Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson

Kuna uhusiano wa karibu kati ya Ekolojia ya binadamu na mazingira.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya Ekolojia na utunzaji bora wa mazingira.

Kardinali Turkson: Ekolojia ya binadamu inazingatia utu, haki na amani

21/07/2018 15:03

Ekolojia ya binadamu ina uhusiano wa karibu sana na mazingira nyumba ya wote, lakini nafumbatwa katika taratibu, wema, haki, amani, udugu, mshikamano, ibada na uchaji wa Mungu mambo msingi yanayoboresha maisha ya mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

FAO: Mabadiliko ya tabianchi yatakuwa na athari kubwa sana katika uzalishaji kwenye sekta ya uvuvi duniani.

FAO: Mabadiliko ya tabianchi yatakuwa na athari kubwa sana katika sekta ya uvuvi duniani ifikapo mwaka 2050.

Mabadiliko ya tabianchi yataathiri sana sekta ya uvuvi duniani, 2050

13/07/2018 16:52

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa linasema, kwamba, kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ifikapo mwaka 2050, sekta ya uvuvi duniani itakuwa imeathirika kwa asilimia 5.3% kutoka katika asilimia 2.8% kwa sasa na waathirika wakubwa ni maskini kutoka nchi changa duniani!

Viongozi wa kidini nchini Kenya wanasema, saratani ya rushwa inawapekenya sana wananchi inapaswa kutangazwa kuwa ni janga la kitaifa.

Viongozi wa kidini nchini Kenya wanasema, rushwa na ufisadi unawapekenya sana wananchi wa Kenya na inapaswa kutangazwa kuwa ni janga la kitaifa!

Viongozi wa Kidini Kenya wasema, rushwa ni janga la kitaifa!

13/07/2018 16:03

Viongozi wa kidini nchini Kenya wanasema, rushwa na ufisadi umewapekenya wananchi wa Kenya kiasi kwamba, imekuwa kama saratani inayoendelea kusababisha majanga katika maisha ya wananchi wengi! Wanamwomba Rais Kenyatta kutangaza kuwa sasa rushwa ni janga la kitaifa!

Jumapili ya Utume wa Bahari: Kanisa limewakumbuka mabaharia, wavuvi na familia zao kutokana na matatizo, changamoto na mchango wao katika uchumi.

Jumapili ya Utume wa Bahari: Kanisa limewakumbuka na kuwaombea mabaharia, wavuvi pamoja na familia zao kutokana na changamoto, matatizo na mchango wao katika kukuza uchumi fungamani.

Utume wa Bahari: Mateso, changamoto na mchango wa mabaharia na wavuvi

09/07/2018 15:01

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jumapili ya Utume wa Bahari amewakumbuka na kuwaombea: mabaharia, wavuvi pamoja na familia zao, lakini zaidi wale wanaoishi na kufanya kazi katika mazingira magumu na tete; wanaokabiliwa na ghasia pamoja na uharamia baharini!

Nishati mpito na utunzaji bora wa mazingira ni mjadala unaojikita katika umuhimu, changamoto, hatari na mbinu mkakati wa kuendeleza nishati rafiki!

Nishati mpito na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni mjadala unaopania kupembua umuhimu, fursa, changamoto, sera na mikakati ya nishati bora zaidi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya binadamu.

Umuhimu wa nishati mpito, changamoto na fursa za maendeleo endelevu!

09/06/2018 16:18

Nishati mpito na utunzaji wa mazingira nyumba ya wote: mjadala kuhusu hatari, fursa, changamoto na njia muafaka za utekelezaji ni mambo msingi yaliyojadiliwa kwenye kongamano la kimataifa lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu na Nostre Dame.

Fedha inapaswa kuwa ni kipimo na kikolezo cha huduma na maendeleo endelevu ya binadamu na wala si vinginevyo!

Fedha inapaswa kuwa ni kipimo na kikolezo cha huduma na maendeleo endelevu ya binadamu!

Mang'amuzi ya kimaadili kuhusu mfumo wa uchumi na fedha duniani

08/06/2018 14:36

Waraka kuhusu "Mang'amuzi ya kimaadili kuhusu mfumo wa uchumi na fedha" uliotolewa hivi karibuni mjini Vatican unabainisha umuhimu wa fedha kama chombo cha huduma ya maendeleo endelevu; utu na heshima ya binadamu na wala si mtawala wala chombo cha kunyanyasia watu!

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia kwa mwaka 2019 itaongozwa na kauli mbiu "Amazonia: Njia Mpya ya Kanisa na kwa ajili ya Ekolojia Endelevu".

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia itaongozwa na kauli mbiu "Amazonia: Njia Mpya ya Kanisa na kwa ajili ya Ekolojia Endelevu".

Sinodi ya Amazonia: Njia mpya ya Kanisa kwa ajili ya ekolojia endelevu

09/04/2018 14:50

Baba Mtakatifu Francisko analitaka Kanisa kujikita katika masuala ya haki, amani na mshikamano; utume na huduma ya upendo, ili kuhakikisha kwamba, Injili ya Kristo inatamadunishwa katika uhalisia wa maisha ya wananchi wa Amazonia, ili Kanisa liweze kupaya sura mpya ya watu wa Amazonia!

Papa Francisko ni shuhuda wa majadiliano ya kiekumene yanayowawezesha Wakristo kutembea, kusali na kufanya kazi kwa umoja kwa ajili ya huduma!

Papa Francisko ni shuhuda na chombo cha majadiliano ya kiekumene kinachowawezesha Wakristo kutembea, kusali na kufanya kazi katika umoja kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia.

Papa Francisko ni shuhuda wa majadiliano ya kiekumene katika huduma

13/03/2018 07:47

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Machi 2018 anaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 5 tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kwa kulitaka Kanisa kujielekeza zaidi katika: huduma kwa maskini kama amana na utajiri wa Kanisa; Amani na Utunzaji Bora wa Mazingira bila kusahau Uekumene!