Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Roma

Jumuiya ya Mt. Egidio imekuwa mstari wa mbele katika majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni kwa kuwekeza katika afya na elimu.

Jumuiya ya Mt. Egidio imekuwa mstari wa mbele katika majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni kwa kuwekeza zaidi katika maboresho ya sekta ya elimu na afya kwa njia ya Mradi wa "The DREAM na BRAVO".

Jubilei ya Miaka 50 ya Jumuiya ya Mt. Egidio: Amani, Afya na Elimu!

13/02/2018 10:34

Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani anasema, katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imejipambanua katika kukuza na kudumisha mchakato wa majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni; kwa kujikita katika maboresho ya afya na elimu pembezoni mwa jamii!

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwak mwaka 1968.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kunako mwaka 1968.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inajikita katika Neno, Maskini na Amani

12/02/2018 09:59

Baba Mtakatifu Francisko anasema, maisha na utume wa Kanisa yanafumbatwa katika. Kusoma, Kulitafakari na Kumwilisha Neno la Mungu katika maisha; Pili ni Ushuhuda wa Injili ya upendo inayomwilishwa katika huduma makini kwa maskini sanjari na kujikita katika kutafuta, kukuza na kudumisha amani!

Katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Jumuiya ya Mt. Egidio imejikita katika: Sala, Maskini na Amani duniani.

Katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imejikita katika: Sala. Maskini na Amani duniani.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 ya Utume

09/02/2018 17:02

Tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yenye Makao yake makuu mjini Roma, hapo tarehe 7 Februari 1968 imeendelea kutekeleza dhamana na wajibu wake kwa kujikita katika maisha ya sala, huduma makini kwa maskini pamoja na mchakato wa kutafuta na kudumisha amani duniani!

 

Patriaki Hilarion wa Urusi ameandika matashi mema kwa Jumuiya ya Mt. Egidio katika maadhimisho ya dhahabu tangu kuanzishwa kwake

Patriaki Hilarion wa Urusi ameandika matashi mema kwa Jumuiya ya Mt. Egidio katika maadhimisho ya dhahabu tangu kuanzishwa kwake

Ujumbe wa Pariaki Hirarion kwa Jubilei ya dhahabu ya Jumuiya ya Mt. Egidio

02/02/2018 15:24

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,katika nusu karne imeweza kugeuka kuwa Jumuiya kubwa ya walei wanaunganisha maelfu ya watu nchini Italia,Ulaya na ulimwengu mzima.Ni maneno ya Patriaki Hilarion wa Volokolamsk Urusi katika barua ya matashi mema kwa tukio miaka 50 ya Jumuiya hiyo

 

 

 

Jumuiya ya Mt.Egidio katika harakati za kusaidia maskini,wazee na wenye shida ili washiriki meza ya Sikuu ya kuzaliwa kwa Bwana

Jumuiya ya Mt. Egidio katika harakati za kusaidia maskini, wazee na wenye shida ili washiriki Meza ya Sikuu ya kuzaliwa kwa Bwana

Jumuiya ya Mt.Egidio:Ongeza kiti mezani siku ya Kuzaliwa kwa Bwana!

13/12/2017 15:43

Kusheherekea Krismasi na maskini,wasiokuwa na makazi,familia zenye shida na wazee ndiyo lengo la Jumuiya ya Mt.Egidio kuandaa chakula cha mchana tarehe 25 Desemba 2017.Na ndiyo maana ya kampeni ya kukusanya fedha yenye kauli mbiu,Ongeza kiti mezani siku ya Krismasi mwezi Desemba 

.

 

Mkataba usio na malipo wa hospitali ya Mtakatifu Camillo na Jumuiya ya Mt. Egidio, ni habari njema kwa maelfu ya wagonjwa kutoka Afrika

Mkataba usio na malipo wa hospitali ya Mtakatifu Camillo na Jumuiya ya Mt. Egidio, ni habari njema kwa maelfu ya wagonjwa kutoka Afrika na pia Afrika yenyewe

Sahini ya Jumuiya ya Mt.Egidio na Hospitali ya Mt. Camillo wa ajili ya Afrika

07/10/2017 14:14

Sahini ya Jumuiya ya Mt.Egidio na Hospitali ya Mt. Camillo kwa ajili ya Afrika, ni mkataba usio na malipo kwa maelfu ya wagonjwa kutoka Afrika.Wataweza kwenda kupata ushauri wa kiafya  kwa ngazi ya juu na hata katika hali ngumu ya umasikini au ukosefu wa  zana kwa ajili ya utafiti zaidi wa afya.

 

Kunako Mwaka 1986 Papa Yohane Paulo II alianzisha Siku ya Kuombea Amani Duniani, huko Assisi, Italia.

Kunako Mwaka 1986 Papa Yohane Paulo II alianzisha Siku ya Kuombea Amani Duniani, tukio ambalo walau kila mwaka linawakutanisha viongozi wa dini mbali mbali ili kusali kwa pamoja kuombea amani duniani.

Maandalizi ya Kumbu kumbu ya Miaka 30 ya Roho ya Assisi yapamba moto!

06/07/2017 14:58

Waamini wa dini mbali mbali wanahamasishwa kusimama kidete, kulinda, kutetea na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu! Mtakatifu Yohane Paulo II, miaka 30 iliyopita, aliwakutanisha viongozi mbali mbali wa kidini kwa ajili ya kuombea amani duniani. Hii ni changamoto endelevu!

Zakumbukwa roho za marehemu wahamiaji

Zakumbukwa katika mkesha wa sala wa Jumuiya ya Mt. Egidio, roho za marehemu wahamiaji

Wakumbukwa wahamiaji waliofariki katika safari ya matumaini

23/06/2017 14:37

Jumuiya ya Mt. Egidio yafanya mkesha wa sala siku ya Alhamisi, tarehe 22 Juni 2017, kuwakumbuka wahamiaji marehemu, waliopoteza uhai wao wakati wa safari ya matumaini kupata hifadhi barani Ulaya. Padre Marco Gnavi, awaalika waamini barani Ulaya kudumu katika mshikamano na ukarimu.