Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kauli mbiu:Vijana, imani na mang'amuzi ya miito

Mama Kanisa kwa Mwaka 2018-2019 anakazia: Utume wa Vijana na Maisha ya Ndoa na Familia.

Mama Kanisa kwa Mwaka 2018-2019 anakazia utume wa vijana na maisha ya ndoa na familia.

Vipaumbele vya Kanisa kwa Mwaka 2018-2019: Vijana na familia

21/07/2018 08:41

Mama Kanisa kanisa katika mwaka 2018-2019 anapenda kujielekeza zaidi katika utume kwa vijana, ili kujenga sanaa na utamaduni wa kuwasikiliza, kuwasindikiza na kuwaongoza vijana kufanya maamuzi mazito katika maisha. Pili ni utume wa maisha ya ndoa na familia, ili kutangaza Injili ya familia. 

Papa Francisko analihamasisha Kanisa kujenga utamaduni wa kuwasikiliza, kuwajali na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Papa Francisko analihamasisha Kanisa kujenga utamaduni wa kuwasikiliza, kuwathamini, kuwajali na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Baba Mtakatifu Francisko kukutana na vijana wa Italia, Agosti, 2018

12/05/2018 07:53

Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi cha miaka miwili, amewahamasisha viongozi mbali mbali wa Kanisa kujenga na kudumisha utamaduni wa kuwasikiliza, kuwathamini pamoja na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao ya kiroho, ili waweze kufanya maamuzi magumu na yenye busara.

Maandalizi ya Sinodi ya Vijana yanaendelea kushika kasi hata Barani Afrika.

Maandalizi ya Sinodi ya vijana yanaendelea kushika kasi hata Barani Afrika. Ni wakati kwa viongozi wa Kanisa kujenga utamaduni na sanaa ya kuwasikiliza vijana wa kizazi kipya!

Maandalizi ya Sinodi ya Vijana yanazidi kupamba moto Barani Afrika

30/04/2018 08:15

Maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana itakayoadhimishwa mwezi Oktoba 2018 mjini Vatican yanaendelea kupamba moto sehemu mbli mbali za Bara la Afrika kama sehemu ya ujenzi wa utamaduni na sanaa ya kuwasikiliza na kuwatahamini vijana katika utume wa Kanisa!

Jumapili ya Kristo Yesu Mchungaji Mwema ni Siku ya 55 ya Kuombea Miito Duniani kwa Mwaka 2018.

Jumapili ya Kristo Yesu Mchungaji Mwema ni Siku ya 55 ya Kuombea Miito Duniani kwa Mwaka 2018.

Siku ya Kuombea Miito Duniani: Mashemasi 16 kupewa Daraja Takatifu

20/04/2018 08:44

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jumapili ya Kristo Yesu Mchungaji mwema sanjari na maadhimisho ya Siku ya 55 ya Kuombea Miito Duniani kwa Mwaka 2018 anatarajiwa kutoa Daraja Takatifu ya Upadre kwa Mashemasi 16 kati yao 11 ni wale wanaotoka Jimbo kuu la Roma. Ombeeni miito!

Papa Francisko anawaalika waamini kutafakari kuhusu: Kusikiliza kwa makini; Kung'amua na hatimaye, kuishi upya wa maisha unaoletwa na Kristo.

Papa Francisko anawaalika waamini katika ujumbe wake wa Siku ya 55 ya Kuombea Miito Duniani kwa Mwaka 2018: Kusikiliza kwa makini; Kung'amua na kujikita katika unabii na hatimaye, kuishi upya wa maisha unaoletwa na Kristo Yesu.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 55 ya Kuombea Miito Duniani 2018

19/04/2018 07:49

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa 55 wa Kuombea Miito Duniani kwa Mwaka 2018 anakazia mambo makuu matatu: Kusikiliza kwa maskini sauti ya Mungu na kupima mambo kwa mwanga wa imani; pili, kufanya mang'amuzi na kuendelea kujikita katika unabii na hatimaye kuishi upya wa maisha.

Papa Francisko anawataka vijana kutumia karama zao ili kukutana na kuwahudumia maskini pamoja na kujenga uhusiano na Kristo Yesu.

Papa Francisko anawataka vijana wa kizazi kipya kuachana na ubinafsi wao tayari kutumia karama na mapaji yao kukutana na kuwahudumia maskini pamoja na kujenga mahusiano ya pekee na Kristo Yesu.

Vijana tumieni karama zenu kumpenda Yesu na kuwahudumia maskini!

24/03/2018 14:13

Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa kizazi kipya kushinda kishawishi cha ubinafsi na tabia ya kupenda raha kupita kiasi ili kuanza safari ya kukutana na maskini, tayari kuwahudumia kwa kutumia karama na mapaji ya ujana! Wajenge uhusiano na mafungamano mema na Kristo Yesu!

Vijana wanatarajia kuwasilisha hati yao kwa Papa Jumapili ya Matawi, Kanisa linapoadhimisha Siku ya 33 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2018.

Vijana wanatarajia kuwasilisha hati yao kwa Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili ya Matawi, Kanisa linapoadhimisha Siku ya 33 ya Vijana Duniani ngazi ya Kijimbo kwa mwaka 2018.

Sinodi ya Vijana! Hakuna kulala, Jumapili wanawasilisha hati kwa Papa

21/03/2018 16:09

Wawakilishi wa vijana katika maadhimisho ya utangulizi wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana wanaendelea "kuchakarika" ili kuhakikisha kwamba, Jumapili ya Matawi, Siku ya 33 ya Vijana Duniani katika ngazi ya Kijimbo wanawasilisha Hati yao kwa Baba Mtakatifu Francisko tayari kufanyiwa kazi!

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa Siku ya 33 ya Vijana Duniani kwa mwaka 2018 anawataka vijana kuorodhesha mambo yanayowaogofya katika maisha yao!

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa Siku ya 33 ya Vijana Duniani kwa mwaka 2018 anawataka vijana kuorodhesha mambo yanayowaogofya katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 33 ya Vijana Duniani, 2018

21/03/2018 07:08

Usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu, ndiyo kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya Siku ya 33 ya Vijana Duniani ambayo kwa Mwaka 2018 inaadhimishwa katika ngazi ya kijimbo! Baba Mtakatifu anawataka vijana kutoogopa, bali wajizatiti kutaja hofu zinazowasumbua mioyoni!