Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Jumapili ya V ya Kwaresima

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni kielelezo cha: huruma, upendo na maisha mapya!

19/03/2018 09:54

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa mateso na kifo cha Mwana mpendwa wa Mungu, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa binadamu wa nyakati zote! Kwa njia ya Madonda yake Matakatifu watu wameponywa!

Mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu ni kielelezo cha utii; upatanisho na chemchemi ya maisha mapya!

Mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu ni kielelezo cha utii na uhuru kamili; upatanisho kati ya Mungu na binadamu na chemchemi ya maisha mapya!

Kifo cha Kristo ni kielelezo cha utii, upatanisho na uhai mpya!

17/03/2018 08:56

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya tano ya Kipindi cha Kwaresima ni mwaliko kwa waamini kutafakari kwa kina na mapana kuhusu Fumbo la Msalaba hasa mateso na kifo cha Kristo Yesu, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha utii, upatanisho kati ya Mungu na binadamu na chemchemi ya maisha mapya!

Kristo Yesu kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake ameanzisha Ufalme wa Mungu unaoangaza macho ya watu kwa maneno, kazi na uwamo wake.

Kristo Yesu kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake ameanzisha Ufalme wa Mungu unaoangaza macho ya watu kwa neno, kazi na uwamo wa Kristo.

Vueni utu wa kale uliochakaa kwa dhambi kwa kujivika utu mpya!

14/03/2018 11:50

Mama Kanisa anafundisha kwamba, Kristo Yesu alianzisha Ufalme wa mbinguni hapa duniani, unaangaza macho ya watu kwa neno, kazi na uwamo wa Kristo. Kanisa ni mbegu na mwanzo wa Ufalme, kielelezo cha utii na sadaka ya Kristo Yesu katika kazi ya ukombozi wa mwanadamu!

Yesu akiinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake, kielelezo cha utii na utimilifu na mwanzo wa Agano Jipya na la milele!

Kristo Yesu akiinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha utii kwa Baba yake wa mbinguni, mwanzo wa Agano Jipya na la milele.

Kristo Yesu akishakuinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake!

13/03/2018 14:46

Saa ya Kristo Yesu kadiri ya mafundisho ya Mwinjili  Yohane ni Fumbo la Pasaka, yaani: Mateso, Kifo na Ufufuko wa Kristo unaomkirimia mwanadamu ukombozi. Hiki ni kielelezo cha hali ya juu kabisa cha Utii kwa Baba yake wa milele na utimilifu wa Agano Jipya na la Milele linalofumbata Sadaka yake!

 

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wa Jimbo Katoliki Carpi kuwa ni mashuhuda wa Injili ya maisha, matumaini na mshikamano!

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wa Jimbo Katoliki la Carpi, Italia kuwa ni mashuhuda wa Injili ya maisha, furaha na matumaini ili kuweza kukabiliana na changamoto za maisha!

Ziara ya Papa Francisko Jimboni Carpi, Italia

02/04/2017 14:18

Baba Mtakatifu anawakumbusha waamini kwamba, matatizo na changamoto mbali mbali ni sehemu ya maisha, lakini kwa kumfuasa Kristo kwa dhati, wataweza kukirimiwa uthabiti wa maisha kwani Kristo Yesu ni ufufuo na uzima; ni chemchemi ya furaha na faraja ya moyo; ni amani na utulivu wa ndani!

 

Mwanadamu anatenda dhambi huyo amekufa kiroho!

Mwanadamu anatenda dhambi na kutembea katika giza la mauti, amekufa kiroho!

Imani katika Ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo!

31/03/2017 15:48

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya tano ya Kipindi cha Kwaresima ni mwaliko wa kutafakari tena madhara ya dhambi ambayo yamepelekea kifo sanjari na upendo wa huruma ya Mungu unaojionesha kwa mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu, kiini cha imani na amana ya Kanisa katika uzima wa milele.

Ufufuko wa wafu na uzima wa milele ni sehemu ya imani na matumaini ya Kikristo yanayopata mwanga katika Fumbo la Pasaka!

Ufufuko wa wafu na uzima wa milele iyajo ni sehemu ya imani na matumaini ya Kikristo yanayopata mwanga kutoka katika Fumbo la Pasaka yaani, mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu!

Yesu ni njia, ukweli, uzima na ufufuo kwa wale wanaomwamini!

29/03/2017 16:01

Maana ya Kikristo ya kifo imefunuliwa katika mwanga wa Fumbo la Pasaka yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu ambamo ndani mwake waamini wanapata chemchemi ya tumaini katika maisha ya uzima wa milele. Mkristo anayefariki dunia "huuachamwili na kujiunga na Mungu".

 

Yesu Kristo ni Hakimu mwenye haki anayetetea uhai na kutoa nafasi kwa mdhambi kutubu na kumwongokea tena Mungu!

Yesu Kristo ni Hakimu mwenye haki anayetetea Uhai na kutoka nafasi kwa mdhambi kutubu na kumwongokea Mungu kwani haki ya Mungu ni huruma yake!

Vitimbwi Mahakamani! Patashika nguo kuchanika!

11/03/2016 08:25

Waswahili husema eti mfungwa hachagui gereza! Leo Yesu anajipambanua kuwa ni Hakimu mwenye haki anayetetea sheria ya Mungu iliyoandikwa katika akili na nyoyo za watu! Anawafunuliwa wadhambi na wakosefu haki ya Mungu ambayo ni huruma yake! Kiini na muhtasari wa imani ya Kikristo!