Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Juma la Amani Nchini Colombia, 2017

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi mbali mbali wa dunia wakati akirejea mjini Vatican.

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wa nchi na wakuu wa Serikali wakati akirejea mjini Vatican, Jumatatu, tarehe 11 Septemba 2017.

Papa Francisko: Salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi na serikali

11/09/2017 14:07

Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea kutoka Colombia kwa hija yake ya kitume, ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi na Serikali ya: Colombia, Netherland, Marekani, Ureno, Hispania, Ufaransa na Italia. Amewashukuru wananchi wa Colombia kwa mapokezo makubwa!

Liturujia ya Upatanisho wa Kitaifa nchini Colombia ni tukio lililowagusa wengi!

Liturujia ya Upatanisho wa Kitaifa nchini Colombia tarehe 8 Septemba 2017 ni tukio liliwagusa wananchi wa Colombia kutoka katika undani wa maisha yao!

Yaliyojiri kwenye Ibada ya Upatanisho wa Kitaifa nchini Colombia

09/09/2017 16:21

Baba Mtakatifu Francisko anasema, ametamani sana kupata nafasi ya kulia, kusali na kuomba msamaha na familia ya Mungu nchini Colombia kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa amani na upatanisho, tayari kuanza ukurasa mpya unaosimikwa katika umoja, udugu na mshikamano wa kitaifa!

Papa Francisko anawataka wananchi wa Colombia kujipatanisha na Mungu na jirani zao, kukubali ukweli, kutubu na kuongoka!

Papa Francisko anawaka wananchi wa Colombia kujipatanisha na Mungu, Jirani na Mazingira! Kukubali ukweli ili kupokea na kutoa msamaha!

Tafakari ya Papa Francisko katika Liturujia ya Upatanisho wa Kitaifa

09/09/2017 14:07

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwaalika watu wa Mungu nchini Colombia kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao! Wasiogope ukweli na haki; kupokea na kutoa msamaha; kujipatanisha; kwa kujikita katika toba na wongofu wa ndani ili kujenga na kudumisha amani, haki, utu na heshima ya binadamu.

Papa Francisko amewasili nchini Colombia tayari kuanza hija ya amani na upatanisho kati ya watu wa Colombia!

Baba Mtakatifu Francisko amewasili nchini Colombia tayari kuanza hija ya amani na upatanisho miongoni mwa wananchi wa Colombia!

Baba Mtakatifu Francisko "atinga timu" nchini Colombia!

07/09/2017 12:16

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wananchi wa Colombia kuwa ni mashuhuda wa furaha na matumaini na kamwe wasiwaruhusu wajanja wachache kuwapoka furaha yao; wajielekeze sasa katika mchakato wa haki, amani na maridhiano yanayofumbatwa katika msamaha na upatanisho wa kweli!

Papa Francisko akiwa njiani kuelekea Colombia ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi alimopitia!

Papa Francisko akiwa njiani kuelekea nchini Colombia ametuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi alimopitia.

Papa Francisko atuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi

06/09/2017 14:26

Baba Mtakatifu Francisko katika hija yake ya kitume kuelekea nchini Colombia Jumatano tarehe 6 Septemba 2017 ametuma sala na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi akiwatakia heri, baraka, ustawi, maendeleo na amani! Kwa namna ya pekee amewakumbuka wananchi wa Venezuela!

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko "ang'oa majembe" kuelekea Colombia!

06/09/2017 11:01

Baba Mtakatifu Francisko ameanza hija yake ya kitume ya 20 nje ya Italia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi! Anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika hija hii kwa sala na sadaka zao, ili izae matunda ya amani na upatanisho.

Upatanisho: Mapadre 40 waliuwawa kati ya mwaka 1987 hadi mwaka 2003; Makanisa 63 kuchomwa moto katika kipindi hiki.

Upatanisho: Mapadre 40 waliuwawa nchini Colombia kati ya Mwaka 1987 hadi mwaka 2004; Makanisa 63 kuchomwa moto.

Mada zinazoongoza hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Colombia!

05/09/2017 12:26

Baraza la Maaskofu Katoliki Colombia linasema, hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Colombia inaongozwa na mada zifuatazo: Upatanisho, haki na amani; Injili ya uhai na familia; Ufuasi, Umisionari na utume unaowasukuma Wakristo kuwa ni vyombo na mashuhuda wa uinjilishaji wa kina!