Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Perù mwaka 2018 inapania kuimarisha mafungamano ya kijamii.

Hija ya Papa Francisko nchini Perù kwa mwaka 2018 inapania kuimarisha mafungamano ya kijamii.

Hija ya Papa Francisko nchini Perù kuimarisha mafungamano ya kijamii

23/09/2017 17:13

Baba Mtakatifu Francisko, mwaka 2018 anatarajia kufanya hija ya kitume inayopania kuimarisha mahusiano na mafungamano ya kidiplomasia kati ya Vatican na familia ya Mungu nchini Perù. Hadi sasa kuna uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, lakini hija ya kitume itayakuza zaidi!

Waamini wanapaswa kukita maisha yao kwenye Injili ya Kristo Yesu, ili waweze kukua na kukomaa katika imani, matumaini na mapendo.

Waamini wanapaswa kukita maisha yao katika Injili ya Kristo Yesu, ili waweze kukua na kukomaa katika imani, matumaini na mapendo.

Kanisa limejengwa katika msingi wa imani ya Mitume wa Yesu!

20/09/2017 07:09

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anawahamasisha kukita maisha yao katika Habari Njema ya Wokovu, ili waweze kukua na kukomaa katika msingi ya imani, matumaini na mapendo kwa Mungu na jirani. Waamini kwa njia ya ushuhuda wao wajitahidi kuzima kiu ya haki na amani kati ya watu!

 

Marehemu Kardinali Velasio de Paolis amesindikizwa kwenye usingizi wa amani!

Marehemu Kardinali Velasio de Paolis amesindikizwa kwenye usingizi wa amani, Jumatatu tarehe 11 Septemba 2017.

Marehemu Kardinali De Paolis amepumzishwa kwenye usingizi wa amani!

12/09/2017 12:43

Kanisa lina amini n akufundisha juu ya Fumbo la Kifo na Ufufuko kutoka kwa wafu! Hii ndiyo imani ambayo Kanisa, Jumatatu, tarehe 11 Septemba 2017 limeishuhudia kwa kumkumbuka, kumwombea na kumsindikiza Marehemu Kardinali Velasio de Paolis kwenye makao ya uzima wa milele!

Kardinali Velasio de Paolis, amefariki dunia, Jumamosi tarehe 9 Septemba 2017 akiwa na umri wa miaka 81. RIP.

Kardinali Velasio de Paolos, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81. RIP.

Tanzia: Kardinali Valasio De Paolis amefariki dunia

10/09/2017 15:43

Kardinali Velasio de Paolis aliyezaliwa kunako mwaka 1935 na kupewa Daraja Takatifu ya Upadre mwaka 1961, akateuliwa kuwa Askofu mkuu mwaka 2003 na hatimaye, Kardinali mwaka 2010 amefariki dunia, tarehe 9 Septemba 2017 akiwa na umri wa miaka 81 na maziko yake ni tarehe 11 Septemba 2017.

 

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko "ang'oa majembe" kuelekea Colombia!

06/09/2017 11:01

Baba Mtakatifu Francisko ameanza hija yake ya kitume ya 20 nje ya Italia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi! Anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika hija hii kwa sala na sadaka zao, ili izae matunda ya amani na upatanisho.

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini na watu wenye mapenzi mema kuondokana na kishawishi cha kutaka kulipa kisasi!

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuondokana na kishawishi cha kutaka kulipiza kisasi na badala yake wajikite katika matendo ya huruma, wema na upendo.

Kardinali Parolin: tendeni wema, msilipize kisasi!

29/08/2017 14:10

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anatambua madhara ya vitendo vya kigaidi katika utu, heshima, ustawi na maendeleo ya binadamu! Aanwataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujikita katika matendo mema na kamwe wasilipe ubaya kwa ubaya!

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua uwepo wa Mungu kati ya maskini.

Kardinali Pietro Parolin anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua uwepo wa Mungu kati ya maskini.

Kardinali Parolin; jitahidini kumwona Mwenyezi Mungu kati ya maskini

28/08/2017 09:03

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujitahidi kumwona Mungu kati ya maskini! Kanisa linataka kuwekeza kwa elimu makini kwa ajili ya vijana na kwamba, kuna haja ya kudhibiti utandawazi kwa kujenga umoja na mshikamano wa dhati!

Ziara ya kikazi ya Kardinali Parolini imepata mafanikio makubwa katika maisha na utume wa Kanisa; Kisiasa na Kidiplomasia!

Ziara ya kikazi ya Kardinali Parolina imepata mafanikio makubwa katika maisha na utume wa Kanisa; katika masuala ya kisiasa na kidiplomasia.

Yaliyojiri katika ziara ya kikazi ya Kardinali Parolin nchini Russia

26/08/2017 10:06

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anasema, ziara yake ya kikazi nchini Russia imekuwa na mafanikio makubwa yanayofumbatwa katika matumaini ya utekelezaji wa mambo msingi yaliyofikiwa katika majadiliano ya kiekumene na viongozi wa Kanisa la Kiorthodox pamoja na kisiasa!