa kujenga na kudumisha umoja na mshikamano unaofumbatwa katika tunu msingi za maisha ya kiroho na kiutu kwa ajili ya mafao ya wengi!