Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Jumapili IV ya Kwaresima

Yesu Kristo aliteswa  na kufa Msalabani ili kuwakomboa wanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Kristo Yesu aliteswa na kufa Msalabani ili kuwaokomboa watu kutoka katika lindi la dhambi na mauti.

Kwaresima ni kipindi cha mapambano dhidi ya dhambi na mauti!

10/03/2018 06:30

Kristo Yesu hana budi kuinuliwa ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye. Fumbo la Umwilisho linalopata utimilifu wake katika Fumbo la Pasaka linalenga kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti! Kristo ni mpatanishi kati ya Mungu na binadamu na kati yao wenyewe!

Hekima ya Mungu inafumbatwa katika nguvu ya Msalaba wa Kristo Yesu!

Hekima ya Mungu inafumbatwa katika nguvu ya Msalaba wa Kristo Yesu.

Huruma ya Mungu ni muhtasari wa historia ya ukombozi!

09/03/2018 17:08

Kanisa linaungama na kufundisha kwamba, "kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili wokovu wetu" Yesu aliteswa, akafa Msalabani na hatimaye akafufuka siku ya tatu kadiri ya Maandiko Matakatifu, ili kuwapatanisha watu na Baba yake wa mbinguni. Kristo Yesu ni ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu!

 

Waamini wanahamasishwa kushuhudia imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa kutembea katika mwanga wa Pasaka!

Waamini wanahamasishwa kushuhidia imani yao kwa Kristo na Kanisa lake kwa kutembea katika mwanga wa Pasaka!

Shuhudieni imani yenu kwa matendo ya mwanga, alama ya maisha mapya!

08/03/2018 16:13

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya Nne ya Kipindi cha Kwaresima ni mwaliko wa kumshuhudia zawadi ya imani kwa njia ya matendo ya mwanga, kwa kutembea katika mwanga wa Kristo, kwani kwa njia ya Ubatizo wamezaliwa upya kwa maji na Roho Mtakatifu, kielelezo cha huruma na upendo wa Mungu.

Yesu ni mwanga wa mataifa, waamini wanahamasishwa kufungua macho ya imani yao, ili kumshuhudia kwa watu wa mataifa!

Yesu ni mwanga wa mataifa, waamini wanahamasishwa kufungua macho yao ya imani ilikumwona Yesu mwanga wa mataifa, kumkiri na kumshuhudia kati ya watu wa mataifa!

Fungueni macho yenu ya imani ili kumwona Yesu Mwanga wa Mataifa!

25/03/2017 15:23

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Kwaresima ni mwaliko wa kufungua masikio ili kuweza kulisikia Neno la Mungu likitangazwa na kushuhudiwa; kuungama imani kwa midomo yao kwamba, Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliye hai na kumshuhudia Kristo mwanga wa mataifa!

Upofu wa imani unawazuia waamini kuona kama aonavyo Mungu na hivyo kushindwa kumuungana na kumshuhudia katika maisha!

Upofu wa imani unawazua waamini kuona kama aonavyo Mwenyezi Mungu na kushindwa kumshuhudia katika medani mbali mbali za maisha!

Furahini katika Bwana kwani amewafumbua macho ya imani na ushuhuda!

23/03/2017 13:30

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Kwaresima, ni mwaliko kwa waamini kufurahi katika Bwana, kwani amewaondoa kutoka kwenye upofu wa imani, akawajalia mwanga wa kuona matendo makuu ya Mungu katika maisha yao, sasa wanatumwa kumkiri na kumshuhudia Kristo Yesu!

Waamini wanaalikwa kumwomba Mungu afungue macho ya imani ili waweze kumwona Yesu, Mwanga wa Mataifa na kumshuhudia kwa watu!

Waamini wanaalikwa kumwomba Mungu awafungue macho kwa mwanga wa Roho Mtakatifu ili waweze kumwona Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, mwanga wa mataifa, tayari kumshuhudia katika medani mbali mbali za maisha.

Kipofu akutana mubashara na Yesu, asimulia yaliyomsibu!

22/03/2017 14:18

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Kwaresima, inayojulikana pia kuwa ni Jumapili ya furaha, inatoa changamoto kwa waamini kumtafuta Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa ili aweze kuwasaidia kuona matendo makuu ya Mungu na kuyatolea ushuhuda wenye mvuto na mashiko!

 

Iweni na huruma kama Baba!

Iweni na huruma kama Baba!

Iweni na huruma kama Baba!

04/03/2016 15:54

Injili ya Baba mwenye huruma ni kiini cha tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu, ambamo waamini waalikwa kutubu na kumwongokea Mungu, ili waweze kuonja huruma, upendo na msamaha wake wa daima! Iweni na huruma kama Baba

 

Iweni na huruma kama Baba Yenu wa mbinguni!

Iweni na huruma kama Baba yenu wa mbinguni!

Hapa ni mnuso kwenda mbele! Mwenye roho ya kwanini atajiju mwenyewe!

04/03/2016 15:34

Iweni na huruma kama Baba aliyethubutu kumkimbilia mwana mpotevu, akambusu ili kumwonesha upendo; akamvika vazi jipya, kumnrudishia utu wake unaofumbata sura na mfano wa Mungu; akamvita pete, alama ya uaminifu na viatu miguuni ili atembee katika njia ya haki na salama!