Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kardinali Giovanni Angelo Becciu

Rais Sergio Mattarella amewapongeza Makardinali wapya kutoka Italia kwa dhamana na utume waliokabidhiwa na Papa Francisko.

Rais Sergio Mattarella amewapongeza Makardinali wapya kutoka Italia walioteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko.

Rais Sergio Mattarella awapongeza Makardinali wapya kutoka Italia

11/07/2018 16:44

Rais Sergio Mattarella wa Italia amewapongeza Makardinali wapya waliotoka nchini Italia kwa dhamana na wajibu mkubwa waliokabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwa washauri wake wa karibu katika kuongoza, kutakatifuza na kuwafundisha watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia!

Makardinali ni wasaidizi na washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Makardinali ni wasaidizi na washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Makardinali wapya 14 wanatumwa kutangaza upendo wa huruma ya Mungu!

28/06/2018 08:56

Makardinali ni washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro katika maisha na utume wa Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 28 Juni 2018 anawasimika Makardinali wapya 14 kati yao Makardinali wawili wameteuliwa kutokana na kujipambanua kwao katika maisha na utume wao kwa Kristo na Kanisa lake!

 

Tangu sasa, Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican itajulikana kama Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Tangu sasa, Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican itajulikana kama Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Baraza la Kipapa la Mawasiliano!

23/06/2018 17:10

Baba Mtakatifu Francisko ameamua kwamba, Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican kuanzia sasa itambulikane kama "Baraza la Kipapa la Mawasiliano" linalounganisha: Radio Vatican, Kituo cha Televisheni cha Vatican pamoja na Gazeti la L'Osservatore Romano na hivyo kuunda "Vatican Media".

 

Kardinali mteule Becciu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu.

Kardinali mteule Giovanni Angelo Becciu ametangazwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, kuanzia mwezi Agosti, 2018.

Kardinali mteule Becciu, kuongoza Baraza la Kipapa la Watakatifu

26/05/2018 16:22

Kardinali mteule Giovanni Angelo Becciu aliyezaliwa mwaka 1848, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mwaka 1972; akateuliwa na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu mwaka 2001; akatumikia sehemu mbali mbali kama Balozi wa Vatican; sasa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la watakatifu.